Bei ya Dizeli na Mafuta ya Taa zapanda huku bei ya Petroli ikipungua kwa mwezi Machi, 2019

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,402
Watumiaji wa dizeli na mafuta ya taa nchini watatumia fedha nyingi zaidi kupata bidhaa hiyo mwezi huu huku watumiaji wa petroli wakitabasamu kutokana na mabadiliko ya bei ya ukomo kwa bidhaa za petroli zilizotangazwa leo Jumanne, Machi 5, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaeleza bei ya rejareja kwa dizeli imeongezeka kwa Sh51 kwa lita sawa na ongezeko la asilimia 2.44 na mafuta ya taa Sh50 kwa lita sawa na asilimia 2.47.

Hata hivyo bei ya petroli imepungua kwa Sh23 kwa lita sawa na asilimia 1.07 ikilinganishwa na bei ya mwezi uliopita. Bei hizo zinaanza kutumika rasmi kesho.

“Mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la ndani yanatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia pamoja na gharama za usafirishaji (BPS Premium),” ilieleza taarifa hiyo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
dora imeshuka samani


kila jumatano ya kwana ya mwezi bei z mafuta hubadilika kwa tangazo lnalitolewa jumanne,hizi bei mpya zitanza kutumika usiku saa sita
 
Taarifa ya February ilisema Tanga bei haitashuka kwa sababu waagizaji walikuwa na mzigo mkubwa. Lakini hii ya March iliyoongezeka kwenye dizeli na mafuta ya taa nina hakika bei itaongezeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom