Bei ya daladala yapaa juu, toka maeneo ya Mbezi, Kimara, Korogwe kwenda Kariakoo ni shilingi 1000, nani amepanga bei hii?

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,502
6,403
Habari JF,

Hakika hii imenishtua sana baada ya kuona bei ya daladala zinazofanya safari ndani ya jiji la dar es salaam kupandisha bei ya nauli kimyakimya au naweza kusema kinyemera pasipo kuutarifu umma

Kwa sasa usafiri kutoka mbezi, kimara kuelekea city center si tatizo tena kwani coaster zimeruhusiwa za kutosha baada ya kuona mwendokasi umezidiwa na uwingi wa abiria wanaoelekea katikati ya jiji, hili ni jambo jema na limerahisisha usafiri hapa mtu anachagua mwwenyewe atumie mwendokasi au daladala

Shida imekuja katika issue ya nauli, kutoka mbezi mpaka kariakoo bei ni shilingi 1000, hii haingalii umepandia gari kimara wala korogwe na baruti wote bei ni hiyo

Hapa mjini kuna daladala zinatembea route ndefu sana lakini nauli zake hazijawahi kufikia kiwango cha 1000, chanika to kariakoo ni 750. mbezi mwisho to temeke ni 750, mbagala to kawe ni 750, makumbusho bunju ni 750
hii route ya mbezi kariakoo inauspecial gani mpaka bei yake iwe 1000?

Ni nani amehusika kupanga bei hii kubwa inayoumiza wananchi bila kujali kwamba gharama za mafuta zimepungua na umbali si mrefu kiasi iko?

Ni kwanini gari zinazopita route hii hazijabandika bei?

Tunaomba mamlaka husika zamani mlikua mnaitwa SUMATRA sasa ni LATRA mlifanyie kazi swala hili

Wananchi wanyonge ndio wanaoumia
 
Lipa mzee, level seat hizo.

Na buku imekuwaje wewe? Me naona bado ni nafuu. Kimara mpaka kariakoo duh lipa tu
 
Aisee kiongozi tuache na maisha yetu maana tumeongea tumechoka hawa Trafik wamefanya hii nchi ni yao. Kuna zile daladala za simu 2000 makumbusho. Siku hizi ni Mbezi Mawasiliano na hakuna kushikwa. Kariakoo na 1000
 
Kwani mbezi- kariakoo na mwendokasi sh ngapi? Labda ndo nauli walopangiwa ili abiria wa mwendokasi wasikimbie😂😂
 
Back
Top Bottom