Bei mpya za uchimbaji wa visima, ground water survey na pump installation

Mr.Mak

JF-Expert Member
Feb 23, 2011
2,832
2,000
Habari wana jf.Natumai ni wazima wa afya,sisi ni vijana wajasiliamali tunaojihusisha na masuala yahusuyo uchimbaji wa visima vya maji.
Ili uwe na kisima chako cha maji ni lazima kuna baadhi ya hatuwa itakubidi uzifuate.Nazo hatua hizo ni kama nilivyo ziainisha hapo chini,
1. Itakubidi uchimbe kisima (kizuri ni cha kuchimba na mashine sio na mikono)
2. Kisima chako itabidi kiwekwe casing (pvc[screen and plane])
3. Pia itatakiwa kiwekwe Graves
4. Kisha itawekwa pump iliyounganishwa na waya ulioyoka kwenye control box na pia pampu iliyoonganishwa na poly pipe kwa ajili ya kupitisha maji
5. Pia pump lazima ifungwe na kamba,mara nyingi tunapenda kutumia kamba za Manila kwa sababu ni imara na pia ni ngumu kuoza.
6. Baada ya hapo maji yatapandishwa kisha yatachukuliwa sample yake ili yakapimwe kama ni salama kwa matumizi ya binaadamu,mifugo au mimea

Nb. Kabla ya kufunga pampu kisima kina takiwa kiflashiwe ili kiachwe kikiwa kipo safi kabisa.

Hizo zote ni baadhi ya huduma ambazo pia tunazitowa,japokuwa kuna baadhi ya huduma kama kupima maji bado hatujaanza kutoa hiyo huduma, ila kama mteja atataka tumsaidiye kufanya hiyo huduma tutamsaidia kupitia kwa watu wengine.

Bei/gharama zetu za huduma:

Kuchimba kisima tunachimba kwa shillingi elfu sitini (60000) kwa mita moja hii ni bei kwa walioko Dar es salaam
Kwa walioko nje ya dar es salaam tutakubaliana kutokana na mkoa mteja alipo.
Na kwa bei hiyo tajwa hapo juu ni pamoja na usafili na ufungaji wa pampu unakuwa juu yetu.

Mfano: uchimbaji wa kisima cha mita 90 gharama yake ni...
Mita 1 = 60000 tsh
Mita 90 = y
Cross multiplication
Mita 90 × 60000 tsh/mita 1y
Cut Mita both side
90 × 60000tsh/1
5400000tsh
Kwa hiyo gharama za kuchimba kisima cha mita 90 ni shillingi millioni tano na laki nne...gharama hizo ni pamoja na pampu.
Hapo mteja atatakiwa kununuwa maji yatakoyohitajika katika uchimbaji wa kisima na maji hayo yana uzwa tanki moja la lita elfu moja ni shillingi elfu kumi na tano.

Gharama/bei za ground water survey...
Kwa suala la upimaji wa uwepo wa maji tunachaji shillingi 250000 kwa mkazi wa dar es salaam, kwa mteja aliyepo nje ya dar es salaam tunaaanziya kuchaji shillingi laki tano lakini itategemea na mteja alipo.

Njia ya malipo:
Malipo ya ufanyaji wetu wa kazi huwa tunafanya tunapokuwa tupo site, tukishafika site kwa mara ya kwanza pamoja na vifaa vyetu vyote kwa ajili ya kuanza kazi hapo itabidi mteja atowe asilimia 65 ya gharama nzima.Ambayo hela hizo ndizo itakazo tumika kununulia vifaa vya kisima.

Mahali tulipo:
Offisi zetu zipo morogoro wilaya ya kilosa lakini baadhi ya vifaa vyetu vipo Dar es salaam kwa hiyo mteja akituhitaji kama yupo dar es salaam tunaweza kumfanyia kazi kwa gharama zetu za usafili na malipo yatafanyika tutakapo fika site tukiwa na vifaa vya uchimbaji.

Mawasiliano:
Piga simu namba 0628080096
Karibuni nyoote tuwahudumie
subirini waziri wa maji na sawasco watusambazie maji mazuri muone kama hamtotupigia magoti.. Ipo siku mtachimba meter 1 kwa elf 10. Mnatumia udhaifu wa wizara ya maji kutosambaza maji nanyi mnatunyonya sana wananchi. Siku zenu Zinahesabika za kutupiga mibei yenu hiyo
 
tawa driller

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
296
250

Mkuu bei inapangwa kutokana na gharama za utendaji...
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,683
2,000
Ikitokea umechimba na maji yakatoka sio salama kwa binadamu, je hela inarudi au
 
Olumolongez

JF-Expert Member
Dec 19, 2015
824
500
Ni rahisi kujua aina ya maji kama ni ya baridi au chumvi kabla ya kuanza kuchimba kisima?
 
Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,483
2,000
Mkuu mm nahitaji huduma hii ila ni kijijni, kijiji ni kilimahewa wilaya mkuranga mkoa wa pwani, kijiin kwetu hakuna umeme je nitayavuta vipi maji kutoka kwenye kisima? Niambie garama kiasi gan kwa mkadirio na ushaur mwingine unaofaa maana nimeanzisha mradi wa kufuga kule kwa hyo nahitaji maji sana
 
Ok kwa maeneo ya mkuranga maji unapata mpaka mita mia ila huwezi kuzid hapo ila znaweza kupungua huu ni kwa uzoefu wangu wa maeneo ya hapo mkuranga mjini sasa sijuwi huko kilimahewa kuna umbali gani kuyoka mkuranga mjini kwa tabia ya eneo linawezakubadilika au pia yakafanaa kikubwa unaweza uka quote estimation zangu au ukafanya ground water survey. Kuhusu suala la kuvuta maji na huna umeme unaweza kutumia other sources of energy kama solar power au genereta that's your option brother.
 
tawa driller

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
296
250
Mkuu mm nahitaji huduma hii ila ni kijijni, kijiji ni kilimahewa wilaya mkuranga mkoa wa pwani, kijiin kwetu hakuna umeme je nitayavuta vipi maji kutoka kwenye kisima? Niambie garama kiasi gan kwa mkadirio na ushaur mwingine unaofaa maana nimeanzisha mradi wa kufuga kule kwa hyo nahitaji maji sana
Kwa makadirio ya juu hapo ni kama shillingi Millioni sita na nusu mkuu
 
Fikra Angavu

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
301
225
Habari wana jf.Natumai ni wazima wa afya,sisi ni vijana wajasiliamali tunaojihusisha na masuala yahusuyo uchimbaji wa visima vya maji.
Ili uwe na kisima chako cha maji ni lazima kuna baadhi ya hatuwa itakubidi uzifuate.Nazo hatua hizo ni kama nilivyo ziainisha hapo chini,
1. Itakubidi uchimbe kisima (kizuri ni cha kuchimba na mashine sio na mikono)
2. Kisima chako itabidi kiwekwe casing (pvc[screen and plane])
3. Pia itatakiwa kiwekwe Graves
4. Kisha itawekwa pump iliyounganishwa na waya ulioyoka kwenye control box na pia pampu iliyoonganishwa na poly pipe kwa ajili ya kupitisha maji
5. Pia pump lazima ifungwe na kamba,mara nyingi tunapenda kutumia kamba za Manila kwa sababu ni imara na pia ni ngumu kuoza.
6. Baada ya hapo maji yatapandishwa kisha yatachukuliwa sample yake ili yakapimwe kama ni salama kwa matumizi ya binaadamu,mifugo au mimea

Nb. Kabla ya kufunga pampu kisima kina takiwa kiflashiwe ili kiachwe kikiwa kipo safi kabisa.

Hizo zote ni baadhi ya huduma ambazo pia tunazitowa,japokuwa kuna baadhi ya huduma kama kupima maji bado hatujaanza kutoa hiyo huduma, ila kama mteja atataka tumsaidiye kufanya hiyo huduma tutamsaidia kupitia kwa watu wengine.

Bei/gharama zetu za huduma:

Kuchimba kisima tunachimba kwa shillingi elfu sitini (60000) kwa mita moja hii ni bei kwa walioko Dar es salaam
Kwa walioko nje ya dar es salaam tutakubaliana kutokana na mkoa mteja alipo.
Na kwa bei hiyo tajwa hapo juu ni pamoja na usafili na ufungaji wa pampu unakuwa juu yetu.

Mfano: uchimbaji wa kisima cha mita 90 gharama yake ni...
Mita 1 = 60000 tsh
Mita 90 = y
Cross multiplication
Mita 90 × 60000 tsh/mita 1y
Cut Mita both side
90 × 60000tsh/1
5400000tsh
Kwa hiyo gharama za kuchimba kisima cha mita 90 ni shillingi millioni tano na laki nne...gharama hizo ni pamoja na pampu.
Hapo mteja atatakiwa kununuwa maji yatakoyohitajika katika uchimbaji wa kisima na maji hayo yana uzwa tanki moja la lita elfu moja ni shillingi elfu kumi na tano.

Gharama/bei za ground water survey...
Kwa suala la upimaji wa uwepo wa maji tunachaji shillingi 250000 kwa mkazi wa dar es salaam, kwa mteja aliyepo nje ya dar es salaam tunaaanziya kuchaji shillingi laki tano lakini itategemea na mteja alipo.

Njia ya malipo:
Malipo ya ufanyaji wetu wa kazi huwa tunafanya tunapokuwa tupo site, tukishafika site kwa mara ya kwanza pamoja na vifaa vyetu vyote kwa ajili ya kuanza kazi hapo itabidi mteja atowe asilimia 65 ya gharama nzima.Ambayo hela hizo ndizo itakazo tumika kununulia vifaa vya kisima.

Mahali tulipo:
Offisi zetu zipo morogoro wilaya ya kilosa lakini baadhi ya vifaa vyetu vipo Dar es salaam kwa hiyo mteja akituhitaji kama yupo dar es salaam tunaweza kumfanyia kazi kwa gharama zetu za usafili na malipo yatafanyika tutakapo fika site tukiwa na vifaa vya uchimbaji.

Mawasiliano:
Piga simu namba 0628080096
Karibuni nyoote tuwahudumie
Nachotaka kujua... ni kujua kama maji ni salama au sio salama ni baada ya kuchimba au kabla...?
na kama ni baada ya kuchimba je..?
ikatokea maji sio salama... hio hasara inakua kwangu au kwenu...!?
au mkigundua sio salama mnafanyeje..!?
 
tawa driller

JF-Expert Member
Dec 11, 2015
296
250
Nachotaka kujua... ni kujua kama maji ni salama au sio salama ni baada ya kuchimba au kabla...?
na kama ni baada ya kuchimba je..?
ikatokea maji sio salama... hio hasara inakua kwangu au kwenu...!?
au mkigundua sio salama mnafanyeje..!?
Kujuwa maji ni salama au sio salama hiyo inakuja baada ya kuchimba tayari na maji yakafanyiwa lanoratory test then ndio tutajua.kama ikitokea sio salama sisi hatutakuwa na tatizo maana utahitajika sisi utulipe kwa kazi tuliyotakiwa kuifanya ya kuchimba mkuu
 
Fikra Angavu

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
301
225
Kujuwa maji ni salama au sio salama hiyo inakuja baada ya kuchimba tayari na maji yakafanyiwa lanoratory test then ndio tutajua.kama ikitokea sio salama sisi hatutakuwa na tatizo maana utahitajika sisi utulipe kwa kazi tuliyotakiwa kuifanya ya kuchimba mkuu
Aaah basi... mkuu.. bado huduma yenu sio nzuri....
kama ni ivo haina maana ya kuchukua kwenda kupima... kama ikitokea hayafai iwe haiwahusu...

apo maana yake kama vile mnakisia mwamba mlio upasua

Kwa elimu ndogo ninayojua ni kwamba maji yapo kwenye miamba... kinachotakiwa ni mchimbaji kutoboa muamba sahihi wa kutoa maji safi.
maana yake lazima mchimbaji ajue aina ya miamba inayopatikana sehemu husika ili ampe huduma bora mteja wake.
kwaio apo tunazungumzia kujali mteja wenu kwa kutoa huduma bora mteja aliyotegemea.

Au nimekosea... sio kweli...!?
 
Unaruhusiwa kutafuta surveyor wako unayemuamini then sisi tukakuchimbia kupitia report yake
 
josam

JF-Expert Member
Nov 22, 2011
2,234
2,000
Ninahitaji kampuni inayo fanya shughuli ya utafiti na uchimbaji maji.
Kazi zinazo takiwa kufanyika:
1. Kufanya survey na kushauri,
2. Kuchimba Kisima.

Asante. Josam
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom