Bei mpya ya umeme na siasa yetu

The Planner

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
357
118
Siasa inapoingia katika masuala ya msingi, tunaelekea kuua taifa letu! leo tunaambiwa bei ya unit 1 ya umeme inapanda kwa asilimia 18, so kutoka ilipo karibu Shs. 129 tunaelekea Shs.160 kwa unit moja and then tuna matumaini ya kuvuka kutoka uchumi unaotegemea kilimo kuwa industrial led economy, Jamani acheni kuchakachua mambo ya msingi kama ikiwezaka EWURA si ife tu!
 
Tunabanana ilikuilipa dowans.Na hiyo nadhani ni mwanzo tu wa kazi za mafisadi.KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Tunaanza kulipia gharama za ufisadi sasa.Tulirukaruka na kufurahia kanga,kofia na tshirts za kijani na kuwapa kura,hii ndo ari zaidi,kasi zaidi na nguvu zaidi.
 
Mtalalamika mpaka lini! nashukuru hizi bei hazibagui CCM wala cuf or chadema> Sote tunapigwa nyundo?
 
Wakati wa kupiga kura nilikuwa nabeba mabox kwa @ $10.00 an hour
Wakati wa matokeo nilikuwa nabeba mabox
Sasa kibano cha CCM kimeanza kukolezwa mimi bado nabeba mabox tu kama laana vile.

Niko mbali siangukiwi na mti.
Nikitoa dola moja moja hapo kila saa nakumtumia Msua pale Madongo kuinama Chai na Mkate asubuhi haijambo.

Umeme? Nilisha Funga Sola siku nyingi nataraji kuipanua ili waweze hata kupampu maji na kuyachemsha.
Dowans nilisha wapa radhi siku nyingi.

Lakini Maajenti wa Hao dowans si walisha wafidia KangaTshirt za Green Vest ya kijani na kofia?
Ng'ombe akisha kula majani ya kijani maziwa ni halali ya mlishaji!
Mlikua hamjui hiyo kitu?
 
sasa wale wakina kaka na kinadada waliokuwa wanapewa tishirt ni wakati wakulipia vyote vya bure, kwa maisha ya namna hii, nashindwa kumuelewa mtu anayesema yaye ni kada wa chama, shime kinadada wenzangu, nyie ndio mlikuwa wapiga kura wengi, mlijaza mikutano ya kampeni ya ccm, na sasa mnaona mnakolipeleka taifa, haki ya mungu moto ndio unaanza tutegemee matatizo zaidi
 
Wakati wa kupiga kura nilikuwa nabeba mabox kwa @ $10.00 an hour
Wakati wa matokeo nilikuwa nabeba mabox
Sasa kibano cha CCM kimeanza kukolezwa mimi bado nabeba mabox tu kama laana vile.

Niko mbali siangukiwi na mti.
Nikitoa dola moja moja hapo kila saa nakumtumia Msua pale Madongo kuinama Chai na Mkate asubuhi haijambo.

Umeme? Nilisha Funga Sola siku nyingi nataraji kuipanua ili waweze hata kupampu maji na kuyachemsha.
Dowans nilisha wapa radhi siku nyingi.

Lakini Maajenti wa Hao dowans si walisha wafidia KangaTshirt za Green Vest ya kijani na kofia?
Ng'ombe akisha kula majani ya kijani maziwa ni halali ya mlishaji!
Mlikua hamjui hiyo kitu?

Mkuu kati ya wafuatiliaji wa post zako na mimi nimo, kwani, ukiacha fasihi unayotumia ambao huniacha sina mbavu pia kuna mafunzo makubwa sana. Nilikumiss kwa muda mkuu. Boksi zilizidi nini?
 
Hii ni habari njema sana,kwani uoga wetu ndio unafanya tuongozwe kama punda.Sasa maisha yanavyozidi kupanda siku itakapo fika tukashindwa gharama hizi, ndio tutakapochagua kama tukae ndani tufe njaa kwa kuogopa mabomu ya machozi au tuandamane kudai haki yetu.
 
Hiyo ndo CCM bana haina huruma wala kujali wananchi wake! kufa hatufi ila cha moto tunakiona
 
Ukisikia utamu hasa sasa ndio tunaanza kuonjeshwa huo utamu. Tulifurahia T-shirt, Kofia, Muziki toka TOT, mapipa ya komoni nakadhalika. Utamu wa kuongezeka kwa bei ya umeme kwa 18% kwa kila unit, haiishii tu pale unaponunua umeme.Sheshe lake linaingia katika nyanja kibao za uchumi na uzalishaji mali. Kila bidhaa yenye kutengenezwa kwa mashine inayotumia umeme wa Tanesco, basi nayo itapanda kwa karibu ya asilimia kama hiyo. Anzia ugali kwa mama Lishe, gharama ya kushona suruali/gauni, Bei ya ndoo moja ya maji pale kwenye bomba la mpemba mtaani kwetu, gharama ya kilo moja ya samaki toka mwanza nk. Gharama itapanda kwa kila kitu. Huundio mwanzo wa ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI na KASI ZAIDI. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sasa mnasemaje?
Maana naona ninachokisoma humu naona ni manung'uniko na kunyoosheana vidole ambavyo havitatusaidia kitu!!

Hivi mnajua wenzetu Zambia down the road wakiongezewa hata senti moja kwenye kilo ya unga huko mtaani hapatoshi na nchi huwa haikaliki?
Why not here?
Can't we do something? Anything???
Damn it wasomi, anything!!!
 
Jenerali Ulimwengu aliwahi kuandika wakati tunaelekea uchaguzi kuwa, tuna tabia ya kuchagua hovyo na baadaye tunalalamika nadhani uchaguzi wetu ndio umeleta matunda haya sasa hatuna budi kulalamika next time tuwe waangalifu kwenye uchaguzi ili kuepuka kulalamika.
 
Naomba nichangie kwa mara ya kwanza. Hili suala la bei kupanda za umeme halafu na mgao, ni tatizo litokanalo na mipango isiyokuwa endelevu katika suala la umeme. Unaweza ukatoza bei hiyo lakini huduma iwe ya uhakika. Tanzania inatakiwa kutumia vyanzo madhubuti katika kuzalisha umeme kama vile upepo kule Singida, Geothermal (Jotoardhi) hii ni rasilimali nzuri sana tuliyonayo lakini hatuitumii nenda kenya uone jinsi wanavyoitumia geothermal Mungu akupe nini! Vyanzo ni vingi sana ndugu zangu.
Tutabaki na mipango ya muda mfupi tu, mara bwawa limekauka,mara gesi sijui imefanyaje...
 
Siasa inapoingia katika masuala ya msingi, tunaelekea kuua taifa letu! leo tunaambiwa bei ya unit 1 ya umeme inapanda kwa asilimia 18, so kutoka ilipo karibu Shs. 129 tunaelekea Shs.160 kwa unit moja and then tuna matumaini ya kuvuka kutoka uchumi unaotegemea kilimo kuwa industrial led economy, Jamani acheni kuchakachua mambo ya msingi kama ikiwezaka EWURA si ife tu!

CCM,CCM,CCM MAISHA BoRA KWA KILA MTZ ,RAHA SANA KUWA MTANZANIA
 
Hii ndio hatari ya kufanya mambo ya maana kisiasa, asubuhi nimemsikia mkuu wa EWURA akisema Tanzania tunalipa bei ndogo ya umeme ukilionganisha na nchi za Kenya na uganda, sina uhakika na maelezo yake maana kila kukicha wafanya biashara na wenye viwanda (CTI) wanalalamika gharama za uzalishaji( Umeme ukiwepo) ziko juu kulinganisha na wenzetu. Tuna kila sababu ya kutenganisha siasa na mambo ya kimaendeleo
 
Back
Top Bottom