BEI MPYA YA UMEME: CHADEMA, wasomi, wanaharakati wapinga bei mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BEI MPYA YA UMEME: CHADEMA, wasomi, wanaharakati wapinga bei mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 14, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Umeme wazua balaa

  • CHADEMA, wasomi, wanaharakati wapinga bei mpya

  na Mwandishi wetu
  Tanzania Daima


  BEI mpya ya umeme iliyotangazwa juzi na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (Ewura), imezua balaa kubwa baada ya makundi ya kijamii na kisiasa kuipinga kwa madai kuwa itasababisha ugumu wa maisha kwa wananchi.

  Makundi hayo kwa nyakati tofauti jana, yalionyesha kukerwa kwao na jinsi serikali ilivyoamua kukosa na huruma kwa watu wake ambao wanakabiliwa na ugumu wa maisha.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, John Mnyika (CHADEMA), pamoja na kuahidi kutoa tamko rasmi wakati wowote, alisema ongezeko hilo ni matokeo ya serikali kudharau maoni ya kambi ya upinzani yaliyotolewa wakati wa kikao cha Bunge mwaka jana.

  Mnyika alisema Ewura haijaonyesha kwa ukamilifu iwapo njia zote zimetumika katika kupunguza gharama za uendeshaji za Tanesco mpaka kufikia hatua ya kupandisha gharama za huduma ya umeme kwa kiwango cha asilimia 40.29.

  Alisema akiwa waziri kivuli wa wizara hiyo, alitarajia kwamba serikali ingefunga mkanda na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima ikiwemo ya posho za vikao na kupanua wigo wa mapato ikiwemo katika sekta ya madini na kuingozea fedha Tanesco bila kubebesha mzigo mkubwa kwa wananchi wa kawaida kama CHADEMA ilivyopendekeza bungeni Julai 15 na Agosti 13, 2011.

  Pamoja na matatizo ya kifedha ya Tanesco ambayo serikali inapaswa kuyashughulikia kwa njia mbadala katika kipindi hiki cha mpito gharama kubwa za uzalishaji zinazolikabili shirika zinachangiwa na ufisadi wa muda mrefu katika mikataba ikiwemo ya uzalishaji wa gesi na ukodishaji wa mitambo ya kufua na pia maamuzi ya kukopa kibiashara katika kutekeleza mpango huo.

  "Wananchi wakumbuke kwamba hii ni mara ya pili katika kipindi cha takriban mwaka mmoja kwa Tanesco kupandisha bei ya umeme; mara ya kwanza ikiwa mwezi Januari 2011 ambapo umeme ulipanda kwa asilimia 18.5 na kuchangia katika kupanda kwa gharama za uzalishaji katika nchi na kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi," alisema Mnyika.

  Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo alisema serikali kabla ya kuongeza bei ya umeme kwa Watanzania wa kawaida, ingewaeleze wananchi imewapunguzia mzigo kiasi gani kwa kupitia upya mikataba ya kifisadi inayolinyonya Shirika la Umeme Tanzania kama ilivyopendekezwa kwenye ripoti mbalimbali ikiwemo maazimio ya Bunge ya mwaka 2008 juu ya mkataba wa ukodishaji wa mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Richmond Develepment Company LLC ambapo orodha ya mikataba na makampuni mengine ilitajwa ambayo mpaka sasa inaendelea kuipa mzigo Tanesco ikiwemo ya Songas na Pan African Energy Tanzania.

  Alikumbusha jinsi alivyoionya serikali kuepuka uamuzi wa kuchukua mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa ambayo imeongeza zaidi gharama za uzalishaji wa umeme na hivyo kuifanya Tanesco iongeze zaidi bei ya umeme kwa wateja.

  "Uamuzi huu wa kupandisha kwa kiwango kikubwa bei ya umeme utasababisha ongezeko la ziada la mfumko wa bei hali ambayo ni tishio kwa usalama na uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.

  "Serikali izingatie kwamba mfumko wa bei nchini umeongezeka na bidhaa zinazochangia mfumko huo kwa kiwango kikubwa ni vyakula, mafuta na umeme.
  Kupanda kwa bei kwenye sekta ya nishati pekee kumechangia kwa kiwango kikubwa kupanda kwa gharama za maisha, sasa viongozi wajiulize itakuwaje baada ya kupanda kwa umeme?"

  Profesa Baregu: Ni maumivu kwa mwananchi

  Mmoja wa wasomi na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SAUT, Profesa Mwesigwa Baregu, alisema ongezeko hilo la umeme licha ya kupingana na kampeni ya utunzaji wa mazingira, litachangia ongezeko la bei kwa mtumiaji wa kawaida ambaye ni mwananchi.

  Alisema kutokana na nishati hiyo ya umeme kuzidi kuwa aghali wananchi watarudi nyuma na kuanza kutumia kuni na hivyo kuharibu vyanzo vya maji na kusababisha kutopatikana kwa mvua kwa wakati.

  Baregu alisema serikali ingepaswa kueleza kwa ufasaha hasa ni sababu gani iliyosababisha kupandisha bei kwa nishati hiyo na itakuwa kwa muda gani kwa kuwa kwa sasa imekuja kama zima moto na kuongeza kwamba inahitajika mabadiliko ya sera katika suala zima la nishati ya umeme.

  Naye mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Uchumi na Takwimu, Profesa Morisi Mbago, alisema ongezeka la asilimia iliyotangazwa na Ewura limekuwa kubwa mno ukilinganisha na kipato halisi cha wananchi.

  Profesa Mbago alisema bei ya umeme ya sasa, wananchi hawaimudu na ongezeko hilo jipya litawaumiza zaidi na kufanya maisha yao kuwa magumu kwao.

  "Kwa sasa kila bidhaa sokoni iko juu sasa hiyo bei mpya ya umeme itakapoanza kutumika rasmi kesho ni wazi kwamba hali itazidi kuwa mbaya kwa wananchi ambao wengi wanaishi kwa mlo mmoja," alisema.

  Huko Dodoma, baadhi ya wananchi wamepinga vikali kupanda kwa gharama za umeme kwa madai kuwa kutasababisha gharama za maisha kuwa juu.

  Mmoja wa wafanyabiashara maarufu mjini hapa Peter Olomi alisema kuwa kwa sasa maisha bora kwa Mtanzania ni kitendawili na kwamba kitendo cha kupanda kwa gharama ya umeme kitayaathiri makundi yote ya kijamii.

  Olomi alidai Watanzania wategemee kuona mfumko wa bei, ukosefu wa ajira ikiwa ni pamoja na makampuni mengi kufilisika.

  "Fikiria kwa sasa maisha yako juu, mafuta yanauzwa kwa bei kubwa wakati shilingi yetu haina thamani na sasa angalia umeme umepanda bei unategemea wananchi kuishi maisha gani?

  "Kwa sasa kila kitu kitapanda bei na atakayeumia zaidi ni mlaji wa mwisho," alisema Olomi.
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kila kitu kitapanda bei tena haswa, BAK huku nilipo photocopy 1 karatasi ya A4 wanatoa sh 150-200. Wacha wapinge asee mie pia nawaunga mkono!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  itaishia kwenye MATAMKO TU,i hate this hakutakuwa na mabadiliko yeyote,jus wait
   
 4. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Lakini hoja yao ambayo kwa kweli ni ya kipuuzi ni kwamba - watakaoathirika ni wale wanaotumia umeme mkubwa, sio watumiaji wadogo wadogo. Na hili ni tambo la serikali la mwaka jana Bungeni (Ngeleja), na limerudiwa tena na Ewura. Lakini je, kama ni serikali hiyo hiyo ambayo inadai inakazana kupunguza umaskini - kumuongezea mzalishaji gharama ya umeme maana yake si ni kwamba atahamishia gharama hizo kwa mnunuzi? Serikali gani hii isiyokuwa makini na matamko yake? Hivi sasa gharama ya uendeshaji biashara kwa wastani ni kama asilimia 25 hadi 35 ya faida; ukichanganya na hii ya ongezeko la gharama ya umeme, gharama za mzalishaji kwa ujumla wake zitafikia wastani wa asilimia 50 hadi 60 ya faida. Sasa ongezeko hili linampunguzia vipi ugumu wa maisha mtumiaji mdogo wa umeme? Ni kama vile serikali inampa unafuu kwenye mkono wake wa kulia, na kumpora unafuu wake huo kwenye mkono wa kushoto. Na je, kwa mwendo huu, tutakuza ajira kweli kwa mtindo huu? au ndio kuua ajira?
   
 5. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  TUCTA watuanzishie kama Nigeria, au trade union za TZ ni bla bla tu? au hakuna sababu??? 40% ni kubwa sana.

  Vikianzisha vyama vya siasa na vyombo vya kupigania haki CCm watasema mbinu za CHADEMA.
   
 6. a

  agripinadaud Member

  #6
  Jan 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado! Ccm wanafanya mambo as if hii nchi ni "kiosk chao". Watz mkiona watu wa mataifa mengine wanaandamana na kupoteza uhai mjue wanakuwa wamefikia "the point of no return". So if one day that point reaches in our country automatically watz wataingia mitaani kudai kuondoka kwa hawa "black-colonialists (ccm)"!
   
 7. V

  Vitalino mlelwa Member

  #7
  Jan 14, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu tunusuru na hili janga tuondoshee wachumia tumbo na wenye mawazo mgando kwenye safu ya uongozi na watalamu.
  Hiv tunaosoma kwa kodi za wanainchi huwa tunajiuliza tunawarudishia fadhira gani walipa kodi?. Kwasababu kila kunapokuwa na shida kupanda kwa gharama ya vitu mbalimbali hata kwa kuvurunda kwa watumishi wa sehemu husika mzigo wote hutupiwa wanainchi wakawaida hv sisi ndo wenye unafuu sana wamaisha au? Sasa pandisheni na mishahara basi mlianza mafuta watu wamepaki magari na viwanda vimefungwa hamjarizika mmehamia kwenye umeme.
   
 8. Kipis

  Kipis JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 493
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umasikini wa mawazo unaowasumbuwa viongozi wa serikali hii dhalimu.
   
 9. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  maoni yangu kwa wanaccm wenzangu na serikali ni kuangalia upya uamuzi huu, na sababu za kupanda kwa bill hizo.
  1. kupitia upya taarifa ya ukusanyaji wa bill na ikiwezekana kuandaa utaratibu mbovu unaopelekea shirika kupoteza mafao
  2. kuziba mianya yote mfano uchakachuaji wa mita haza hizi za luku, mfano mbeya mjini luku nyingi zinaoneka ni mbovu na watumiaji hawalipi na luku haikati umeme.
  3. tulishauri shirika kuligawa mara tatu yaani ugavi/usambazaji, uzalishaji, kuuza umeme ili kupunguza kwa namna moja mludikano wa majukumu.
  4. kusambaza umeme kwa wahitaji wengi zaidi kwa kuzingatia ukubwa wa nchi na mtandao wake badala ya ilvyo sasa kuwa ni asilimia 16% ndiyo wenye umeme na ni hao tu wanaooneka ni wateja wa tanesco na hivyo kubebeshwa gharama zote.
  5. kushusha gharama za uendeshaji kwa serikali kutoa subsdy na kuondoa wafanyakazi ili kubaki na wale wa muhimu tu.
   
 10. M

  Makupa JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  tujiandae kwa mlipuko wa magonjwa hasa kipindupindu kwa maana sio siri familia nyingi sana hazitakuwa na uwezo wa kuchemsha maji ya kunywa
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160

  Dawa yao ni kuvua hilo gamba na kuvaa gwanda kaka/dada
   
 12. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #12
  Jan 14, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Uzuri wa bongo itaibuka mipasho ya muda kama wa wiki mbili then wanaibua kitu cha kipumbavu wote mnahamia huko,la kivukon lishapita,yaan kama vile mtu kashika remote ana forward movies ikisha-mboa kidogo,nyie subirin ****** akiwa bored ana forward tu au anapiga NEXT ije movie mpya staring Nape!!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Kupanda umeme: Vilio kila mahali
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 13 January 2012 19:37
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  [​IMG]Waandishi Wetu
  KUPANDA kwa bei ya umeme kumepokewa kwa mshtuko na wananchi wa kada mbalimbali wengi wao wakisema hicho ni kitanzi kingine kwao wakati huu ambao gharama za maisha zimepanda, thamani ya shilingi imeshuka huku mfumuko wa bei ukiongezeka.

  Wananchi wengi waliohojiwa na waandishi wa habari wa gazeti hili jana wameelezea kushangazwa kwao na kauli iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (Ewura) kwamba kupanda huko kwa bei ya umeme hakutawagusa watumiaji wadogo huku wakibainisha kwamba hawawezi kukwepa athari zitakazosababishwa na ongezeko hilo.

  Wakazi wa mikoa mbalimbali nchini wakiwamo wasomi, wafanyabiashara, wafanyakazi na watu wa kawaida, wamesema Serikali isingepandisha gharama hizo kwa wakati huu na badala yake ingewaonea huruma kwa kutafuta namna nyingine ya kutatua tatizo hilo.

  Juzi, Ewura iliidhinisha kupanda kwa bei ya umeme kwa asilimia 40.29 kuanzia keshokutwa, Januari 15 mwaka huu huku Mkurugenzi wake, Haruna Masebu akisema ongezeko hilo halitawahusu wateja wa hali ya chini, wanaotumia chini ya uniti 50 kwa mwezi pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco).

  Kauli yake imepingwa na wananchi wengi ambao walisema gharama kubwa za umeme zitakuwa na athari kubwa kila mwananchi kwani zitasabisha ongezeko la bei za bidhaa na huduma.

  Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Siena Italia, Emmanueli Maliti alisema: "Kila mwananchi atakutana na makali ya gharama hizi nje ya makazi yake, hakuna jinsi ya kukwepa. Kwanza hakuna utafiti wowote wa kitaalamu ambao umefanywa na kuthibitisha kwamba hata hao wanaoitwa walalahoi kama wanaweza kugharimia hiyo uniti moja ya umeme kwa Sh60, lakini pia hata kama wangewapa umeme bure, lazima wakutane na makali ya gharama hizo kwenye bidhaa na huduma."

  Alisema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa hata wasio walalahoi ni watumiaji wakubwa wa mkaa na kwamba kupanda kwa bei kutasababisha matumizi makubwa zaidi ya mkaa hivyo kuathiri mazingira.
  "Hapa ndipo unaona mgongano kati ya sera ya kuhifadhi mazingira na sera ya nishati. Kupandisha bei ya umeme siyo suluhisho la matatizo ya Tanesco. Hatujaambiwa Tanesco inashughulikia vipi gharama zake za uendeshaji kwa sababu unaweza ukashusha gharama na kubaki na mapato makubwa bila kuongeza bei," alisema.
  Mhadhidi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Bwete Gabriel alisema gharama za umeme zitamwelemea mwanchi wa kawaida na akisema matokeo yake ni kukua kwa umasikini.
  Dk Gabriel alisema kupandisha bei kwa watu wa juu na kusema suala hili halimgusi mlalahoi ni utapeli kwani vitu vyote kutoka katika gharama hizo vitamrudia huyohuyo mlalahoi kwa gharama kubwa zaidi.
  Umeme wapandisha bei ya maji Dar
  Makali ya kupanda kwa bei ya umeme yameanza baada Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), kueleza azma yake ya kupandisha bei ya maji kutokana ongezeko hilo la gharama za umeme.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasa, Jackson Midala alisema jana kuwa kutokana na bei mpya ya umeme, shirika lake litalazimika kulipa umeme Sh820 milioni kwa mwezi badala ya Sh580 za sasa.

  "Mitambo inahitaji umeme mwingi na siyo jenereta. Kutokana na kupanda kwa gharama za umeme tunalazimika kuongeza zaidi ya Sh240 milioni katika fedha hizo ili tuweze kuzalisha. Tupo kwenye mchakato wa kupandisha bili ya maji," alisema Midala.

  Alisema mpaka sasa lita 1,000 za maji zinauzwa kwa Sh850 na ndoo moja ni Sh17 na kwamba fedha hizo ni ndogo zisizoweza kukidhi mahitaji ya uendeshaji kutokana na ongezeko la gharama za umeme.

  Alisema tayari Dawasa wamewasilisha maombi Ewura kwa ajili ya kupandisha gharama hizo, lakini kwa sasa watalazimika kupitia upya mchanganuo wa gharama walizoainisha kwenye maombi hayo ili ziendane na gharama za sasa.

  Gharama za tiba juu
  Mkurugenzi wa Hospitali ya Shree Hindu Mandal, Kaushiki Ramaiya alisema hatua ya kuongeza bei ya umeme itaathiri gharama za uendeshaji katika sekta ya afya na kwamba wananchi wajiandae kukabiliana na ongezeko la gharama za dawa na baadhi ya huduma za hospitali.

  Alisema ongezeko hilo litaonekana zaidi kwenye hospitali binafsi hivyo akaonya: "Hawakuangalia anayeumia ni nani."

  Alisema atakayeubeba mzigo wote wa gharama ni mwananchi kwa sababu wamiliki wakati wote wanahakikisha gharama za uendeshaji hazizidi mapato katika kutengeneza faida.

  Kilio cha wakazi wa Dar
  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walisema kupandishwa kwa gharama hizo kunaashiria wazi kuwa hakuna mipango madhubuti ya kuwasaidia walalahoi.

  Mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Zainabu Ally alisema hivi sasa taifa linaelekea kubaya kwani imefikia mahali viongozi wanatoa uamuzi kwa manufaa binafsi… "Kama tusipokuwa makini na uamuzi wa mambo mbalimbali hasa yenye maslahi kwa taifa letu, tutafika mahali kila kitu kitatisha.

  Mkazi wa Buguruni, Jaremiah Agustino alisema wananchi wengi wanaishi chini ya kipato cha Sh1,600 (dola moja) kwa siku na kwamba bei mpya za umeme zitaendelea kuwadidimiza kiuchumi.

  Kwa upande wake, Fatuma Suleimani, mkazi wa Kinondoni anayejishughulisha na saluni alisema: "Kweli Serikali inaonyesha kila dalili za kutudidimiza badala ya kutuimarisha kiuchumi. Katika maisha ya mwanadamu kwa sasa umeme una asilimia 70 ya kipato chake, sasa kama ndiyo hivi gharama imeongezeka na mgawo usiokuwa na ratiba tunakokwenda ni wapi?"

  Arusha wapinga
  Baadhi ya wakazi wa Arusha wamepinga uamuzi huo kupandisha bei ya umeme wakisema utasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali na hivyo kuongeza gharama za maisha.

  Mmoja wa wakazi hao, Joram Manga alisema umefika wakati kwa Serikali kuisaidia Tanesco ili iweze kujiendesha kwa kulipa ruzuku na madeni mengine badala ya mzigo wote kuachiwa wananchi.

  Mkazi mwingine, Jenifer Minja aliwalaumu watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini akisema ndiyo tatizo kwani wamekosa ubunifu wa kupatikana umeme wa gharama nafuu badala yake wamejikita katika umeme wa mafuta wa kukodisha.

  Kwa upande wake, mkazi wa jiji hilo, Ismail Mohamed aliitaka Serikali kuwa makini akisema kuendelea kupitisha mipango inayoongeza ugumu wa maisha kwa wananchi kunaweza kusababisha machafuko.

  Mkazi wa Arusha, Yesaya Bayo alishauri wanaharakati na wabunge wazalendo kushirikiana kupinga ongezeko la gharama za umeme akisema ni hatari kwa usalama wa nchi kutokana na idadi kubwa ya watu kuendelea kuwa masikini.

  Morogoro wahofia maendeleo
  Mkoani Morogoro, baadhi ya wananchi wamesema kupanda kwa umeme kutarudisha nyuma maendeleo ya nchi na kuathiri uchumi wao na nchi kwa ujumla.

  Mmoja wa wakazi hao, Amani Kasanga alisema nishati ya umeme na mafuta ndiyo mihimili ya maendeleo ya mtu na taifa lolote lile duniani hivyo kutetereka kwa nishati hizo kutavuruga mikakati mingi ya kujiimarisha kiuchumi.

  "Hivi sasa umeme umepanda na mafuta yamekuwa yakipanda kila uchao, wananchi watarajia kupanda kwa gharama za maji, chakula na gharama za maisha kwa ujumla," alisema Kashanaga.

  Mkazi mwingine Amani Mwaipaja alisema: "Japokuwa tunaambiwa kuwa gharama hizi haziwahusu watumiaji wadogo lakini kimsingi watakaoathirika na ongezeko hilo ni watu wa kipato cha chini."

  Alisema Serikali inapaswa kutambua kuwa Tanesco, ni shirika la umma hivyo halipaswa kufanya biashara badala yake litoe huduma.

  Mratibu wa Mradi wa Umoja wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Morogoro (Ungo), Venance Mlali alisema madeni makubwa ambayo Tanesco inazidai taasisi za umma ndicho chanzo cha mzigo mzito wa gharama kubebeshwa wananchi wa kawaida.

  Mlally alisema Serikali ina uwezo wa kukabiliana na makali ya umeme kwa kusaka vyanzo vingine vya mapato ili kukidhi gharama za umeme zinazoongezeka kila kukicha

  Mwanza walia
  Huko Mwanza, baadhi ya wakazi wa jiji hilo na wanaharakati wamesema kupanda kwa bei ya umeme ni mwiba kwa wote kwa sababu wazalishaji wataongeza gharama za bidhaa zao sokoni ili kufidia gharama hizo.

  Meneja Utetezi wa Sera wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake Kivulini, Celestina Nyenga alisema kupanda kwa gharama hizo za umeme kutawaathiri zaidi wanawake kwa vile ndiyo wazalishaji wakubwa wa familia na ndiyo wanaobeba mzigo pindi gharama za maisha zinapopanda.

  Kwa upande wake, mmiliki wa karakana ya uchongaji wa vyuma vya mapambo ya nyumbani, Emmaunul Goodluck alisema Serikali imekuwa ikilazimisha mambo kwa mujibu wa matakwa yake na siyo kwa maslahi ya wananchi.

  "Najua kabisa utendaji wangu wa kazi ambao unategemea umeme utanilazimu kupandisha bei kufidia gharama za umeme. Nitaongeza bei kwa mteja na karakana yangu itaendelea na kazi," alisema Goodluck.

  Dodoma wapinga
  Baadhi ya wakazi wa mjini Dodoma wamesema hawakubaliani na sababu iliyotolewa na Tanesco ya kupandisha gharama za umeme.

  Mmoja wa wafanyabiashara wa mjini Dodoma, Josephat Kishobera alisema sababu zilizotolewa hazimwingii akilini akisema hivi sasa maji ni mengi… "Huu ni ujanja wa Serikali wa kutaka sisi watumiaji wa umeme tuilipie deni la Dowans. Sababu walizozitaja Tanesco hazina msingi wowote na sisi wafanyabiashara tutapandisha bei ya bidhaa zetu," alisema.

  Mwananchi mwingine, Josephat Nyaindi ambaye ni fundi wa kushona nguo alisema kupanda huko kwa bei, kutawagusa zaidi wananchi wa hali ya chini ambao ndiyo watumiaji wa mwisho wa bidhaa ambazo kwa kiasi kikubwa zinazalishwa kwa umeme.

  "Kupanda huko lazima kutamgusa mwananchi wa hali ya chini kutokana na wao kutumia bidhaa zinazotokana na umeme kwa mfano, mimi nashona suruali kwa Sh16,000 ni lazima nitapandisha mpaka Sh20,000 ili kulipia ongezeka hilo," alisema Nyaindi.

  Kwa upande wake, Naye Neema James ambaye ni mama wa nyumbani alisema imefika wakati sasa wa kutumia nishati mbadala wa umeme kwani kiasi kilichopanda ni kikubwa ikilinganishwa na kipato cha mwananchi wa kawaida.

  "Tunatumia umeme kwa shughuli nyingi, nadhani imefika wakati wa kutumia nishati mbadala wa umeme kama kuni na sola ambazo zina gharama nafuu kuliko huo umeme wa Tanesco" alisema.

  Songea waishangaa Tanesco
  Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Songea, Ruvuma wameshangazwa na kitendo cha kupandishewa kwa gharama za umeme wakati mgawo wa nishati hiyo ukiendelea.

  Mfanyabishara ya mashine ya kukoboa nafaka, Victor Ngongi alisema inashangaza Tanesco kupandisha bei ya umeme ilhali nishati hiyo haipatikani kutokana na mgawo.

  Alisema kupanda kwa bei ya umeme kutachangia kupanda kwa ongezeko la bei ya vyakula kwani nao watapandisha bei ya ukoboa kwa asilimia 50 ili kufidia ongezeko hilo na gharama nyingine.

  Mkazi wa Bombambili mjini Songea, Meriana Mapunda alisema hatua hiyo ina lengo la kumuumiza mlaji… "Kwa kweli hali ya umeme bado ni mbaya hasa hapa kwetu, umeme ni tatizo vitu vimepanda bei na tunawashangaa kwa kupandisha tena gharama za maisha wakati umeme wenyewe ni tatizo."

  Mbeya walia
  Huko Mbeya, baadhi ya wananchi wamesema kitendo cha Ewura kuidhinisha kupanda kwa bei ya umeme kwa asilimia 40.29 ni mbinu za Serikali kutaka kulipa deni la Dowans… "Wameamua kutangaza gharama kubwa ili kupata unafuu wa kulipa deni hilo," alisema mkazi wa Mwanjelwa, Ngussa Edward.

  Mwananchi mwingine, Isaac Samson alisema si kweli kwamba wananchi wanaotumia chini ya uniti 50 hawataguswa akisema maisha yataendelea kuwa magumu kutokana na bidhaa za viwandani kupanda na mtumiaji akiwa huyohuyo mwananchi wa chini.

  Mkazi wa Uwanja wa Ndege, Ulimboka Benjamin alisema kitendo hicho kitaendeleza umasikini kwa wananchi na kwamba ni ndoto kwa wasio na huduma hiyo kuipata sasa.

  "Je, kwa kuongeza gharama hizo tutaweza kuwafikia wananchi wote kupata huduma ya umeme? Huu ni unyonyaji kwa manufaa ya watu wachache na kutaka kulipa deni la Dowans," alisema Ulimboka.

  Habari hii imeandaliwa na Ellen Manyangu, Ibrahim Yamola, Fidelis Butahe na Shakila Nyerere - Dar, Patricia Kimelemeta -Ruvu, Joyce Joliga - Songea, Brandy Nelson - Mbeya, Venance George - Morogoro, Mussa Juma- Arusha, Frederick Katulanda - Mwanza, Masoud Masasi na Hamisi Mwesi - Dodoma.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kamati ya Bunge kuibana Ewura bei ya umeme [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 16 January 2012 20:56 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Patricia Kimelemeta na Hussein Issa
  Mwananchi

  KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini imesema itakutana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), kujadili kupanda kwa gharama za umeme huku ikisema itakata rufaa kwenye Baraza la Ushindani Kibiashara kupinga ongezeko hilo.

  Mwishoni mwa wiki, Ewura ilitangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 40.29, hatua ambayo imekuwa ikipingwa na wananchi wengi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, January Makamba alisema ongezeko hilo limewaumiza vichwa wabunge, jambo ambalo lilisababisha kamati kukaa na kuijadili.

  Makamba alisema katika mkutano wake huo na Ewura, kamati hiyo itayapatia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Tanesco pamoja na kukokotoa bei mpya na ile iliyopita ili waweze kujua uhalali wake. "Bei mpya ya umeme imetuchanganya sana, hii inatokana na kuongeza kwa kiasi kikubwa jambo ambalo wananchi wa kawaida watashindwa kuimudu.
  Kutokana na hali hiyo, tutakutana na mamlaka husika ili tuweze kujadili na kuangalia hatua zitakazofuata," alisema Makamba. Kikao hicho ambacho kimepangwa kufanyika juma lijalo, kitajadili bei hiyo na endapo itaonekana haikustahili watakata rufaa.

  Alisema Serikali ilitoa Sh200 bilioni kwa ajili ya kununua umeme, ambazo ni sawa na asilimia 60 ya umeme, huku Tanesco ikichangia asilimia 40 akisema kama ingeshindwa kutoa kiasi hicho, gharama za umeme zingekuwa kubwa kuliko zilizotangazwa hivi karibuni.

  Viwango vipya Katika ongezeko hilo la bei ya umeme ambalo limeanza kutumika Januari 15 mwaka huu, wateja wa hali ya chini wanaotumia chini ya uniti 50 kwa mwezi, wataendelea kulipa Sh60 kwa uniti wakati watumiaji wa majumbani wanaotumia zaidi ya uniti 50, bei hiyo imepanda kutoka Sh195 hadi Sh273 kwa uniti.

  Watumiaji wa kawaida wakiwemo wenye biashara ndogondogo, bei imepanda kutoka Sh157 hadi Sh221 kwa uniti wakati watumiaji umeme mkubwa wa kati, bei imepanda kutoka Sh94 hadi Sh132 kwa uniti, wakati watumiaji umeme mkubwa hasa wenye viwanda na migodi, bei imepanda kutoka Sh84 hadi Sh118 kwa uniti.

  Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), litauziwa umeme kwa Sh106 kwa uniti kutoka Sh83 ikiwa ni ongezeko la asilimia 28.21.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. l

  lausere New Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ninachoona mm ni kwamba serikali imekuwa ya "SPENDERS" and not "ENTREPRENEURS" haiwezekani umeme uzalishwe kwa hasara kubwa na bado waTZ Tutegemee kutakuwa na punguzo la bei, the problem Supply ya umeme ni ndogo na endapo serikali haitafanya mchakato wa kuinvest kwenye uzaalishaji umeme wa kutumia maji na upepo kwa sana. HAIWEZEKANI watanzania 2tegemee punguzo lolote la bei za umeme bali ongezeko... TZ ilipaswa izalishe umeme mwing tuuzie majirani but miaka inavyoenda sisi ndo 2takuwa 2unanunua kwa majirani. ningependa Tungeiga mfano wa Mississipi marekani miaka ya the great economic depression 2ukifanya hivyo tZ tutapata umeme wa kutosha ajira za kutosha na makazi mapya yatajengwa.. shida ni NANI ATAYATENDEA KAZI MAWAZO HAYA?????????????????:shock::shock:
   
 16. A

  August JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kupanda kwa umeme kuna sababishwa na ujeuri na ufisadi wa baadhi ya viongozi wa serikali inayoongozwa na chichiemu, hivyo mabadiliko hato yasikubalike walio tutia hasara hii ndio wafidie au warudishe chenji yetu?
   
 17. M

  MtuKwao Senior Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 7, 2006
  Messages: 190
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa, hakuna mtu anayetaka kufikiri.
  Bei ya umeme ni lazima iangaliwe kwa kulinganisha na mataifa mengine tunayofanya nayo biashara kwa karibu, hususan EAC na SADC. Kama bei zao za umeme ni ndogo kuliko zetu, basi uchumi wetu tunauchimbia kaburi kwa vile uzalishaji wetu utakuwa wa gharama kubwa zaidi kuliko wenzetu na hivyo gharama za bidhaa zetu hazitauzika kwenye soko ambalo tumeamua liwe huru! Wawekezaji nao hawatawekeza TZ kwa sababu hiyo. Kwa sababu hii KUU, bei ya umeme hasa kwa TZ, inatakiwa KUSHUKA, siyo kupanda kwa sababu tunazo rasilimali zinazotuwezesha kufanya hivyo. Ili kuweza kufanya hivyo (Kushusha bei ya sasa), natoa mapendekezo yafuatayo kwa Kamati ya Nishati na Serikali kwa ujumla:

  • Serikali ishiriki (siyo kifisadi, siyo kuziachia kampuni binafsi) kuweka miundombinu ya kuzalisha na kusambaza Gesi yetu ya Asili (kwa gharama nafuu) kwa wanaohitaji kuzalisha umeme! Hii ni rasilimali ambayo tunahitaji kuitumia kwa nguvu zote na binafsi sielewi ni kwa nini Serikali inaiachia kampuni moja ya SONGAS inatuuzia gesi YETU kwa bei mbaya!!
  • Shirika la Umeme la TANESCO liko ICU, halilipi kodi, linaendeshwa kwa gharama kubwa mno na utendaji wao siyo mzuri na umeme mwingi sana unapotea! Shirika hili linahitaji kuvunjwa na majukumu iliyo nayo sasa yawe huru kwa mtu au kampuni yoyote kufanya, kwa mfano kampuni yeyote itakayokidhi vigezo iweze kuzalisha umeme. Vivyo hivyo usambazaji na uuzaji. Kwa kufanya hivyo tutaongeza ushindani, bei itashuka, na KODI ITALIPWA.
  • Lazima Serikali izuie umeme kupanda bila kuzingatia vigezo muhimu vya kulinda uchumi wetu. Vigezo hivyo vizingatie ushindani wa bidhaa zetu kwenye soko.
  • Serikali iweke mkakati wa kupanua matumizi ya gesi asilia majumbani sehemu za mijini ili kulinda misitu/uoto na kuzuia nchi kuelekea kuwa jangwa kunakosababishwa na matumizi ya mkaa. Hii nayo inahitaji miji iliyopangika vizuri kuwezesha kuweka miundombinu hiyo. Viwanda navyo vihimizwe kutumia gesi, pia vyombo vya usafiri.

  n.k.
   
 18. M

  MtuKwao Senior Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 7, 2006
  Messages: 190
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa, hakuna mtu anayetaka kufikiri.
  Bei ya umeme ni lazima iangaliwe kwa kulinganisha na mataifa mengine tunayofanya nayo biashara kwa karibu, hususan EAC na SADC. Kama bei zao za umeme ni ndogo kuliko zetu, basi uchumi wetu tunauchimbia kaburi kwa vile uzalishaji wetu utakuwa wa gharama kubwa zaidi kuliko wenzetu na hivyo gharama za bidhaa zetu hazitauzika kwenye soko ambalo tumeamua liwe huru! Wawekezaji nao hawatawekeza TZ kwa sababu hiyo. Kwa sababu hii KUU, bei ya umeme hasa kwa TZ, inatakiwa KUSHUKA, siyo kupanda kwa sababu tunazo rasilimali zinazotuwezesha kufanya hivyo. Ili kuweza kufanya hivyo (Kushusha bei ya sasa), natoa mapendekezo yafuatayo kwa Kamati ya Nishati na Serikali kwa ujumla:

  • Serikali ishiriki (siyo kifisadi, siyo kuziachia kampuni binafsi) kuweka miundombinu ya kuzalisha na kusambaza Gesi yetu ya Asili (kwa gharama nafuu) kwa wanaohitaji kuzalisha umeme! Hii ni rasilimali ambayo tunahitaji kuitumia kwa nguvu zote na binafsi sielewi ni kwa nini Serikali inaiachia kampuni moja ya SONGAS inatuuzia gesi YETU kwa bei mbaya!!
  • Shirika la Umeme la TANESCO liko ICU, halilipi kodi, linaendeshwa kwa gharama kubwa mno na utendaji wao siyo mzuri na umeme mwingi sana unapotea! Shirika hili linahitaji kuvunjwa na majukumu iliyo nayo sasa yawe huru kwa mtu au kampuni yoyote kufanya, kwa mfano kampuni yeyote itakayokidhi vigezo iweze kuzalisha umeme. Vivyo hivyo usambazaji na uuzaji. Kwa kufanya hivyo tutaongeza ushindani, bei itashuka, na KODI ITALIPWA.
  • Lazima Serikali izuie umeme kupanda bila kuzingatia vigezo muhimu vya kulinda uchumi wetu. Vigezo hivyo vizingatie ushindani wa bidhaa zetu kwenye soko.
  • Serikali iweke mkakati wa kupanua matumizi ya gesi asilia majumbani sehemu za mijini ili kulinda misitu/uoto na kuzuia nchi kuelekea kuwa jangwa kunakosababishwa na matumizi ya mkaa. Hii nayo inahitaji miji iliyopangika vizuri kuwezesha kuweka miundombinu hiyo. Viwanda navyo vihimizwe kutumia gesi, pia vyombo vya usafiri.

  n.k.
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Maandamano jamani Maandamanooooo!!!!!!
   
 20. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Serikali haina huruma na wananchi wake.
   
Loading...