Bei mpya ya mafuta: Ewura chonde chonde ipitieni upya

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,661
18,035
Imekuwa ni desturi kwa Ewura kuwa inatangaza bei ya mafuta bila uwazi kwa namna ilivyokokotoa bei mpya.

Hii inasababisha kukoss uhalisia wa bei hiyo ukilinganisha na bei ya dunia.

Bei mpya iliyotangazwa ya petrol ni imepungua kwa sh 166/= tu likiwa ni punguzo la asilimia 7.5%. Lakini kwenye soko la dunia mafuta yamepungua kwa asilimia 51%.

Tulitegemea bei pia ingepungua kwa asilimia takriban hiyo hiyo 51% au karibu na hiyo na hivyo bei ya lita moja ya petroli ingeuzwa kwa takriban sh 1100/= tu.

Ninawapa changa moto Ewura wajitokeze hadharani na kutoa maelezo ya kina kwa nini bei pia isishuke kwa kuakisi ilivyoshuka kwenye soko la dunia na waweke wazi mahesabu yao yaliyopelekea bei hiyo ya juu sana ukilinganisha na bei ya soko duniani.

Nazialika taasisi nyingine za kiuchunguzi nazialika pia zichunguze jambo hili ambalo naona kama vile lina harufu ya sintofahamu! Lakini pia walaji/wanunuzi/watumiaji waa mafuta tuwe macho hapa kunafuka moshi. Ushahidi wa bei ya mafuta duniani kushuka kwa asilimia 51% huu hapa:

Crude Brent prices fell in March
In March of 2020, price of Brent crude was 32.15$ per barrel, while the price was 56.21$ dollars per barrel in February of 2020. Over last twelve months the price has fallen 51.39%.
 
Mfumo wa upangaji bei wa nchi yetu katika sekta ya mafuta ukiujua hautakusumbua sababu bei iliyopangwa sasa mwezi wa April hayo mafuta yalinunuliwa katika soko la dunia mwezi wa February na yaliingizwa nchini mwezi March.
 
Wakati huu ulikuwa wa kuwapa wananchi natumaini na ahueni, si kuwakamua kwa tozo mbalimbali zisizokuwa wala realistic. Hali za watu katika taharuki ya ugonjwa huu ni nani asiyezijua?

Kuwa kwa taarifa zilizopo serikali imepandisha mno hata kodi tu za mapato kwa wafanya biashara kwa mwaka huu.

Kuwa ni Makonda tu ndiye ambaye hadi sasa aliyejitokeza labda jwa kujibalaguza, kuwataka watoza kodi za mapango wawafikirie wateja wao kwa mapunguzo ya kodi kufikia angalau 50% kwa miezi 3 ijayo.

Kwa hakika iaijulikani Makonda huyu anaiwakilisha serikali ipi? Kweli ni serikali hihi ya awamu ya tano?

Je, Makonda anajua kuwa serikali, si tu kuwa haijakuwa na chembe ya kutambua magumu yoyote yanayo wakabili watu kufuatia hali ya ugonjwa huu, bali pia ime viongeza mno viwang vya kodi hata kwa hao wenye nyumba za kupangisha ambao yeye sasa anawataka wawe na utu kupunguza kodi wateja wao?

Je, Makonda anafahamu kuwa serikali imetumia kipindi hiki hiki cha hali duni ya uzalishaji kujineemesha yenyewe mno pasipo na kuwajali walipa kodi wowote kwa lolote?

Mwenye dala dala linalolazimika kwenda na abiria wachache zaidi (level seat) kwa sasa, kodi yake imepandishwa mno wakati mapato yake yameshuka hali serikali ya kina Makonda inamtaka yeye awe na utu ilaa wao aah aaah!.

Sijui hesabu za serikali hii kama ni hizi hizi ambazo wa mataifa mengine wanazitumia.

Labda zao ni za kiajemi au kiyahudi.
 
Mfumo wa upangaji bei wa nchi yetu katika sekta ya mafuta ukiujua hautakusumbua sababu bei iliyopangwa sasa mwezi wa April hayo mafuta yalinunuliwa katika soko la dunia mwezi wa February na yaliingizwa nchini mwezi March.

Mkuu ukweli mchungu. Usanii kwenye zetu ni mwingi mno.

Subiri za mwezi wowote kama zitakuja reflect hiyo 51% reduction at any time.
 
Ngoja tusubiri majibu yao,tofauti na hapo huu nao ni wizi tu

Sent from my TECNO K8 using Tapatalk
 
Mkuu ukweli mchungu. Usanii kwenye zetu ni mwingi mno.

Subiri za mwezi wowote kama zitakuja reflect hiyo 51% reduction at any time.

Unajua mkuu katika lita moja ya mafuta nchini karibu sh 700 ni kodi ya serikali pekee na hapo ujaongeza other statutory charges sijui TBS, EWURA, WMA, Railway Levy, Marking charges na Wharfage charges
 
Unajua mkuu katika lita moja ya mafuta nchini karibu sh 700 ni kodi ya serikali pekee na hapo ujaongeza other statutory charges sijui TBS, EWURA, WMA, Railway Levy, Marking charges na Wharfage charges

Hizi serikali zetu kwa hakika ni shida kweli kweli. Wao ni kujineemesha kama wao tu.

Imagine hata kwa nini katika hali ya sasa bunge linaendelea? Kama ilivyo kawaida upinzani na wa chama tawala ikija kwenye posho lao moja.
 
Kuna sababu mbili za kushuka kwa bei ya mafuta kwanza ni mgogoro wa wazalishaji kwenye ku control output; uliopelekea Russia na Saudi Arabia kuzalisha kupitiliza. Matokeo yake supply has outstripped demand na kufanya bei kushuka.

Pili Corona kasababisha uzalishaji wa uchumi wa dunia kupungua na mahitaji ya mafuta pia.

Wapangaji bei makini kwa walaji wa mwisho awawezi shusha bei iwapo sababu ya kushuka crude kwenye interenational market ni migogoro ya opec ya ndani au na mzalishaji wa nje kama ilivyo sasa kati ya Russia na Saudi Arabia; kwa sababu siku yoyote wanaweza kaa chini wakamaliza tofauti zao ni kupunguza oil glut wao wenyewe na bei zikapanda the next day.

Sababu ya pili (Corona) inaweza sababisha bei za ndani kupunguzwa kwa sababu ni actual economic factor inayosababisha oil glut kutokana na kushuka kwa uzalishaji and it takes time for economies to recover kwa ivyo it is justified (in a simpler explanation).

Ndio maana kwa sasa inakuwa ngumu kushusha bei kiasi kikubwa kwa sababu watu awajui ni kwa kiasi gani uchumi wa dunia umechangia kwenye percentage na kiasi gani mgogoro unachangia; Saudi Arabia na Russia wakiyamaliza ni rahisi kujua bei halisi ya mafuta kwa sasa sokoni kutokana na supply and demand na kupelekea kupanga bei halisia.
 
Back
Top Bottom