Bei mbovu kuwahi kutokea ya zao la mpunga yadumu misimu miwili Tanzania

MPUNGA MMOJA

JF-Expert Member
May 30, 2015
304
401
Kwa miaka takribani 15 sasa hakujawahi kutokea kuanguka kwa bei ya Mpunga.

Kilimo cha zao la Mpunga kwa msimu wa mwaka 2020/ 2021 kinaleta mashaka makubwa.

Bei ya wakati wa mavuno kwa gunia la serikali la debe 6 kwa msimu 2020 kipindi cha mavuno Tsh 50,000 hii ni bei ya mwezi wa sita wakati wa mavuno, bei hii imedumu mpaka mwezi wa 4/2021 na hakuna dalili za kupanda, miaka ingine mwezi kama huu wa 4 kurudi nyuma wa 3 mpka wa 12 bei hua 90,000 mpaka 110,000.

Wafanyabiashara wa kununua mpunga kwa Mbarali Mkoa wa Mbeya wengi hawajilima msimu huu kwa sababu walinunua mpunga kwa bei ya sh 50,000 wakiamini bei itapanda watauza kwa faida hali imekua siyo imesimama sh 50,000 kwa miezi 10 mfululizo.

Serikali haioneshi kuchukua hatua yoyote ktk kuhangaika kusaka masoko.

Mbeya pekee inazalisha Mpunga asilimia 32 kwa nchi nzima.

Tayari mavuno yanaanza ya msimu mpya wa mwaka 2021 bei ikiwa imesima ileile ya mavuno ya mwaka 2020.
 
Je hio bei inarudisha gharama za uzalishaji pamoja na modest profit?
 
Taarifa nyong'onyezi kw wanaohusle af unaambiwa mali utazipat kw Shamba like seriously?! Hya wabunge kama wasemaji saiv wanalip?!
 
Huko katavi huwa msimu wa mavuno, ni 30, 000 kwa gunia!!mvua zinaponyesha sehemu nyingi , lazima mavuno yawe mengi, kwani kila sehemu wanavuna!!na hata mwaka huu mavuno yatakuwepo!!mimi nashangaa sana, miaka hii kutunza mazao gharani ni sawa na kucheza kamali , bora upate hiyo 100, na kuizungusha, kuliko, kuitafuta 200, ya kubahatisha.

Serikali unadhani itafanya kitu gani kuweza kusaidia, kwani kama ni mipaka iko wazi, soko la ndani ndio hilo tena!!linapumulia mashine kutokana na mzunguko kuwa mdogo
 
Aisee nilijaribu kuingia kwenye hii business japo kidogo ila kilichotokea ni majanga bei haijapanda hata kidogo tangu msimu wa mavuno mwezi June 2020 hadi leo hii🙌
Wakati mwingine uwe unaomba ushauri kwa my hubby wako!! Ona sasa hela imekaa tu ghalani!

Ile mwaka jana (2020) tungeiweka hiyo hela yote kwenye siasa, muda huu tungekuwa tunatafuna tu hela za ubunge!! Yaani ningeshinda saa mbili tu asubuhi!!

Dah!! sasa hivi ungekuwa unatembelea li Vii Eiti!! Halafu unatambulika kama Mke wa Mheshimiwa Dr. Tate Mkuu , Mbunge wa Ushoto!! 😇

All in all, never give up Mummy!! Next time bei itapanda. Si umeona walio weka shehena ya alizeti mwaka huu!! Wanaoga tu mifwedha!! Lita ya hayo mafuta kwa mashineni, yanaanzia tsh. 5000! Mtaani ni kuanzia 6000 na kuendelea!!
 
Serikali ya kisomi ya Magufuli ilishawaambia wakulima kuwa wajipangie kuuza mazao yao bei ya juu.Uzeni bei ya juu sasa,si Rais alishasema muuze bei ya juu?Au hamkumsikia?Ninyi ni viziwi?Tunaposema kuwa Tanzania haina Rais huwa hatutanii hata kidogo na muwe mnatuelewa.Uchumi huwa hauendeshwi hivyo!

131547.jpg


Source:https://dar24.com/magufuli-wakulima-uzeni-mazao-kwa-bei-ya-juu-sana-watwangeni-kwelikweli/
 
Back
Top Bottom