Bei hii pale muhimbili ( moi )yamkatisha tamaa mgonjwa

I Have long givenup on my Serikali ya CCM.siku hizi i take matters into my Hands.nawashauri msitegemee serikali kwa lolote zaidi ya kuwakata Kodi.hapo kitambo nilikuwa nacomplain mpaka siku mzazi wangu akaniambia kuwa hii serikali ilishapoteza Dira na Ramani muda mrefu sana,toka enzi za Mwinyi.
kilichotakiwa Viongozi wake chini na kuchora upya Road Map on how to govern and manage our resources.

Muhimbili ni Taasisi inayoendeshwa kwa kujaza viraka,hawana vision or kama wanayo its a lip service only.
Kumejaa Mbuu wodini.tena hizi ni wodi za private. wodi ya wazazi private hamna pamba wala nini,wafanyakazi(only manesi)wana moyo wa ukweli na kujitolea lakini hospital management ndiyo iko vibaya na hovyo kabisa.

pole sana,mshauri aende Kibaha kuna hospitali nzuri kuzidi Moyo
 
Mkuu uliingia siko, MOI kuna upande wa private na upande wa general.... Kaulizie general then upate bei zake na ina chukua muda sana kuhudumiwa general sababu wagonjwa ni wengi sana sana na almost kila siku kuna emergency.....
 
Bora MOI kuliko bei ya Dr.Ndodi gharama za matibabu yake ni kuanzia mamilioni.

Mbona kuna huduma ya bure jamani, amwone mchungaji Kakobe, Mchungaji mama Lwakatare, prophet Maboya au hata mimi hapa japokuwa sivumi lakini nguvu ile iliyopo kwa hao niliowataja ipo pia ndani yangu. Serious, acha nimjengee imani kwanza labda atanitafuta...Mwezi uliopita nilifika hospital moja ya private si kwa matibabu lakini check up kwaajili ya viza maana hiyo tu ndo inaaminiwa na hiyo nchi niliyotembelea; nika mkuta mtoto mmoja wa dada wa kihindi akiwa katika hatua ya hatari na madaktari hawana jibu dada analia mtoto hataki kula chochote na amedhoofika so wanamlisha kwa drip nika guswa na hilo jambo pamoja na kuwa huyo dada si mkristu lakini imani yake ilinitia nguvu, nikamweleza kama atapenda nimsaidie akakubali nikageuza profession hapo nakuanza kumtibu mtoto kwa utaalamu wa jina la Yesu for about five minutes....Jioni nilimfuatilia kwa simu akasema mtoto ameanza kunyonya baada ya siku mbili akaanza kula and now he is back to normal...

So kama atakuwa kama huyu dada asijali kuhusu yeye ni nani na mimi ni nani its an easy case just for a twinkling of an eye the problem is gone....bila hata kulipa senti moja na kubwa zaidi hata kwa mawasiliano ya pm hapa JF basi inatosha sihitaji kumjua au yeye kunijua....Condition aje atoe ushuhuda hapa hapa kumpa sifa na utukufu Yesu ili wale wasioamini wapate imani!
 
Lakini huo mchanganuo unaonyesha gharama za 'fast track' au IPPM...zinakuwa hazina tofauti kubwa sana na private. Normal track 'daraja la kawaida' kwa hiyo operation unayosema haitazidi laki 2, ila sasa utakuta list ya wanaosubiri operation mpaka mwezi june au july...ndio maana watu huwa wanakimbilia fast track kulipa hizo gharama ulizonyumbulisha. Alternatively, kuna madaktari wapasuaji wengi tu wanaofanya kazi hapo MOI huwa wanakuwa na wagonjwa private na kuwafanyia upasuaji kwenye hospitali/theatre private kwa makubaliano ya gharama kati yako na daktari wako lakini pia itajumuisha theatre charges kwa huko atakapoenda kufanyia! Au nenda Kibaha kwa Dr Bakke..nasikia anafanya cheaper zaidi.
 
Asanteni kwa maoni wana JF. Hiyo ya Kibaha pia nilikuwa siijui. Sasa labda hiyo kesho atachagua kati ya Kibaha na CCBRT. Ushauri nimeshamfikishia. Asanteni mpaka sasa. Sijafunga kupokea ushauri so endeleeni. Many thanks wakuu
 
sisi ndo inatupasa tuandamane wali si wale jamaa wa libya. Kwao elimu ni bure from shule ya msingi hadi chuo kikuu, matibabu ni bure, kuna matabaka mawili la juu na kati chini no. Maji (yasiyo na chunvi kwa wananchi), serikali inawajengea wananchi wake nyumba ya vyumba vitatu. Na bongo vipi pamoja na raslimali mnazokuwa nazo? Tuvumilie tu!

nimeipenda post yako kaka, kweli kabisa,,,,, ,,naona wengi wanaochangia wanaishambulia moi bila kujua chanzo cha haya yote ni hawa watu wanaoitwa viongozi wa serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania. Sisi maskini wengi tengeweza hata kutibiwa bure kwa magonjwa makubwa kama haya ya ndugu yetu lakini tanzania yetu haijawahi kupata viongozi wa kweli wenye uchungu na shida zetu. Na kiukweli hakuna hata kiongozi mmoja anayesukumwa kwenye siasa kwa wito bali ni kimbilio la wale walioshindwa kutajirika sehemu zingine ndo wanakimbilia huko na wanabaki kuhadaa watu watu eti udaktari na unesi ndo kazi za wito pekee.....

LEO HII FEDHA NYINGI INAISHIA MIFUKONI MWA WACHACHE AMBAPO KUNGEKUWA NA UTENDAJI MZURI WA SERIKALI NA UBUNIFU WA VYANZO VINGI VYA MAPATO AMBAVYO TANZANIA IMEBARIKIWA KILIO KAMA HICHI KISINGESIKIKIKA.
 
Mh! Sasa naanza kufahamu sababu kwa nini watu wengi ninaowajua hawataki kurudi nyumbani...
 
Bora MOI kuliko bei ya Dr.Ndodi gharama za matibabu yake ni kuanzia mamilioni.

Ndibalema umelonga.

Kama wiki mbili zilizopita nilimsindikiza jamaa yangu anayesumbuliwa na kisukari kwa muda mrefu. Dr. Ndodi amekuwa akijinadi katika vipindi vyake vinavyorushwa na Star TV kuwa anatibu kisukari; wiki kumi na tano kwa wagonjwa ambao hawajaanza kutumia Insulin. Kwa wale ambao wameshaanza kutumia Insulin, anadai anawatibu kwa wiki 30.

Dr. Ndodi ni mcheshi na mkarimu, aliposikiliza tatizo letu alimwambia jamaa yangu kuwa GHARAMA ZA KUTIBU KISUKARI NI MILLIONI 4......... Na akalalama kuwa vipindi vya Star TV vinamgharimu sana; 26m kwa kipindi kimoja (mnaojua gharama za kurusha kipindi live kwenye TV mtuhabarishe kama hii gharama ni ya ukweli). Baada ya kusikia "stori" hiyo, jamaa yangu aliyekwenda pale akiwa dhaifu, ghafla alipata nguvu na kusema tuishie.
 
Nina rafiki yangu ambae ndugu yake alivamiwa na majambazi na kujeruhiwa mkono. Bei ya out patient pale MOI imemkatisha tamaa kiasi kwamba inabidi akatafute huduma pengine. Bei aliyopewa MOI ni hii:

Operation fee 200,000
Accomodation kwa siku tatu 120,000
Consultation fee 20,000
Theater charges 90,000
theater drugs 15,000
Anaesthesis charges 90,000
Anaesthesian consultation fee 5,000
Lab investigation 20,000
Medication 20,000
Dressing mara mbili 10,000
Jumla kuu 590,000


Mgonjwa alishalipa 50,000 kumuona daktari. Baada ya kupewa hizi bei yamemshinda. Vidole vyake vinajiunga vibaya. Jamani wana JF naomba ushauri kwa hili. Wapi angalao aende penye unafuu maana tena watu wa chini kumudu hizo gharama si unajua tena. Tatizo liko kwenye vidole viwili tu

Mrejesho huu hapa:
Yule ndugu kafuata ushauri wa kwenda CCBRT na kule wamemwambia operation ingeweza kugharimu 300,000 ila hawawezi kumfanyia kwasababu kashachelewa vidole vimeshaunga vibaya. Awali aliwekwa POP kakaa nalo wiki 4 but kuona bado maumivu ni makali ndio akaja Dar kusaka matibabu zaidi. MOI kukamshinda. CCBRT wamesema operation haiwekaniki tena maana itakuwa ni kutafuta tatizo lingine since vidole vimeshaunga vibaya operation ni ngumu maana sijui kuna mishipa gani ........kwahiyo wakamwambia hawawezi kumchukulia hela zake kwa kitu ambacho wanaona haiwezekani. Wakamshauri akae hivyo hivyo bali afanyiwe mazoezi. Jamaa kasema kujiridhisha nafsi ataenda tena na Kibaha akasikie kule watamwambia nini. Ni hayo tu kwa leo. Asanteni kwa ushauri wenu so far.
 
nina rafiki yangu ambae ndugu yake alivamiwa na majambazi na kujeruhiwa mkono. Bei ya out patient pale moi imemkatisha tamaa kiasi kwamba inabidi akatafute huduma pengine. Bei aliyopewa moi ni hii:

Operation fee 200,000
accomodation kwa siku tatu 120,000
consultation fee 20,000
theater charges 90,000
theater drugs 15,000
anaesthesis charges 90,000
anaesthesian consultation fee 5,000
lab investigation 20,000
medication 20,000
dressing mara mbili 10,000
jumla kuu 590,000


mgonjwa alishalipa 50,000 kumuona daktari. Baada ya kupewa hizi bei yamemshinda. Vidole vyake vinajiunga vibaya. Jamani wana jf naomba ushauri kwa hili. Wapi angalao aende penye unafuu maana tena watu wa chini kumudu hizo gharama si unajua tena. Tatizo liko kwenye vidole viwili tu


mpeleke aghakan hospital karibu na baharini njia ya kuelekea ikulu kule kuna nafuu kidogo
 
mbona kuna huduma ya bure jamani, amwone mchungaji kakobe, mchungaji mama lwakatare, prophet maboya au hata mimi hapa japokuwa sivumi lakini nguvu ile iliyopo kwa hao niliowataja ipo pia ndani yangu. Serious, acha nimjengee imani kwanza labda atanitafuta...mwezi uliopita nilifika hospital moja ya private si kwa matibabu lakini check up kwaajili ya viza maana hiyo tu ndo inaaminiwa na hiyo nchi niliyotembelea; nika mkuta mtoto mmoja wa dada wa kihindi akiwa katika hatua ya hatari na madaktari hawana jibu dada analia mtoto hataki kula chochote na amedhoofika so wanamlisha kwa drip nika guswa na hilo jambo pamoja na kuwa huyo dada si mkristu lakini imani yake ilinitia nguvu, nikamweleza kama atapenda nimsaidie akakubali nikageuza profession hapo nakuanza kumtibu mtoto kwa utaalamu wa jina la yesu for about five minutes....jioni nilimfuatilia kwa simu akasema mtoto ameanza kunyonya baada ya siku mbili akaanza kula and now he is back to normal...

So kama atakuwa kama huyu dada asijali kuhusu yeye ni nani na mimi ni nani its an easy case just for a twinkling of an eye the problem is gone....bila hata kulipa senti moja na kubwa zaidi hata kwa mawasiliano ya pm hapa jf basi inatosha sihitaji kumjua au yeye kunijua....condition aje atoe ushuhuda hapa hapa kumpa sifa na utukufu yesu ili wale wasioamini wapate imani!

mod natafuta pa kuweka senkyuu ya pili nisaidie
 
ni doubt yangu kwamba huyu jamaa alimpa kura Mkwere na akaona sera za Dk Slaa za matibabu bure ni changa la macho,....nadhani angemchagua Dk Slaa angekuwa keshapona!!anyway pole mkuu
 
ni doubt yangu kwamba huyu jamaa alimpa kura Mkwere na akaona sera za Dk Slaa za matibabu bure ni changa la macho,....nadhani angemchagua Dk Slaa angekuwa keshapona!!anyway pole mkuu

Yeye hakupiga kura kwasababu ya ile ishu mara jina lako halipo blah blah. By the way kwani Slaa anaponya watu saivi!
 
Yeye hakupiga kura kwasababu ya ile ishu mara jina lako halipo blah blah. By the way kwani Slaa anaponya watu saivi!

dah kila kitu blah blah...dk slaa sio dk wa watu,ila alisema matibabu ni bure ndani ya sera zao..upo hapo kamanda??
 
ni kweli aende CCBRT atapata huduma nzuri na atalipa kwa uwezo wake!
 
Nina rafiki yangu ambae ndugu yake alivamiwa na majambazi na kujeruhiwa mkono. Bei ya out patient pale MOI imemkatisha tamaa kiasi kwamba inabidi akatafute huduma pengine. Bei aliyopewa MOI ni hii:

Operation fee 200,000
Accomodation kwa siku tatu 120,000
Consultation fee 20,000
Theater charges 90,000
theater drugs 15,000
Anaesthesis charges 90,000
Anaesthesian consultation fee 5,000
Lab investigation 20,000
Medication 20,000
Dressing mara mbili 10,000
Jumla kuu 590,000


Mgonjwa alishalipa 50,000 kumuona daktari. Baada ya kupewa hizi bei yamemshinda. Vidole vyake vinajiunga vibaya. Jamani wana JF naomba ushauri kwa hili. Wapi angalao aende penye unafuu maana tena watu wa chini kumudu hizo gharama si unajua tena. Tatizo liko kwenye vidole viwili tu

Mdau nimeona hii Post juu ya gharama za matibabu MOI,ninachoweza kusema ni kwamba MOI ina aina mbili au tatu za matibabu kuna matibabu ya kawaida(General) ambayo gharama zake ni za kawaida na zimekuwa'subsidized' na serikali na kuna matibabu ya 'private, ambazo mgonjwa analipia gharama halisi za matibabu kama ilivyo hospitali yoyote ya private hapa Tanzania. aina ya tatu ya matibabu ni ile ya matibabu kwa msamaha 'exemption' kulingana na miongozo iliyowekwa na serikali. Hapa wanaopata msamaha wa matibabu ni wazee wa miaka 60+,wagonjwa wa; sickle cell(seli mundu),Kisukari,ukimwi,ukoma,wagonjwa wa rufaa toka mikoani walioletwa na hospitali nyingine(eg referral from mbeya,KCMC, or redistrict and regional hospitals)wenye matatizo ya afya ya akili(psychiatry), waliougua muda mrefu sana(the poor?), watoto chini ya miaka mitano na wagonjwa wa dharura waliopata ajali (zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa wa MOI ni ajali mbalimbali) na baada ya ndugu au mgonjwa mwenyewe kujitambua huombwa kulipia gharama.

Kwa mgonjwa wa General anapohitaji upasuaji, analipa Sh. Elfu 50 tu na hiyo ina-cover accomodation hata kama atakaa wodini miezi mitatu,vipimo na baadhi ya dawa. some of the drugs atatakiwa akanunue. Na kama hana uwezo MOI kuna welfare office ambayo inapitisha mgonjwa afanyiwe huo upasuaji kwa exemption.Kwa wagonjwa wa Private, hawa wanalipia gharama halisi za matibabu kwa sababu hizi zinafuata bei ya soko lakini bado gharama hizo zinakuwa za chini ukilinganisha na hospitali kama Aga Khan, Regency au trauma Center.Mgonjwa Private analipia gharama halisi za huduma yoyote anayopatiwa, na ndio maana kwa mgonjwa wa general analipa kama kifurushi ''package'' lakini mgonjwa wa Private kama huyo wa ''Mdau Truly'' anapewa mchanganuo wa kila service anayofanyiwa kama inavyoonekana. Na huo mchanganuo, ndio unaotumika kufanya billing kimataifa na sio kwa MOI tu! Hospitali yoyote lazima ulipie, madawa ya usingizi(ambayo ni ghali sana dunia nzima), accomodation na hata muda ambao mgonjwa atakaa theater, ndio maana unaona kuna theater charges(90,0000 ina maana upasuaji utachukua saa moja na nusu, kila saa moja ni 60,000!).
Sio kama mdau pmwasyoke kwamba huo ni mchanganuo wa Kisanii.
Kwa maana hyo mgonjwa wa huyu mdau alikuwa ni mgonjwa wa private na sio mgonjwa wa general!Mgonjwa wa Private huwa ni mgonjwa ambaye yeye mwenyewe ameamua kuingia katika huduma ya aina hyo! Huduma ya general ipo kwa mtu yeyote.
Kwa hiyo naungana na mdau BABU LAO ambaye alisema "...mkuu uliingia siko.." na mdau RIWA alisema "..ameingia fast track''.
ANGALIZO: MOI ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa kwa sheria Na 7 ya mwaka 1996. Ni taasisi ya kwanza hapa Tanzania kuanzisha utoaji wa huduma kwa wa ''mseto''(Public-Private Mix) yaani kuwa na huduma za private ndani ya hospitali ya serikali. Lengo la kuanzisha utoaji wa huduma wa aina hii ni kwamba,badala ya daktari kukimbilia katika hospitali za private kutoa huduma akaacha wagonjwa ktk hospitali ya serikali,atakuwa anatoa huduma hapa hapa MOI hivyo atapata kipato na Taasisi itapata fedha.Hii pia ni njia ya kuziingizia kipato hospitali za serikali badala ya kutegemea fedha kutoka Hazina moja kwa moja kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
''Public-Private Mix'' kwa MOI ilionyesha mafanikio makubwa na ndio maana Hospitali ya Taifa muhimbili nao wakaanzisha huduma kama hyo lakni wakaiita "fast-track". Na Hospitali nyingine kama hospitali ya rufaa Mbeya na nyingine zipo katika mchakato wa kuanzisha mfumo kama huo.
Kwa hiyo sio kama alivyodai mdau Sharp Lady kwamba labda wanaosimamia huduma MOI hawana moyo wa utu,huduma au wanatumia taaluma kuwaumiza watanzania maskini, la hasha!Mdau AK-47 hajakosea kumwambia mdau Truly kwamba amtafute Almasi Jumaa ambaye ni Afisa Uhusiano, angepata maelekezo ya kina juu ya nini cha kufanya. Ofisi yake ipo chumba namba 101 na anapatikana muda wote sio kama mdau MESTOD alivyodai kwamba Almasi anaweza asipatikane!
Mdau Truly anaweza kumuona na kupata ushauri zaidi japo anasema ndugu yake kaenda CCBRT.
Pia kuna mdau ameongelea suala la MOI kutokuwa na vitanda vya kutosha! Hilo ni kweli kabisa lakn inabidi watanzania wafahamu kwamba wakati MOI inajengwa ilikuwa inakidhi mahitaji ya wakati ule, lakn kwa sasa imezidiwa. Kumekuwa na ongezeko la ajali na hivyo idadi ya wagonjwa ni kubwa sana. MOI ndio hospitali ya pekee yamifupa hapa Tanzania inayotoa huduma katika ngazi ya "Tertiary care". kwa hiyo ni hosp pekee inayotoa specialized orthopaedic and neurosurgical care kwa watanzania wote mil.40! na si kwa wakazi wa dar pekee. Hapo msongamano ni lazima. Aidha, sisi wote tunafahamu au kushuhudia ongezeko la ajali za pikipiki ambazo zinaumiza watu kwa wingi sana. MOI kwa wastani inapokea wagonjwa 10(minimum) kwa siku wa ajali za pikipiki! Halafu magonjwa ya mifupa sio kama malaria, kuhara au mengine ya medical cases ambayo yanaponywa kwa dawa na mtu anakaa siku chache sana hospitali. Ukivunjika mfupa hakuna dawa ya kuufanya uunge haraka japo huwa wagonjwa wanawekewa "implants"(vyuma au antenna)ili kuufanya uunge (in layman's language),ndio maana wagonjwa wa mifupa wanakaa muda mrefu wodini na kufanya wodi zijae sana na hivyo inakuwa shida kupata vitanda. lakini kuna baadhi ya wagonjwa mabao hulipiwa na makampuni au Bima huomba wakae siku zaidi kwa kuwa hawatoi hyo pesa mifukoni mwao na kufanya iwe ngumu kidogo kupata kitanda.
Kuhusu operesheni ya Nyonga(Total Hip Replacement-Kubadili nyonga iliyosagika kile kirungu na kikombe cha nyonga) aliyosema mdau Pmwasyoke kwamba alilipa milion4, ni sawa kwa sababu ni operesheni hyo hyo ilikuwa inalipiwa zaidi ya mil 10 mtu anapoenda kufanyiwa india. Na ssasa analipa mil4! wasio na uwezo wanalipiwa na serikali.
kwa hyo nimejifunza yafuatayo:
1. No reserach no right to speak: maana watu wameanza kuitupia lawama MOI bila kujua system ya MOI inafanyaje kazi. MOI inajali sana wagonjwa wasio na uwezo kwa kutumia system ya exemption. MOI ni hospitali pekee ambayo wagonjwa wasio na uwezo wanapatiwa dawa hata kwa kununua katika maduka ya dawa ya nje. wagonjwa wanaotoka nje ya Dar wanapatiwa kila kitu kuanzia tiba, chakula,na nauli kurudi makwao.Kama wanahitaji nurse escort,wanapatiwa kwenda sehemu yoyote Tanzania. Si hivyo tu, wagonjwa wanapatiwa vifaa kama miguu bandia,Crutches nk.
2. wagonjwa wanaingia huduma za private ambazo hawana uwezo nazo na inapofikia wakati kama huo wanapopewa gharama za malipo ndipo wanagundua kwamba hawazimudu. so, ni vema wagonjwa wakiuliza ili kupata maelezo ya kina
 
Nina rafiki yangu ambae ndugu yake alivamiwa na majambazi na kujeruhiwa mkono. Bei ya out patient pale MOI imemkatisha tamaa kiasi kwamba inabidi akatafute huduma pengine. Bei aliyopewa MOI ni hii:

Operation fee 200,000
Accomodation kwa siku tatu 120,000
Consultation fee 20,000
Theater charges 90,000
theater drugs 15,000
Anaesthesis charges 90,000
Anaesthesian consultation fee 5,000
Lab investigation 20,000
Medication 20,000
Dressing mara mbili 10,000
Jumla kuu 590,000


Mgonjwa alishalipa 50,000 kumuona daktari. Baada ya kupewa hizi bei yamemshinda. Vidole vyake vinajiunga vibaya. Jamani wana JF naomba ushauri kwa hili. Wapi angalao aende penye unafuu maana tena watu wa chini kumudu hizo gharama si unajua tena. Tatizo liko kwenye vidole viwili tu

Mimi naona aanzie tuu Kanisani kwake ili angalau wafanye fund raising. Lakini kama ni mwajiriwa TShs. 590,000 anaweza omba salary loan kazini. Thamani ya viungo vyake vinavyohitaji kurekebishwa ni zaidi ya hiyo pesa. Tatizo kubwa Watanzania wengi wanatibia kwa Sick Sheet hivyo hawajui gharama za tiba. Huyo mgonjwa kama akitaka kumwoza binti yake atatumia shilling ngapi kwenye "SEND OFF" na hizo pesa zitatoka wapi?
 
Back
Top Bottom