Bei hii pale muhimbili ( moi )yamkatisha tamaa mgonjwa

Truly

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
228
32
Nina rafiki yangu ambae ndugu yake alivamiwa na majambazi na kujeruhiwa mkono. Bei ya out patient pale MOI imemkatisha tamaa kiasi kwamba inabidi akatafute huduma pengine. Bei aliyopewa MOI ni hii:

Operation fee 200,000
Accomodation kwa siku tatu 120,000
Consultation fee 20,000
Theater charges 90,000
theater drugs 15,000
Anaesthesis charges 90,000
Anaesthesian consultation fee 5,000
Lab investigation 20,000
Medication 20,000
Dressing mara mbili 10,000
Jumla kuu 590,000

Mgonjwa alishalipa 50,000 kumuona daktari. Baada ya kupewa hizi bei yamemshinda. Vidole vyake vinajiunga vibaya. Jamani wana JF naomba ushauri kwa hili. Wapi angalao aende penye unafuu maana tena watu wa chini kumudu hizo gharama si unajua tena. Tatizo liko kwenye vidole viwili tu
 
Kuna uhitaji mkubwa sana wa jicho la tatu kufanyakazi yake haraka iwezekanavyo. Lasivyo maskini anazidi kukosa chake hata zile huduma za lazima sana hasa ukizingatia hamna anayeomba kuumwa. Khaa utadhani kila mtu anapokea bilions of money kwa mwezi na hana mahitaji mengine. MOI wekeni huduma, utu na taaluma zenu mbele tunaamini mnakutana na changamoto nyingi sana katika maisha kuanzia kwenye kipato na mengineyo ila kitendo chakutokuwa na upangaji bei unaoeleweka na wenye usimamizi mzuri huku ukireflect maisha halisi ya wanaotegemea huduma zao itakuwa ngumu kwa asiyefisadi kupata huduma ifaayo.
 
Ajaribu kumuona Almas Jumaa ni Afisa Uhusiano wa Moi aone kama anaweza kufanikiwa kukidhi vigezo vya msamaha ili apatiwa matibabu ya bure. Nchi hii bwana imekuwa ngumu mno kwa sisi tusionazo serikali haitujali ndio maana gharama hazinatofauti sana na hospitali za binafsi.
 
Tatizo hata kumuona huyo Almas, inaweza kuwa rahisi kuiona almasi yenyewe! Aende CCBRT pale huduma kidogo zipo chini.
 
yaani kwenda muhimbili ni kama kuchungulia kaburi! uongozi wa pale ni mbaya sana kuliko hospital zote duniani! and they are very slow like snales!:decision:
 
Bora MOI kuliko bei ya Dr.Ndodi gharama za matibabu yake ni kuanzia mamilioni.
 
Sisi ndo inatupasa tuandamane wali si wale jamaa wa Libya. kwao elimu ni bure from shule ya msingi hadi chuo kikuu, matibabu ni bure, kuna matabaka mawili la juu na kati chini no. maji (yasiyo na chunvi kwa wananchi), Serikali inawajengea wananchi wake nyumba ya vyumba vitatu. Na bongo vipi pamoja na raslimali mnazokuwa nazo? tuvumilie tu!
 
imagine daktari analipwa mshahara na pesa ya walipa kodi wa tanzania hapohapo unaambia consultation fee sh. 20,000 kila siku ya mungu utakapokwenda kumwona huyo daktari. Is this fair?
 
Kuna uhitaji mkubwa sana wa jicho la tatu kufanyakazi yake haraka iwezekanavyo. Lasivyo maskini anazidi kukosa chake hata zile huduma za lazima sana hasa ukizingatia hamna anayeomba kuumwa. Khaa utadhani kila mtu anapokea bilions of money kwa mwezi na hana mahitaji mengine. MOI wekeni huduma, utu na taaluma zenu mbele tunaamini mnakutana na changamoto nyingi sana katika maisha kuanzia kwenye kipato na mengineyo ila kitendo chakutokuwa na upangaji bei unaoeleweka na wenye usimamizi mzuri huku ukireflect maisha halisi ya wanaotegemea huduma zao itakuwa ngumu kwa asiyefisadi kupata huduma ifaayo.

Jamani we acha tu. Gharama ya hapo MOI imekuwa ghali kuliko hata private hospital?
 
Operation fee 200,000
Accomodation kwa siku tatu 120,000
Consultation fee 20,000
Theater charges 90,000
theater drugs 15,000
Anaesthesis charges 90,000
Anaesthesian consultation fee 5,000
Lab investigation 20,000
Medication 20,000
Dressing mara mbili 10,000
Jumla kuu 590,000

Mbona kama garama zinalenga katika huduma hiyo hiyo ya operation ila jinsi ya kudai imegawanywagawanywa katika lugha za kidhungu zaidi mmh jamani huruma kidogo ni muhimu.
 
Nina rafiki yangu ambae ndugu yake alivamiwa na majambazi na kujeruhiwa mkono. Bei ya out patient pale MOI imemkatisha tamaa kiasi kwamba inabidi akatafute huduma pengine. Bei aliyopewa MOI ni hii:

Operation fee 200,000
Accomodation kwa siku tatu 120,000
Consultation fee 20,000
Theater charges 90,000
theater drugs 15,000
Anaesthesis charges 90,000
Anaesthesian consultation fee 5,000
Lab investigation 20,000
Medication 20,000
Dressing mara mbili 10,000
Jumla kuu 590,000

Mgonjwa alishalipa 50,000 kumuona daktari. Baada ya kupewa hizi bei yamemshinda. Vidole vyake vinajiunga vibaya. Jamani wana JF naomba ushauri kwa hili. Wapi angalao aende penye unafuu maana tena watu wa chini kumudu hizo gharama si unajua tena. Tatizo liko kwenye vidole viwili tu

Mbona mchanganuo wa gharama umekaa "kisanii"?

Tofauti ya "Operation fee 200,000" na (Theater charges 90,000 + theater drugs 15,000 + Anaesthesis charges 90,000) ni NINI?
 
MOI paone hivivi. Kuna ndugu yangu alifanyiwa operation ya nyonga hivi karibuni. Alilazwa kwa muda wa kama wiki 1. Operation ililipiwa milioni 4 na kulikuwa na malipo mengi mengine ya ziada, pamoja na kununua mafimbo ya kufanyia mazoezi ya kutembea tena.
 
Cha kushangaza ni kwamba kupata kitanda MOI ili ulazwe ni noma, licha ya gharama zao. Hivyo hawana hata motisha ya kupunguza bei.
 
Cha kushangaza ni kwamba kupata kitanda MOI ili ulazwe ni noma, licha ya gharama zao. Hivyo hawana hata motisha ya kupunguza bei.

Mkuu hilo umenena maana mkwe wangu ilimchukua miezi miwili kupata kitanda tena hicho ni cha private
 
MOI paone hivivi. Kuna ndugu yangu alifanyiwa operation ya nyonga hivi karibuni. Alilazwa kwa muda wa kama wiki 1. Operation ililipiwa milioni 4 na kulikwa na malipo mengi mengine ya ziada, pamoja na kununa mafimbo ya kufanyia mazoezi ya kutembea tena.

Da! basi kwa mtindo huu wa kipato cha chini itakuwa ni ishu kupata matibabu hapo MOI.Sikujua pako hivyo mpaka leo hii niliposhuhudia mwenyewe baada ya kupewa hilo karatasi la gharama nikapata shock
 
Mbona mchanganuo wa gharama umekaa "kisanii"?

Tofauti ya "Operation fee 200,000" na (Theater charges 90,000 + theater drugs 15,000 + Anaesthesis charges 90,000) ni NINI?

Kweli ni full usanii. Kwenye hiyo theater charges si na hiyo anaesthesis charge ingekuwemo humo.
 
Sisi ndo inatupasa tuandamane wali si wale jamaa wa Libya. kwao elimu ni bure from shule ya msingi hadi chuo kikuu, matibabu ni bure, kuna matabaka mawili la juu na kati chini no. maji (yasiyo na chunvi kwa wananchi), Serikali inawajengea wananchi wake nyumba ya vyumba vitatu. Na bongo vipi pamoja na raslimali mnazokuwa nazo? tuvumilie tu!

Kweli mkuu. Libya kama huduma wanapata fresh tu, hadi mtu akioa anajengewa nyumba ya 3 rooms? naona wamemchoka tu Gaddaf ila huduma wanapata. Ishi sisi huku bwana, huduma zenyewe bei mbaya mpaka mgonjwa anakata tamaa. Nahisi kama ni kulogwa basi huyo mganga kafa. Bongo shida kibao lakini kuandamana walaaa! watu wengi wanatamani kuandamana ila wa kulianzisha ndio hamna.
 
Cha kushangaza ni kwamba kupata kitanda MOI ili ulazwe ni noma, licha ya gharama zao. Hivyo hawana hata motisha ya kupunguza bei.

Pale nimeshapaona hovyo sasa. Parking yenyewe hata hamna, watu wanashushwa njiani na ukumbuke wengi wana maumivu ya viungo wanaweza wagongwe tena mara ya pili maana hawawezi kuharakisha. Ukisikia bei utadhani hiyo huduma ni kama ulaya kumbe!! Wanakera sana hebu washushe bei bana khaaa!
 
Back
Top Bottom