Bei hasi ya umeme kwa watumiaji na tozo ya capacity charge ndio moja ya sababu za IPTL kunyimwa leseni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Soma habari kamili:

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imekataa kuiongezea muda wa leseni Kampuni ya Kufua Umeme wa Independent Power Tanzania Limited (IPTL) baada ya leseni yake ya kuzalisha umeme kumalizika muda wake.

Kwa mujibu wa tangazo la Ewura, lililotolewa kama taarifa kwa vyombo vya habari na kuchapishwa ndani ya gazeti hili, maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura kilichofanyika Agosti 30, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Machi 28, mwaka huu, Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) iliwasilisha kwa Ewura maombi ya kuongeza muda wa leseni ya kuzalisha umeme kwa miezi 55 kuanzia Julai 16, 2017 hadi Januari 15, 2022.

“Bodi ya Wakurugenzi ya Ewura katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Agosti 2017, imefikia uamuzi wa kukataa maombi ya kampuni ya IPTL baada ya kuzingatia mambo yafuatayo,” ilieleza taarifa hiyo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura.
Iliyataja mambo yaliyozingatiwa na bodi hiyo kuwa ni athari hasi kwenye bei ya umeme kwa watumiaji endapo muda wa leseni ya IPTL ungeongezwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa malipo ya ‘capacity charge’ kwa kiasi cha dola 2.667 milioni kwa mwezi; pingamizi kutoka kwa umma na wadau mbalimbali; na migogoro na kesi mbalimbali za kisheria zinazoendelea zikiihusisha Kampuni ya IPTL.

IPTL ilikuwa na mkataba wa miaka 20 ambao ulimalizika Julai 16, mwaka huu, na kwa miaka yote hiyo imekuwa ikiiuzia umeme serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kutumia mitambo hiyo ya kufua umeme iliyoko eneo la Salasala Tegeta jijini Dar es Salaam.

Lakini katika miaka ya karibuni, kampuni hiyo imejikuta katika mzozo na wamiliki wake, serikali, umma kwa upande mwingine kutokana na kuonekana ‘kuinyonya’ nchi katika malipo hayo ya umeme ambao unaonekana kuuzwa kwa bei ya juu kuliko uhalisi wake hasa suala la ‘capacity charge.’

Aidha, kumekuwapo na kesi zinazoendelea mahakamani kuhusu umiliki wa kampuni hiyo baada ya kuuziana hisa.

Pia hivi karibuni waliokuwa wabia katika IPTL, Harbinder Singh wa Kampuni ya PAP na James Rugemalira wa VIP Engineering Limited wako mahakamani wakishitakiwa kwa uhujumu wa uchumi na kutakatisha fedha.

Chanzo:HabariLeo

Hivi unaweza kuomba kuongezwa leseni kama huna mkataba?

Kati ya leseni na mkataba kipi kinaanza?

Japo mkataba ni mbovu,lakini sababu hizo za kuwanyima leseni zina nguvu kisheria?

Hivi huu mkataba hauna namna ya kuuvunja au kuurekebisha?

Tusitafute short cut bali tuanze kurekebisha hii mikataba vinginevyo tutakuwa tu tunaaihirisha matatizo na si kuyatatua.
 
Kwasababu hizi hawa jamaa wakienda mahakamani tutabaki salama?

Hiyo tozo ya capacity charge ndio tumeijua leo?

Soma habari kamili:

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imekataa kuiongezea muda wa leseni Kampuni ya Kufua Umeme wa Independent Power Tanzania Limited (IPTL) baada ya leseni yake ya kuzalisha umeme kumalizika muda wake.

Kwa mujibu wa tangazo la Ewura, lililotolewa kama taarifa kwa vyombo vya habari na kuchapishwa ndani ya gazeti hili, maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa Ewura kilichofanyika Agosti 30, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Machi 28, mwaka huu, Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) iliwasilisha kwa Ewura maombi ya kuongeza muda wa leseni ya kuzalisha umeme kwa miezi 55 kuanzia Julai 16, 2017 hadi Januari 15, 2022.

“Bodi ya Wakurugenzi ya Ewura katika kikao chake kilichofanyika tarehe 30 Agosti 2017, imefikia uamuzi wa kukataa maombi ya kampuni ya IPTL baada ya kuzingatia mambo yafuatayo,” ilieleza taarifa hiyo ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura.
Iliyataja mambo yaliyozingatiwa na bodi hiyo kuwa ni athari hasi kwenye bei ya umeme kwa watumiaji endapo muda wa leseni ya IPTL ungeongezwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa malipo ya ‘capacity charge’ kwa kiasi cha dola 2.667 milioni kwa mwezi; pingamizi kutoka kwa umma na wadau mbalimbali; na migogoro na kesi mbalimbali za kisheria zinazoendelea zikiihusisha Kampuni ya IPTL.

IPTL ilikuwa na mkataba wa miaka 20 ambao ulimalizika Julai 16, mwaka huu, na kwa miaka yote hiyo imekuwa ikiiuzia umeme serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kutumia mitambo hiyo ya kufua umeme iliyoko eneo la Salasala Tegeta jijini Dar es Salaam.

Lakini katika miaka ya karibuni, kampuni hiyo imejikuta katika mzozo na wamiliki wake, serikali, umma kwa upande mwingine kutokana na kuonekana ‘kuinyonya’ nchi katika malipo hayo ya umeme ambao unaonekana kuuzwa kwa bei ya juu kuliko uhalisi wake hasa suala la ‘capacity charge.’

Aidha, kumekuwapo na kesi zinazoendelea mahakamani kuhusu umiliki wa kampuni hiyo baada ya kuuziana hisa.

Pia hivi karibuni waliokuwa wabia katika IPTL, Harbinder Singh wa Kampuni ya PAP na James Rugemalira wa VIP Engineering Limited wako mahakamani wakishitakiwa kwa uhujumu wa uchumi na kutakatisha fedha.

Chanzo:HabariLeo
Hivi wewe na akili yako unadhani ombi ni agizo?
 
Hii kampuni haikuongezewa muda wa mktaba?

Hili ni gazeti la serikali kumbuka.
 
Usikurupuke kijana kinachoombwa hapa ni leseni tu lakini kumbuka kuwa hapa kuna mkataba uliosababisha kuwepo kwa huo mtambo, je unalijua hili?
Na mimi nadhani ukiisha kuwa na mkataba leseni ni formality tu.... yaani unatakiwa uipate automatic. ..... kuna jambo limefichwa hapa....
 
Usikurupuke kijana kinachoombwa hapa ni leseni tu lakini kumbuka kuwa hapa kuna mkataba uliosababisha kuwepo kwa huo mtambo, je unalijua hili?
EWURA wanahusika na utoaji wa leseni tu hiyo mikataba wanajua pa kwenda kuiulizia wenyewe.
Hivi ikitokea umekodi sehemu ya biashara na umelipa kodi ya pango na kila kitu lakini ukakosa leseni ya kazi yako(leseni ya biashara) unaweza endelea fanya kazi yako au utafunga?
 
Nchi haiko salama mkwa wawekezaji, Pamoja na IPTL kutuibia, hii sio njia sasa ya kuwatoa kwenye kazi yao,

Inafanya wawekezaji wengine waogope kuja, maana Nchi inaamua kufanya kama inavyofanya kwa IPTL, haishindwi kumfutia Leseni muwekezaji yeyote kwa sababu yoyote watayayo ona inafaa.

Kama bei kubwa ya Umeme wao, unatafuta Muwekezaji mwingine, huyu ukiwa umemalizana kiutaratibu, hii njia itatugharim baadae. Huyu mtu anamkataba mpaka miaka kaghaa ijayo, hajashindwa kumaliza hiyo Miaka, ni wewe ndio unasababisha asifike, IPTL hawatashtaki Tanesco wala EWURA, kama wale wa barabara aliweza kushtaki Serikali ya Tanzania na hawa watashindwaje kutushtaki? Kama ingekuwa IPTL kazi imewashinda hakuana wa kupinga, hawa IPTL wanatuhumiwa kuchaji bei kubwa sana, ni sawa bei yao kubwa,

Mkataba unasema bei ikiwa kubwa uwanyime leseni?
Mkinyima Leseni na mkataba wake utakuwa umevunjika?

Mnashindwa nini kuingia na kuupitia Mkataba? kama IPTL wanawauzia Umeme bei kubwa kuliko Makubaliano kwenye Mkataba wenu kwanini msikae na kuuvunja kwa IPTL kukiuka vipenge vya Mkataba?
 
Kwa sasa hakuna namna..
Lazma mkataba wa TANESCO na IPTL lazma uvunjwe..
Sababu ni moja tu..
IPTL kashindwa kutimiza mahitaji ya mkataba...
Na mahitaji ya mkataba ni yeye kupeleka umeme TANESCO...
Sisi hatuangalii umeme atautoa wapi..
Sisi tunataka apeleke umeme TANESCO
sasa yeye kashindwa kupeleka...
So hapo mkataba unatoa mwanya wa kuvunjwa kwake...
Kingine..
Ni kuwa hakuna shughuli inayofanywa bila kuwa na leseni...
Na leseni ina uhai ambao unahuishwa kila baada ya muda fulani..
So ikiisha lazma uombe....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom