singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SERIKALI imesisitiza azma yake ya kuweka bei elekezi ya ada kwa shule binafsi nchini na kuwataka wawekezaji wa shule hizo wawe na mitaji badala ya kutegemea ada kubwa wanazotoza kwa kuwa elimu sio biashara bali ni huduma.
Hayo yamebainishwa jana mjini hapa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo (Chadema) aliyehoji sababu ya serikali kuweka bei elekezi ya ada kwa shule binafsi.
Lyimo alisema sio sawa kwa serikali kuja na bei elekezi ya ada katika shule hizo ilhali ubora wa elimu ni mkubwa. “Ninataka serikali itoe sababu ya kuweka bei elekezi ilhali ubora wa elimu utolewayo ni mkubwa, tumeshuhudia ndani ya miaka 10 mfululizo shule hizi zimekuwa zikiongoza kwa ubora,” alihoji Lyimo.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Manyanya alisema ni lazima serikali iweke bei elekezi ya ada kwa kuwa shule hizo zinatoza bei tofauti ukilinganisha na ubora wa elimu itolewayo. “Bei elekezi ni lazima tuweke na wamiliki wanapaswa kujua elimu ni huduma inayochangiwa na sio biashara, mfano tu kuna shule binafsi ya Figwa, Rukwa inatoza ada ya Sh 100,000 na kuna shule ya Feza, Dar es Salaam inatoza ada milioni 9.4 sasa lazima kuwe na ada elekezi,” alisema Manyanya.
Akitoa mifano mingine ya baadhi ya shule binafsi nchini zinazotoza ada kwa kiwango tofauti na wakati mwingine ada hizo ni kubwa kuliko uhalisia wa maisha ya wananchi wengi, aliitaja kuwa ni Shule ya Idigome ya Mbozi, Songwe inayotoza ada Sh 100,000, Azovu ya Nkasi, Rukwa inayotoza ada Sh 100,000.
Aliendelea kutaja shule nyingine kama vile Shule ya Msingi Imani inayotoza ada Sh milioni 5.9, Shule ya Alliance, Mwanza inayotoza ada Sh milioni 4.8 na Shule ya Msingi Alpha inayotoza ada Sh milioni 4.8.
“Sasa kwa hali hii ni lazima tuweke ada elekezi kwa sababu ada zinazotozwa zinatofautiana kwa kiasi kikubwa kulingana na huduma zinazotolewa, hata Mamlaka ya Maji na Nishati (Ewura), nao wanatoa bei elekezi,” alisisitiza.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) aliyehoji upangaji bei elekezi za ada kutasababisha ubora wa elimu kuporomoka na kutaka serikali ifafanue jambo hilo, Naibu Waziri alisema serikali ilifanya utafiti wa gharama za kusomesha mwanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari na kubaini ada zinazotozwa kwenye shule hizo binafsi zinatofautiana kwa kiasi kikubwa kulingana na huduma inayotolewa. Hata hivyo, wizara hiyo ilifanya mazungumzo na baadhi ya taasisi zinazosimamia shule hizo binafsi na wamekubaliana jinsi ya kufikia viwango vya ada elekezi.