Bei elekezi kwa Cement 42.5 kwa Dar inawatajirisha Mawakala wa cement

entrepreneur2005

New Member
Nov 18, 2020
1
20
Serikali imeweka bei elekezi kwa cement kwamba isizidi 15,000 kwa mfuko mmoja. Bei hiyo haijalishi ni cement aina gani. Kuna aina kuu mbili zinazouzwa ambazo ni 42.5 na 32.5. Kwa wajenzi wengi cement ya 42.5 ndio inapendwa lakini bei yake ipo juu.

Kwa wauzaji wa rejareja bei elekezi ya 15,000 kwenye cement 42.5 haina faida yoyote. Naamini serikali inaweka mkakati ili kwenye ujenzi wa kawaida huku mitaani itumike 32.5 na hiyo ya 42.5 iende kwenye miradi mikubwa kama SGR, NYERERE DAM, TANZANITE BRIDGE n.k well and good, lakini mawakala wa cement wameamu kuuza wao kwa bei elekezi 42. 5@15,000 na 32.5@14,500.

Ina maana wenye maduka madogo wengi hawataweza kufanya biashara na watapunguza wafanyakazi wao huku mawakala wakifaidi soko walitongenezewa na serikali.

Nimefanya utafiti huu kwa kukagua maduka na mawakala kutoka Ferry-Kigamboni mpaka Mikwambe.

Hoja hujibiwa kwa hoja.
Cheers.
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
4,616
2,000
Hili suala. Eti. La cement eti 42.5,ni mkumbo tu, mbona watu wamejengea hiyo ya 32.5 miaka yote hiyo na ubora upo, ila huu upepo eti wa kujengea 42.5 ndio umevuma sasa!!? Kwa nyumba za kawaida naina maana sana!!
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
7,024
2,000
😂 Ahahahaaa ...

Eti bei elekezi, kuna kitu nyuma ya pazia lazima mlipe bili utake usitake na wapi pametumika ili waleti iliyopungua iweze kujaa ndipo hapa tunaanzia kwenye cement.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom