Samahani waungwana ila a few monts ago nimeanza kubugia pombe kama maji. Nilikuwa nimemwamini sana mke wangu. nilimpa asilimia mia moja. nami baada ya ndoa sijawahi kumsaliti sasa yeye kaamua kutoka na my best friend. jamaa yangu kawaona live wanatoka guest house akaja kunambia. mimi nilikuwa na mashaka na mahusiano ya mke wangu na rafiki yangu tangu muda mrefu kwa sababu nikiwa na mke wangu nikikutana na rafiki yangu mwizi, mke wangu anaangalia chini na hawezi kabisa kumtizama jamaa. sasa imethibitika mke wangu anananihiwa na rafiki yangu. Sijamwambia kitu hadi sasa ila nimeanza kunywa pombe kama maji. Na hapa JF naomba msinishauri kuâcha pombe. Nimeweka thread hii kuwatahadharisha wale wenye ujinga kama wangu wa kumwamini mke 100%. Samahani yawezekana kuna wanawake waaminifu pia. Ila nimeacha kabisa kufanya the needful na mke wangu. hata akiwa uchi namwona kama mwanamme mwenzangu tu. Sijui kama nitakuja kugusa K maishani. Kila nikijisikia kudo nakamata bia. Kwaherini akina dada. Ninajua JF mna hekima na busara ila kwa sasa sihitaji ushauri wowote. Am married to vodka. Nawaasa tu wale walioweka 100% kwa wake zao. YAMENIKUTA. Naomba kuwasilisha wakuu.