Beginner Level : Je, Online Freelancing ni nini? Kazi zinatoka wapi? Ni Skills gani zinahitajika? Nitalipwaje pesa? Jifunze kila kitu hapa

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
767
1,655
Greetings JF massive!

Karibu tena katika darasa la leo ambapo leo ni siku mahususi kwaajili ya biginners wanaotaka kuanza kufanya kazi kama Online freelancer lakini hawafahamu Online freelancer ni nini, ujuzi gani unatakiwa uwe nao lakini pia je kama ukifanya kazi pesa yako utalipwa vipi?

Watu wengi wamekuwa wakiniuliza maswali mengi kuhusu Online freelancing, wengine wamekuwa wakienda mbali nakusema si kitu haiwezekani kuwa freelancer ukiwa Tanzania na mambo kama hayo. Lakini niseme tu kukosa taarifa sahihi na ujinga ndiyo tatizo kubwa hadi inasababisha baadhi ya watu kujaribu kupinga kila positive kinachofanyikia mtandaoni wasijue sasa hivi, nikiongelea upande wa employment waajiri wengi wanachagua kuajiri Online kuliko traditional hiring iliyozoeleka.

Sababu hapo ni simple tu.

Ni gharama nafuu kumuajiri Online Based freelancer akufanyie project yako.

Pia ni rahisi kupata “perfect candidate” kama Employer ataamua kuajiri Online Based Freelancers kwasababu anachaguo kubwa kuangalia nani anamfaa kati ya candidates waliotuma maombi toka sehemu tofauti duniani.

Angalia hii survey ya UpWork

IMG_7228.JPG


Ok baada ya kusema haya sasa naomba tuanze darasa letu la leo.

1 • Je, Online Freelancing ni nini hasa?

Online freelancing kwa lugha rahisi maana yake ni kufanya kazi ya mtandaoni kwa kutumia ujuzi/skill uliyonayo na wewe kulipwa pesa.

Ujuzi huu unaweza kuwa

a) kutambua na kuondoa makosa ya kimaandishi katika katika article ya Kiswahili au kiingereza (proofreading)

b) data entry

c) vitual assistant service ( kuwa mfanyakazi wa kampuni fulani ukifanyia kazi zako home. Kazi hizi mara nyingi ni ku-deal na customers. Kupiga simu, kutuma emails/kujibu etc)

d) Facebook Advertising (kusaidia watu Ku-manage Facebook advertising campaign)

e) logo & business card design

f) web development & IT

g) programming

h) research

i) article, ghost writing

j) digital marketing

k) na ujuzi mwingine tofauti tofauti

Kazi hizi zinapatikana baada ya wewe kujiunga na freelancing site uliyochagua kama vile UpWork, Fiverr, Freelancer.com, Guru na site nyingine nyingi.

Kwa kawaida kujiunga ni bure.

Lakini katika site kama UpWork maombi yako ya kujiunga yanaweza kukataliwa iwapo hutoweza kuwa na Skills zenye demand. Hapa inabidi uwe mindful. Kama huna Skills zenye demand unaweza kwenda Guru au Freelancer.com utakubaliwa haraka tu.

2 • Kazi zinatoka wapi?

Kazi zinazopatikana kwenye site nilizozitaja hapo juu zinatumwa na client (waajiri) wanaohitaji kufanyiwa kazi zao na kukulipa pesa.

Kwa kawaida client akiweka tangazo la kazi (project) anayotaka afanyiwe huwa inaonekana hivi.

IMG_7232.JPG



Au inaweza kuwa project ya muda mrefu kama hii

IMG_7233.JPG



Hapo kazi ya kwanza clinet anatafuta mtu wakumuandikia mashairi ya Kiswahili kwa $10

Kazi ya pili ni kazi ya muda mrefu miezi 6+ na kazi hapo ni kutoa support kwa wanafunzi wanaojifunza Kiswahili mtandaoni.

Je, haya hiyo itakushinda?

3 • Ni Skills gani zinahitajika?


Hapa kwenye Skills niseme tu zipo nyingi.

Hapo number 2 unaweza kuona aina za kazi zinahitaji Skills kama vile kufahamu lugha ya Kiswahili, kufahamu Online support, kufahamu kiingereza pia.

Lakini mbali na hapo unaweza kuwa na Skills kama vile logo design, article writing, vitual assistant, researcher, digital marketer, Ms Excel, web development, translation na Skills, voice over artist na Skills nyingine nyingi.

Iwapo huna skills unaweza tumia muda wako kujifunza ili ukijisajili upate kazi kweli.

Kumbuka kuna na skill inayouzika (yenye demand) ni muhimu. Hautoweza pata kazi kama wewe ni mediocre.

4 • Nitalipwaje Pesa baada ya kufanya kazi?

Kwanza kabisa ulifanikiwa kupata kazi kiasi cha pesa uliyokubaliana na client kitawekwa katika escrow account. Maana ya escrow account ni Account inayoshikilia pesa ili ukikamilisha kazi ipelekwe sasa kwenye Account yako tayari kuhamishwa kwenda kwenye bank account yako.


IMG_7221.JPG



Kumbuka wakati unajisajili ukishakimisha accout yako itaweza kuchagua njia ya wire transfer kama njia ya kupokea malipo na utaweka details za bank account yako.

Kama utakauwa unahitaji msaada niandikie.

5 • Neno la mwisho.

Kama nilivyosema awali Online freelancing inahitaji kwanza kuwa na Skills utakazoweza kumshawishi client kwamba wewe ni perfect candidate.

Kama wewe ni article writer au translator inabidi kweli ufahamu nini unachokifanya.

Kama hujaiva usione uvivu wakujifunza zaidi. Usikurupuke tu ukaenda kujisajili ukidhani ukimwandikia client proposal atakupatia kazi kisa umesema wewe ni translator. Je, akikupa “test” utafuzu?

Alright.

Kwa leo niishie hapa.

Unahitaji kujifunza zaidi? Niandikie makingmoneyonlinetz@gmail.com

Tukutane tena katika darasa jingine amazing kama hili.

Cheers 🥂
 
Wakuu upwork mnapataje kazi profile yangu tayari nimeiweka Sawa shida kupata client
 
mkuu mimi nina interest sana ya kufanya kaz kama izi za kwenye computer maana pia napenda sana kutumia computer...ila sasa sijasomea mambo ya computer japo najiona kabisa nikipata mtu akani brash ni kama vile nitaweza....je, kwa haya niliyoyaeleza naweza kuwa proffessional kweli kama ninavyofikiria endapo nitapata lesson?? na vip kuusu upatakanaji wa seem za kujifunza??? naweza chukua mda gan mpaka kuja kuwa atleasts na idea kidogo za kufanyia kazi??
asante
 
Back
Top Bottom