Beda baada ya ukabila sasa umehitimisha kwa kumweka Eric mwanao kuila UCC?

nakupinga kwa hilo, nimetoa oni most of engineering students by that time wa hayan na km walitoa wanfunzi kutoka engineering what did you expect?is to get many hayas
 
Ni kweli kuna malalamiko pale UCC-UDSM kwamba idadi ya wahaya inakuwa kubwa.Lakini pia ni lazima tujiulize kuwa ni wapi tunachora mstari kuwa wahaya wamezidi???.
Pili mafanikio ya Prof.Beda pale UCC kamwe hayamfanyi asiwe mkabila(anayependelea watu wa kabila lake).Inawezekana kabisa kuwa Prof.Beda amesaidia sana kukua kwa UCC lakini hilo halimtakasi kuwa yeye si mkabila! Kwa hiyo basi kuna haja ya kulifanyia uchunguzi wa kina ni kwa nini idadi ya nikugambirege inakuwa kubwa siku hadi siku pale UCC au je ni kweli kuwa wahaya ndiyo wao wanaijua computer kuliko makabila mengine?.Kumbuka kuwa ile si mali ya Beda na familia yake au ya wahaya bali ni mali ya watanzania wote.Hivyo basi watanzania wanayo haki ya msingi kufuatilia kulikoni!

Tatu kama huyo bwana mdogo Eric anakiuka maadili ya kazi kwa kuwanyanyasa au kuwadhalilisha wafanyakazi wengine ati tu kwa sababu baba yake ndiye mkuu wa kitengo basi ni kazi raisi sana kumnasa kwenye mtego.Tumieni kila aina ya tecknologia kama vile tape recording,kamera, na kadhalika ili kupata ushahidi halafu muuweke kwenye umma wa watanzania waamue wenyewe.

Nne naona umefika wakati sasa kwa watanzania kuamka na kuwafunua wote wanaondekeza mambo haya ya ukabila,udini,uhindi,uchina na kadhalika.Na hii haijali kama mtu ni profesa au ni waziri au mdosi au nani wawekeni hadharani hawa wabaguzi mambo leo ili tule nao sahani moja.Tumechoka kubaguliwa kwa rangi zetu,kabila zetu,dini zetu,nywele zetu,macho yetu,lafidhi zetu na kadhalika!!

Wembe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom