Mjadala huu hauna tofauti na ule wa TRA na mingine ya aina hii tuliyowahi kuiona hapa JF.
Mleta hoja na wengine wanaomuunga mkono wametoa ushahidi wa kuwepo wahaya wengi hapo UCC kuwa ni ushahidi unaojitosheleza kuhitimisha kuwa pale pana ukabila. Hiki ni kigezo kimoja mhimu, lakini nadhani hakiwezi kujitosheleza kuhitimisha kuwepo kwa ukabila bila ya kuwa na vidokezo vingine vinavyokijengea nguvu.
Mimi ningependa tupewe ushahidi unaoonyesha kwamba kuna watu walionyimwa haki yao ya kuajiliwa au kupewa huduma kwa sababu tu ya ukabila uliojijenga pale UCC.
Inaudhi na inachukiza sana kama watu bado wanafanya upendeleo kwa misingi hii ya kiukabila na kiaina nyingine yoyote.
Kufanya kazi kwa bidii, au kusifika kwa umahiri wa kiongozi hautoshi kama kiongozi huyo anayo roho ya kibaguzi. Watu aina hiyo hawafai kuongoza.