Beckham atuma salam....

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Kiungo anayeaminika kumwaga majalo yenye upako Daudi Yusuph Robert Beckham juzi alianza ktk kikosi cha kwanza cha klabu yake ya sasa ya AC Milan na kuisaidia klabu hiyo yenye vikombe vingi zaidi vya kimataifa kuliko klabu yoyote ile kupata ushindi wa goli 5 ktk mchezo wa ligi ya Serie A...

Ktk mechi hiyo Becks alionekana akiwa yuko fiti na akiwa ktk munkari wa kuwasubiri vibonde hiyo February.

Pia ktk mechi hiyo kiungo mshereheshaji muheshimiwa Ronaldo de' Asis Moreirra al-maaruf kama Ronaldinho Gaucho alitambulisha chenga mpya ikiwa ni utamaduni aliojijengea kwa siku za hivi karibuni.

Inaaminika chenga anazopiga Dinho kwa sasa haziwahi kupigwa na mtu yeyote duniani.

Wataalamu na wachambuzi wa maswala ya soka walipata kuweka wazi kuwa ''kama mpira ungekuwa unaongea basi ungesema kuwa kila dakika ya mchezo upelekwe kwa Dinho ili akauchezee na washabiki wafurahi''.

Mapema Mwezi ujao Milan watakutana na Manchester UTD ktk dimba la Sansiro, Dimba ambalo ni kama machinjio ya Manchester na ndiyo mechi ambayo Becks anaisubiri kwa hamu.

FORZA MILAN
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom