BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,006
Yaani hivi waTanzania tunafurahishwa na hili la dada, watoto, zetu kwenda kuanikwa uchi kwenye haya ma playboy sijui manini? Jee, huu ndio ustaarabu? kama kujiweka uchi ni ustaarabu basi mbuzi, paka na mbwa ni wastaarabu kuliko sisi, wao daima wako uchi.
Yaani hivi waTanzania tunafurahishwa na hili la dada, watoto, zetu kwenda kuanikwa uchi kwenye haya ma playboy sijui manini? Jee, huu ndio ustaarabu? kama kujiweka uchi ni ustaarabu basi mbuzi, paka na mbwa ni wastaarabu kuliko sisi, wao daima wako uchi.
Ukifikiri sana hao mbuzi,paka na mbwa ni wastaarabu kuliko sisi binadamu! Lini umesikia kuna fisadi anatoka katika hao? Haya ya kutembea uchi, ni uhuru wao. Tusiwaingilie ili mradi wamefanya kwa hiari yao na ni watu wazima na hawamdhuru mtu mwingine.
Kama wewe huoni kuwa ni ufisadi kuwaweka wanawake uchi na kuwafanya ndio njia ya kuuza magazeti au bidhaa nyingine basi tunapishana sana kimtazamo na labda ni kuwa haujuwi maana ya ufisadi ni nini.
Hakuna hiyari kwenye mambo ya aibu ya kuwa weka hawa kina dada na mama zetu uchi ila tu kwa watu wasiokuwa na maadili na wale ambao sheria za nchi zao wamezifanya zikubali upotofu wa maadili na hawafati sheria za dini zao.
Jee, dada yako au mama yako utakubali afanye hivyo? kwa kuwa kapenda mwenyewe na ni mtu mzima?
Nifahamishe mbwa,paka au mbuzi gani amefanya ufisadi? Pengine kweli nahitaji shule ya neno fisadi. Nitashukuru ukinifahamisha.
Mama yangu au dada yangu akiamua kufanya hivi, mimi nani nimzuie? Au hauamini kuwa wao ni watu wazima wenye haki ya kufanya maamuzi wenyewe? Tunapoteza wakati kuchachamalia ya kijinga kama haya wakita yaliyo maovu zaidi tunayachangamkia! Jamii inayowaua bibi vizee kwa ajili wana macho mekundu, tunaowafanyisha kazi watoto wadogo, tunaowaangalia watoto wadogo wakijiuza kwenye mabaa yatu, tunaowachoma moto wale tunaowahisi wameiba kuku, tunaowatembeza tumbili mtaani tukiwa tumewafunga minyororo shingoni na vidonda vya bakora mwilini kama burudani, tunaoua watoto wetu kwa sababu ni vilema, tunaowaua wake zetu kwa kuamini kuwa wametuvunjia heshima, tunaowafungia jirani zetu katika nyumba na kutia kibiriti kwa vile si kabila yetu, tunaomchinja mtu hadharani kwa sababu tu si dini yetu na mengine mengi unaiita imestaarabika kuliko hao wanyama uliowataja? Kama unaona vitendo vya hawa mabinti haviendani na maadili yako kwa nini umenunua Play Boy? Si ungelipita tu na kuwaachia wenye haja nalo walinunue? Tusiwaingilie watu ati kwa sababu vitendo vyao haviendani na dini ZETU, maadili YETU ili mradi wana umri wa kutosha wa kufanya maamuzi wenyewe na wamefanya hivyo kwa hiari yao. Kama ni ndugu yako au rafiki yako anayefanya hivi, na wewe haufurahii anachokifanya basi usimkaribishe kwako.
Kama muono wako ndio huo wa kuweza kukubali mama yako na dada yako wapigwe picha za uchi na kuanikwa kwenye magazeti ya ngono. Sina cha kubishana na wewe kuhusu hilo na umeshinda hoja.
Sina taimu ya kukuelimisha kuhusu ufisadi naomba kajifunze mwenyewe.
Paka fisadi ni yule a) anaechomoa samaki kikaangoni wakati kipo jikoni (paka Mwizi) b) paka fisadi ni yule anaefanya ngono hadharani bila kujificha na kikwetu hapa dar ukiona paka namna huyo ni uchuro.
Kuhusu Mbwa na Mbuzi ukisha yaelewa hayo juu nadhani utapata jibu na kama hujapata jibu utajijuuuu.
Yaani hivi waTanzania tunafurahishwa na hili la dada, watoto, zetu kwenda kuanikwa uchi kwenye haya ma playboy sijui manini? Jee, huu ndio ustaarabu? kama kujiweka uchi ni ustaarabu basi mbuzi, paka na mbwa ni wastaarabu kuliko sisi, wao daima wako uchi.