Beatrice Shimeda: Rais Magufuli nisaidie, nasubiri kufa tuu

Bwana Mapesa

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
2,551
1,777
Hayo ni neno ya Mama Beatrice Shimeda (54) , mkazi wa Kibamba.Mama huyu amepatwa na maradhi ya ajabu ambayo kama jitihada za kumsaidia hazitofanyika basi mguu huu unaweza kupelekea kupoteza uhai wake.

Ameishi na maradhi haya kwa muda wa miaka 21 sasa, anatakiwa kwenda kupata matibabu India ila hana pesa hivyo kupitia Global Tv ameona bora amuombe msaada Rais.

Imeniuma sana nimeamua kushare na wanajf juu ya hili, najua uwezo wa kumsaidia upo, yeyote alieguswa na hili kuna namba za simu zimetolewa kwenye video hapo chini.

Tunayo nafasi ya kurudisha tabasamu usoni kwa Mama Beatrice, tabasamu ambayo ameikosa kwa muda wa miaka 21 sasa.

Dini ya kweli ni kusaidia Wajane na watoto.

Yeye kutwa kucha anaangalia SHILAWADU atajuaje msipowaambia shilawadu
Kaka mimi si mwanafamilia ni msamaria ambaye nimeguswa na tatizo la huyu mama naamini hata Shilawadu wanayo nafasi ya kulijua hili kupitia bandiko hili au mimi na wewe, msaada si lazima pesa.By the way ni wazo zuri.
 
Mlengwa ni Rais Magufuli, yeye huangalia shilawadu, ukitaka ujumbe umfikie mapema, wajulishe SHILAWADU, kisha jiandae watafika haraka tu.
 
Hapa ndio naona raisi wangu atapata shida,akimsaidia huyu kesho ataibuka mwingine. Na keshokutwa mwingine tena
ni muhimu sasa kutengeneza mfumo rasmi kupitia bima za afya,maana hata yy kutoa fedha zake mfukoni kila siku atachoka.
 
Yeye kutwa kucha anaangalia SHILAWADU atajuaje msipowaambia shilawadu
Unanongwa ka mchawi.....
Kila mtu anacho akipendacho....kutwa kucha ulimuona wapi.....kama hupati dhambi ya kutunga....kwani wanaokutumia wamekuambia mchafue....tu.....
Unajua hata kwenda kunya ni kutoa uchafu....ila kuna kupa nafuu....
Nilichogundua wapingaji wengi na wachafuzi wengi wa Huyo....jamaa mnauchungu wa kukosa mlochokitaka na nafsi zenu hazija kubali kuwa mmekosa hadi 2025....
Mtakufa kwa msongo wa mawazo na kropokwa.

Mana ni msaada kwa huyo mama....hamasisha watu wamchangie....na sio kuchonga mdogo tu hapa
Humu siku kna watu wanajidai mambo safi wanakazi nzuri...magari...nyumba..mwdemu wazuri...
Waelimishe wamchangie huyo mama.
Achana na utanzania wa kimbea na hoja mfu za kupimga pinga na kusengenya.

Mwacheni aangalie hata Isidingo ni haki yake....
Yule ni Rais wako tu hata utambike huwezi kumfanya chochote....jiondoe roho ya wivu na mkwakwatu....mtima nyongo... Roho chafu....
Hulazimishwi kumkubali....ila acha afanye kwanza utamkosoa akimaliza
 
Hahaha tunamsaidia apeleke atakakopata msaada haraka
 
Back
Top Bottom