Beatrice Shelukindo ni mvunja utaratibu anapopanda bodaboda. Kapakiwa wawili, hakuvaa helmet!

Status
Not open for further replies.

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Wapanda pikipiki wamekuwa wakituhumiwa kila wakati kwamba hawavai kofia (helmet) ili kuwakinga na ajali.
Kubwa zaidi ni kitendo cha kupakiwa watu zaidi ya mmoja kwenye pikipiki moja.

Tulitegemea watunga sheria yaani wabunge ndiyo wawe wa kwanza kulikemea hili kila linapotokea.

Lakini tazama picha niliyoweka hapo chini. Unawaona Betrice Shelukindo na mtangazaji wa Radio/ITV yaani Wiliam Mngazija.

Wote wawili wamepakiwa kwenye pikipiki moja wakiendeshwa na dereva mmoja. Wote wawili hawajavaa helmet.

Unategemea nini kutoka kwa wabunge kama huyu inapozungumzwa hoja ya kupunguza maafa yanayotokana na kupakia ovyo kwa magari na pikipiki?

Unategemea nini kutoka kwa wabunge kama huyu inapozungumzwa hoja ya kujiweka salama safarini kama vile kufunga mkanda kwenye gari sawa na kuvaa kofia (helmet) kwenye pikipiki.

Siwasingizii, situngi maneno, bali ona mwenyewe picha hii, tena imepigwa na gazeti lao wenyewe IPP media analofanyia huyo mtangazaji.

View attachment IMG.pdf

SOURCE: NIPASHE
DATE: MAY 23, 2012
PAGE: 13
 
Itoe kwene pdf basi ila kwa mtu aliefika wilaya ya kilindi hilo nila kawaida maana niliondoka dar saa tatu nikafika kilindi sa nne usiku na usafiri toka kwediboma hadi kilindi mostly ni bodaboda
 
Itoe kwene pdf basi ila kwa mtu aliefika wilaya ya kilindi hilo nila kawaida maana niliondoka dar saa tatu nikafika kilindi sa nne usiku na usafiri toka kwediboma hadi kilindi mostly ni bodaboda

Naomba wachangiaji mnielewe tusipindishe maudhui. Sijazungumzia ugeni kuhusu shida ya usafiri. Uhitaji wa bodaboda hatuhitaji kufundishwa na watu wa Kilindi. Suburbs za Dar na miji yoote mikubwa hapa nchini bodaboda tunazijua.

Nimezungumzia usalama, kujaza kusiko na maana na kutojilinda kwa mikanda kwenye magari na huku kwenye pikipiki ni helmet.
 
cheap popularity inasumbua sana. anadhani ndo kuonyesha uzalendo na ukaribu kwa wana jimbo lake, kumbe anafundisha utupu kwa watu wake.
leo hii traffic police akiwakamata wengine ambao hawavai helmet si itaonekana ni uonevu wakati mbunge ameshahalalisha hilo!
kwanza MOI itamhusu sasa hivi.
 
Itoe kwene pdf basi ila kwa mtu aliefika wilaya ya kilindi hilo nila kawaida maana niliondoka dar saa tatu nikafika kilindi sa nne usiku na usafiri toka kwediboma hadi kilindi mostly ni bodaboda
Elli Mpwa kwa gari la mheshimiwa njia ile halingeshindwa kwenda kweli, njia ni mbaya lakini si wana l/cruisers ambazo 4wd ?
 
Last edited by a moderator:
9k=
 
MANI si anabana matumizi hahahaaaaaa ni bahili kweli, haya mie naelekea tena jangwani
Elli Mpwa kwa gari la mheshimiwa njia ile halingeshindwa kwenda kweli, njia ni mbaya lakini si wana l/cruisers ambazo 4wd ?
 
Last edited by a moderator:
Itoe kwene pdf basi ila kwa mtu aliefika wilaya ya kilindi hilo nila kawaida maana niliondoka dar saa tatu nikafika kilindi sa nne usiku na usafiri toka kwediboma hadi kilindi mostly ni bodaboda
.
Mkuu Elli nimemsaidia huyu Mkuu SubiriJibu kuitoa kwenye pdf ili kila mtu aweze kuiona
shelukindo.jpg
 
Do, huyo Beatrece Shelukindo mbona kakumbatiwa hivyo, ana mume kweli huyo? Sheria za kindoa haziruhusu mke wa mtu kukumbatiwa hivyo na mwanaume mwingie, na wasivyojali yawezekana hata waki**** hawatavaa pia, hii nayo kali.
 
huyu mama yangu si angekaa nyuma?lakini willy hana tabia mbaya labda kama shetani amemuingilia ndo anaweza kumtamani mama yangu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom