Beatrice: Nimepata Ujauzito na nina Amani! (USHUHUDA MZITO) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beatrice: Nimepata Ujauzito na nina Amani! (USHUHUDA MZITO)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Baba Mchungaji, Jul 28, 2011.

 1. B

  Baba Mchungaji Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bwana wetu Yesu asifiwe sana kwa miujiza anayoifanya. Ninawashukuru sana Strictly Gospel kwa maombi yenu hakika hakuna lisilo wezekana kwa Mungu!Nilituma maombi ilikuwa tarehe 11/5/ 2011 nikiwa katika kipindi kigumu sana lakini nimeona na macho yangu hakuna magumu kwa Mungu wetu mwenye huruma. Tatizo nilikuwa nayo ilikuwa ya kutopata mtoto na kutoelewana na mume wangu yaani alikuwa hataki kuniona. Ila mungu alitenda muujiza kama vile alivyomtendea Hanna mke wa elkana, amen! Wakati muliniandikia mkanifariji kwamba Mungu atayafuta machozi yangu kama vile alivyomufuta mke wa Elkana machozi na mkaniambia kwamba nitamkumbatia mwanangu hakika mulinitia moyo na hivi Mugu alisha jibu maombi hivi ni mama mjamzito na tena nina amani katika ndoa yangu. Jina la Baba libalikiwe na liheshimiwe na litukuzwe milele na milele, amina! Kwa hiyo mwezi wa tano niliendelea kumlilia Mungu huo mwezi wa tano usinipite kabla sijapata mtoto katika tumbo langu kulingana na magumu nilikuwa nayo wakati nilikuwa naomba sauti ya Mungu ikanijia ikaniambia nichukuwe biblia nisome 2wafalme 4;16-18 .na 2wafalme4;1-7, Jina la Bwana libalikiwe. Nilipo lala usiku nikalota mtoto iko anacheza tumboni nikawa nafuraha sana nikamtukuza Mungu wangu mwenye nguvu na hivi mimba iliingia huyo mwezi wa tano kwa sasa hivi ninaomba Mungu aendelee kulinda mtoto wangu na nijifunguwe salama. Jina la Bwana lihimidiwe. Ushuhuda wangu ni huo na mbarikiwe sana na mola wetu amina!Beatrice.Tarehe 11/5/2011 Beatrice Niyo akihitaji maombi aliandika kama ifuatavyo:
  “Mungu wetu asifiwe. Ndugu zangu naomba munisaidie kwa maombi sana nimeolewa lakini sijapata mtoto niko katika kipndi kigumu sana mume wangu anataka kunifukuza juu ya hiyo tatizo ananiambia kama mimi sifai kuwa mkeo wala sina faida kwake mambo mengi sana machozi yanidondoka usiku na mchana natatizo ingine mimi ni yatima sina ndugu wala marafiki wote walisha nikimbia akinifukuza sina nafasi yakwenda nahivi amenipa dakika moja yakuishi nae mda wowote anaweza nitupa inje juu ya hiyo tatizo sina masomo wala vyashala wala kazi ambavyo vinaweza kunisaidia jamani ninahangaika sana. Naomba munisaidiye kwa maombi hata kama inawezekana munisaidiye kwa kufunga hata sikumoja.siku zangu zakufunga ni siku ya tatu yaani wednesday naomba tusaidizane kwa maombi.hivi roho yangu iko sawa kidonda mchana ni giza kwangu na usiku ni huzuni nyingi kwangu. asante mwenyezi Mungu awajalie.”Ushuhuda mwingine wa Beatrice Niyo unapatikana katika link ifuatayo: http://strictlygospel.wordpress.com/2011/05/16/asante-yesu-kwa-kurejesha-amani/

  SOURCE:Beatrice: Nimepata Ujauzito na nina Amani! « Strictly Gospel
   
 2. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Asante kwa ushuhuda ! but science can explain it all ... no offense
   
 3. u

  ureni JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,273
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Bwana yesu asifiwe,hakuna ubishi mungu aliehai yupo,nakuambia mtoto huyo atakuja na baraka tele, nafikiri sasa hivi mmeo atakua ametulia.Na mbarikiwe.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,955
  Likes Received: 2,096
  Trophy Points: 280
  Muda mwingine ni kutokuwa na elimu ya uzazi na kuipuuzia na kutokuona umuhimu wa kuwaona wataalamu na kufuata ushauri wao. Huo ni mwongozo wa Mungu kwani lazima aliwafunulia ile elimu ya namna ya kufanya ile kazi kwa ufasaha ya kuleta mtoto. Tuwetunasoma vitabu na journals za mambo haya kwani walioandika wamepewa karama hizo na Mungu kupitia Roho Mtakatifu ili kufaidiana.

  Hivi haujakutana na pastor au kiongozi wa hao Strictly Gospel na kukueleza namna ya ku-handle tendo la ndoa ikiwemo na vyakula vya kula wewe na mumeo?
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  hongera beatrice,namtukuza mungu pamoja nawe. endelea kumuomba mungu akusaidie kuelewa neno lisemalo 'amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu' (ni yeremia nadhani). ww kuwa yatima, usimfanye mumeo kuwa ndo baba yako. Biblia inasema 'Mungu ni baba wa yatima..'uwe na moyo wa ushujaa.
  nb: mtoa mada,plz jumbe hizi umpelekee bibie
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,265
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na ww kabisa! na kufanyiwa maombi haimaanishi usitafute ushauri wa kitaalamu! 'watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa', mtu anaombewa na hosp haendi tena.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Isije ikawa anamtumia bible na kanisa lengo ikiwa kuna mwanaume anadanganywa mimba ni yake umbe sio Mtu kachukua sperm za mtu mwingine kenda majuuu kawekewa.
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hongera sana kwa kumwamini mungu na mafanikio umeyaona!!
   
 9. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu usiwaondolee furaha yao bhana DNA c imekatazwa hahahahaaaa......kumbe Baba mchungaji ni demu ooooh!!shhhh...sorry kama cjaelewa vyema .Cmama na Bwana nae atakutendea yaliyo makuu zaidi ya uyajuayo ...asema bwana.
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  khee basi kama ndo hivyo Beatrice=baba mchungaji.. ndo ulivyo maanisha
   
 11. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #11
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  .............. kwani Mungu aliwahi kufa ?!
   
 12. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #12
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145

  ........... hii ni karne ya 'hoja' na si 'miujiza' ............. ukiamini miujiza ni upo sawa na wale waliokataa kuwa dunia ni duara na wakamhukumu Galileo !
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ameeeeeeeeen na akili kum kichwa teh teh

  Mkuu unachanganya watu labda kama wewe huna dini wala imani. kama unayo dini na unayo imani ya mungu basi miujiza kwako na mafundisho yeyote yale sio kitu cha kushangaza.
   
 14. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #14
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  sifa na utukufu ni vyake Bwana...
   
 15. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #15
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  sheikh,huu sio uwanja wa mapambano ya kidini.
   
Loading...