Beacons hizi ni za nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beacons hizi ni za nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MJINI CHAI, Jan 25, 2011.

 1. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Wajameni naomba kuuliza kwa yeyote anaefahamu, kuna sehemu nyingi hapa Tanzania Hasa Vijijini utakuta alama za eitha Ukuta wa mita kama 3 kwenda juu na mita 4 upana au utakuta sehemu pamemiminwa zege la cement katikati ya pori, Huwa najiuliza sana hii ni nini? ukiwauliza wenyeji wanasema waliweka wakoloni (Wajerumani) nani anafahamu hivi vitu? na serikali yetu inasemaje juu ya hali hii?

  nawasilisha kwa wajuzi wa mambo
   
 2. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tupatie picha zake na maeneo zilipo utapata jibu.
   
 3. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  mkuu nasikitika kwa wakati ule sikuwa na wazo la kuwa naweza kuwauliza wadau humu jamvini, ingekuwa leo nipo sehemu hizo ningeweka hizo picha, ila alama hizo zinapatikana UTEMINI- Mwadui, MAKOTE -Newala, NAMAJANI- Masasi, MBESA, KIDODOMA- Tunduru na nadhani hata sehemu zingine zitakuwepo
   
 4. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ninaelewa unachokizungumza. Hizo ni alama za upimaji za kiwango cha juu (Yaani Zero-order horizontal control points, First-order horizontal control points na Second-order horizontal control points). Zipo zilizowekwa tangu enzi za mjerumani. Kwa sasa hivi serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi kupitia Idara ya upimaji na ramani, inatekeleza mradi unaogharimiwa na benki ya dunia wa kutengeneza muundo msingi wa upimaji tanzania unaoitwa, "National Mapping Framework". Katika kutekeleza hili, kunaanzishwa alama msingi za upimaji za kiwango cha juu (Higher -order Fundamental Control Network). Katika kutengeneza msingi wa utengenezaji ramani na upimaji nchini, katika mambo ya ramani, sasa Tanzania itakuwa na mfumo wake uliounganishwa katika mfumo wa kimataifa unaoitwa Inter-terrestrial Reference Frames (ITRF). Mfumo huu unatumia Continous Observing Reference Stations (CORS), kwa kupima mwendo kasi wa dunia (Velocity) ukitumia GPS, na pia unaunganishwa na vipimo vingine kama gravity measurements kwa kutumia "Gravimeters".

  Mwisho wa yote unapata kile kinaitwa "Coordinate Reference System" kwa ajili ya upimaji na utengenezaji ramani hapa Tanzania. Mfumo utakaokuwa umezingatia maumbile ya nchi nzima (Topography, Geoid and Geodesic) tofauti na hapo zamani ambapo hakukuwa na taarifa zinazojitosheleza hasa kwenye maeneo ya nyanda za juu na maeneo yenye Maziwa (Lakes) etc.

  Kwa hiyo, minara ya zege unayoiona huko vijijini imetapakaa Tanzania nzima, ni kwa ajili hiyo, na unaombwa uwaelimishe wananchi wasiiharibu maana ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Mapping is very important for the development of any nation. Kuna standards maalumu zinatumika wakati wa kujenga minara hii ya zege, ambapo huanzia chini urefu wa mita moja au mbili na kuwekwa zege hadi juu urefu wa mita moja hadi mbili.

  Hivyo usihangaike kubomoa kwa kudhani kwamba wajerumani wameficha dhahabu, alama nyingi hapo zamani zimeharibiwa na kusababisha hasara na usumbufu wakati wa upimaji. Alama hizi ni za muhimu sana kwa shughuli zozote za upimaji na utengenezaji ramani, na hata katika shughuli za ujenzi wa kihandisi (Construction Enginnering, Roads constructions, railways, dams, powerlines, water pipes laying out, topographic surveys, cadastral surveys, mining explorations, mining engineering etc.).

  Naamini umepata mwanga japo kidogo, kwa yale ambayo hukuelewa kwa sababu ya lugha ya kitaalamu niliyotumia ni kwa sababu ya kukosa mbadala wa kiswahili.
   
 5. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  good explanations
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ngereja hongera sana.
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Nikiwa mwanafunzi nilibahatika kuwa involved kwenye upimaji wa barabara - Manyoni - Tabora - Kigoma Road project, anachosema Ngereja ni ukweli mtupu - katika kazi yetu tulitegemea sana hizi points kutafuta % error kwenye measurements zetu, ingawa mara nyingi tulizipata zikiwa zimefukuliwa na zege kuviringishwa wakidhani kuna madini kaacha mjerumani.

  Kwa msaada wa Ramani na Picha za Juu (Arial Photograph) tuliweza kuzitafuta na kuzipata kwa shida sana, zingine unazikuta katikati ya vichaka nk. tulitumia hizi points kuunganisha reading zetu na zile originals, bila hizi huwezi kufanya kazi yoyote katika mambo ya upimaji na ramani aliyoyasema mtalaam hapo juu.
  .

  .
   
 8. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  waveja sanaa NGEREJA, thanx
   
 9. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Ngereja naona umejitosa mwenyewe kujibu, asante sana.

  Kwa vile wananchi hawakuelimishwa matokeo yake ni kwamba sehemu kubwa ya hizi alama zimeharibiwa na fortune seekers. Kwa kuwa mawasiliano kwa sasa ni mazuri na ni rahisi zaidi kuwafikia wananchi kuliko ilivyokuwa enzi ya Mjerumani basi naona ipo haja kwa serikali yetu kwa sasa kuwaelimisha wananchi wasiendeleze uharibifu.
   
 10. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana kwa kujibu kitaalam zaidi!!!
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Jf kiboko, kitu kimoja tu ndicho jf inaogopa kuweka nadhani ni wakati muafaka sasa kukiweka ili tupate ufafanuzi, nacho ni *UCHAWI*, hii kitu sijaiona humu janvini, inamaana hakuna mwenye uelewa wowote juu ya hili?.
   
 12. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kusimuliwa kuwa enzi za wajerumani walitumia hata vichuguu kama ishara za ki-ramani, mfano wake ni safu za vichuguu zinavyoonekana pembeni ya barabara za mikurutini(ndani ya wilaya ya ilala maeneo ya kivule) au barabara ya mbezi -msumi(kinondoni). Katika baadhi ya maeneo barabara hizi ambazo mara nyingine hutwa barabara za wajerumani huenda sambamba na vichuguu kwenye pande zake mbili. Je, hii lina ukweli?.
   
 13. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35


  Thanks for this useful post.
   
 14. WAKUNJOMBE

  WAKUNJOMBE JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mkuu hongera sana maana kweli umetufumbua wengi...........
   
 15. K

  Kikambala Senior Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni muhimu sana kuhabarisha watu kama hivi,nilisikia mara nyingi kuwa wajerumani walikuwa wameweka hazina katika mahandakii kama hayo kisha wachimbaji waliotekeleza kazi hiyo waliuwawa ili kuficha siri ya hazina hiyo,kumbe sivyo kabisa hongera sana
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Aliyosema mkuu Ngereja ndio maelezo sahihi kabisa ya hizo Beacon zinazoonekana sehemu mbalimbali sikisadikishwa na uhifadhi wa hazina (Madini, Rupia nk),
  na ni kweli kuwa hizo beacon kwa kiasi fulani zimepitwa na wakati, kwa maana zina kuwa na tofauti kidogo kulingana na technologia iliyopo sasa (GPS) ambayo inalink straight na satelites
  Tukae tukijua kuwa hizo beacon ziliwekwa Tanzania na Mjerumani bila kutumia GPS, by that times walitumia sana astronomy na astrologs na hizo beacon zina reference ya kutoka ujerumani, yaani walikuwa wanakuja na coordinates kutoka Ujerumani kwa kufuata Compass, na hayo Mambo ya Nyota. japokuwa zinatofauti ndogo, lakini bado zina mchango mkubwa sana katka hizo sector alizozielezea Ngereja
   
 17. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  umeeleza vizuri Mkuu Ngeleja

  elimu ya kuhifadhi alama hizi huwa haitolewi na matokeo yake kunakuwa na uharibifu mkubwa sana wa alama hizi.
  katika upimaji tumekuwa tukipata shida sana hasa tunapotafuta alama hizi na kukuta zimebomolewa. Juzijuzi hapa tulikuwa tunafanya kazi ya upimaji eneo la ngorongoro, lakini Trig points zote maeneo ya Karatu zimevunjwa na hazifai kabisa.

  ni vizuri Wizara ya Ardhi wafanye jitihada za kuelimisha juu ya hili
   
 18. n

  ngoko JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ngereja umesomeka.
   
Loading...