Be careful: Bidhaa wanazotuuzia wawekezaji!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Be careful: Bidhaa wanazotuuzia wawekezaji!!!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ngoshwe, Mar 21, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  IMG00439-20110321-1158.jpg IMG00434-20110321-1153.jpg IMG00431-20110321-1152.jpg  Kuna wakati niliwahi kuwaleta hapa taarifa kuhusu ubovu wa baadhi ya bidhaa zinazouzwa katika maduka makubwa ya bidhaa (supermarkets) zinazomilikiwa na "wakoloni" nchini hasa zile za vyakula.

  Jana jioni (tarehe 20.03.2011) nilipitia pale Shoprite Mlimani City, moja ya mambo niliyoweza kushuhudia katika harakati zangu ni kukuta baadhi ya bidhaa za matunda zikiwemo "appels" picha zikiwa zimewekwa kwenye makabati ya kuuzia bidhaa (shelves) ili hali muda wake wa kuuzwa umekwisha (expired).

  Hayo ma "appels" yalipaswa kuwa yameuzwa kabla ya tarehe 12.03.2011 lakini cha kusikitisha, bado yamefungwa na vifungashio vyake kuonyesha bei na lini yalipaswa kuuzwa, inaonekana manajimenti ya duka hilo kubwa hapa nchini kama halina nia ya kujitegenezea faida kwa stahili ya kuuza bidhaa zisizofaa basi haipo makini katika kuhakiki bidhaa dukani.

  Katika jitihada za kujaribu kuwafahamisha wadau yale ambayo "wawekezaji" wanatufanyia hapa nchini, niliamua kununua furushi moja kwa Tshs. 6,500 na baada ya kufungua, nakutana na moja ya tunda katika furushi hilo likiwa tayari limeoza (kama mnavyoweza kuona pichani).

  Bidhaa hizi na nyingine ambazo hazina muda wa kutumika katika vifungashio bado mpaka tarehe ya leo (21.03.2011) zipo kwenye makabati ya kuuzia vitu pale Shoprite (kama mtu akiweza kupita hapo achungulie)! Kama upo makini, ukienda kununua, ukishtukia "expiry date" wanachokifanya ni kukubadilishia tu (haijulikani hata yale wanayokubalishia yaliingia lini nchini kutoka huko Afrika ya Kusini yanakozalishwa).

  Kwa utaratibu huu, pengine tunaweza kuamini, vyombo vyetu vyenye dhamana na afya ya walaji kama TFDA havina uwezo wowote wa kupita kwenye maduka ya wawekezaji wakubwa na kuachukulia hatua stahili.

  Cha msingi ni watanzania wenyewe tuwe makini na haya mambo ya bidhaa toka nje hasa za "supermakerts". zinatumaliza kimya kimya.

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa kuna bidhaa nyingi mno kwenye hizi supermarkets ambazo zimepitwa na wakati lakini wahusika hawalioni hilo wao pesa kwanza afya baadae.
   
 3. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,160
  Trophy Points: 280
  hiyo elfu 6 unapata kilo ngapi za ma-apple original toka tanga hapo k-koo?pendeni bidhaa za nyumbani jamani duh.
   
 4. M

  Mawazo1109 Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante kwa taarifa na tahadhari kwa walaji wa apples kutoka South Africa!!! Ulichokifanya ni kizuri kama ulifahamisha uongozi wa Shoprite kuhusu hali hiyo, ili wawe makini zaidi.

  Lakini mi nauliza ni faida gani tunapata tunapobugia hayo matunda kutoka South Africa, wakati matunda ya kitanzania yamezagaa masokoni. Hata kama muda wa kuuza ungekuwa haujaisha, tuna uhakika gani na usalama wa chemicals zinazotumika ku preserve hayo matunda tangu muda yanapotoka mashambani hadi yafike kwenye shelves za Shoprite Dar es Salaam? In the long run tunajua madhara ya hizo chemicals? Na bado tujue kwamba hayo matunda yanayozalishwa kwa ajiri ya kuuzwa nje ya South Africa yanazalishwa katika mashamba maalum na wanatumia madawa mengi tu, kwa sababu wanajua raia wao hawatakula. Tuwe makini jamani; GMOs zina madhara makubwa sana in the long run, acheni kula those apples from South Africa.

  Mi niko huku Johannesburg, juzi juzi nilikuwa na rafiki yangu mmoja, black South African, akanisimulia kwama yeye hata nyama inayozalishwa huku hali, maana hawa ng'ombe wanalishwa madawa tangu wanazaliwa had wakati wa kuchinjwa. Hapo usalama uko wapi?
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  tehe mie sinunui kabsaaa matunda ya supa market mbona yetu mazuri yapo kibao tuuu
   
 6. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Vitu vingi supamaketi huko vimeoza,
  Bora tuendelee kwenda kariakoo
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hivi africa tumekosa nini mpaka tule apples? We should stick with our tropical fruits. Badala yake tropical fruits tunazipeleka nje halafu tuna import useless apples? Matunda karikakoo.
   
 8. I

  Igembe Nsabo Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante sana kaka kwa taarifa hiyo, Mie nilikuwa miongoni mwa walaji wa hayo ma Apple na Mtoto wangu nilikuwa namspoil kweli na hayo Ma Apple! tunawaua kweli watoto wetu na familia zetu kwa vitu hivi vya western country na kuona vitu vyetu vya asili kuwa ni vya KISHENZI. Ni kweli let we change and be proud on our things!
   
 9. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asante kwa kutujuza ila langu ni kuwa je TFDA au TBS wanafanya kazi gani? Au ndio kitu kinatembezwa kwa wakubwa halafu midomo inafungwa? Hizi mamlaka zetu wako tayari waende kwa Babu, Loli kuulizi ubora wa dawa halafu wakaacha ufisadi wa wazi unaofanywa na wenye Supermarkets za hapa nchini.
   
 10. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ama Buguruni, Mabibo hata M/Nyamala
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mkuu, kama unafuatilia kwa karibu, unaweza kubaini kuwa TFDA wamejikita zaidi kuwavurugia biashara wafanyabiashara wadogo wadogo wa dawa baridi (huko ndiko wanakojitangaza zaidi). Japo kwa mujibu wa Sheria inayoanzisha Mamlaka hiyo wanapaswa kuhusika pia katika kufuatilia ubora wa vyakula, hawana nguvu za kufikia wafanyabiashara wakubwa. Kwa upande mwingine, hata ile Tume ya Ushindani wa Bei ambayo katika kipindi fulani ilijijengea umaarufu wa kuharibu bidhaa feki toka chini, sasa imekuwa na kigugumizi katika kulinga haki za walaji na ndio maana unakuwa bidhaa nyingi kama si feki basi zinauzwa kwa bei mara tatu na ile halisi ilimradi tu faida itengenezwe hata kwa kumuua mlaji (consumer) kiuchumi au kiroho.


  Tunahitaji nguvu ya pamoja kufuatilia na kubainisha mambo kama haya katika jamii yetu. Zipo pia hata Bucha ambazo zinauza nyama zilizolala, zipo baa na hoteli zinauza vyakula vilivyopumzika kwnye majokofu na kuchacha lakini hakuna anayefuatilia. Hakika sasa magonjwa yamekuwa mengi na gharama za kuishi zimakuwa juu kutokana na uzembe wa baadhi ya mamlaka katika nchi hii. Kwa sasa hata kwenda kupata matibabu ya kikombe ndani ya nchi hii hihi (kwa wale waumini wa hilo) inawagharimu maumivu makubwa sana kuliko ukitokea nchi jirani kama Kenya. Kikombe 500 lakini kukifikia inaweza kukugharimu mara mia ya 500.

  Tuzikumbushe mamlaka husika huu uozo unalipeleka Taifa letu pabaya!.
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Haiwezekani wakashtakiwa?
   
 13. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Si ajabu ukipita kesho watakuwa wameziondoa! Jamani tule vyetu! Ni vizuri mno!
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ninyi Kilanga chenu cha kula hizo apple hata hamjui zimelimwa wapi cha nini??

  Kwa nini usile embe au ndizi??

  Wenzenu huku majuu tunalanguliwa embe moja $2.00 wakati kwa bei hiyo unapata mfuko wa Apple kibao!

  Ukoloni wa kutawaliwa na mshirika makubwa ya kimataifa kwa kutumia kila kitu katka maisha ya watu umetukamata hata hatujui wapi tuanze kujinasua.

  Eti hata maji watu wanakunywa maji ya kutoka nje??

  Laiti wangejua maji hayo yametekwa wapi??

  Buy Local.

  Kula Mafenesi,Mabungo, Ukwaju, ndizi, mbilimbi,mabuyu,embe bolibo,chungwa lna papai a muheza na tunda aina ya Bibo uongeze afya yako.
  Achana na unajisi wa kula takataka kutoka ughaibuni.
   
Loading...