BBC: Zitto Kabwe amevuliwa vyeo vyote CHADEMA kwasababu ya kugombea uenyekiti wa chama hicho

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
BBC kituo kikubwa cha habari Duniani, Jana jioni na Leo asubuhi wameendelea kusisitiza kuwa Mh. Zitto Kabwe amevuliwa nyadhifa zote za uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu ya Kutangaza kugombea Uenyekiti.

BBC wanasema, Zitto, Mwigamba na Kitila wamevuliwa nyadhifa zao na huku wakipewa siku 14 kama hatima ya uanachama wao ndani ya CHADEMA.

BBC Wanasema "Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma ameingia kwenye mzozo na kashikashi ya kisiasa ndani ya CHADEMA siku za karibuni kutokana na hatua yake ya kutangaza kugombea nafasi ya Uenyekiti ndani ya chama hicho".

Nawasilisha.

Asante BBC kwa kusema ukweli, Haya ya WARAKA wanaoandaa akina BEN wala hayana tija. Huu ndio Ukweli. Vyombo vya habari vya Tanzania Viige Mfano huu wa kusema ukweli.
 
Siku moja nilikua nipo na Hamza Mwamoyo Washington,Asha Rose Migiro akiwa bado UN akapiga simu akilalamika kwenye kipindi cha VOA kuna mchangiaji katoa maoni ya kumpinga Kikwete,akawa anahoji kwa nini wameruhusu baadala ya kurusha maoni ya kumjenga??!! Hata Hamza Mwamoyo ilimkera hoja hiyo kwani maoni yalikua ni ya msikizaji n'a sio mwandishi au VOA yenyewe,CCM N'A PROPPAGANDA NI NG'OMBE N'A KUPE!!!

Sishangazwi na ukibaraka wa watanzania dhidi ya watawala, n'a uzuri hii kampuni ya TUNTETEMEKE inajulikana wabia n'a lengo
 
mengi tutayasikia hili sakata nafkiri tungemsubiri mwenyewe atoe tamko lake kuhusu hii atua iliyochukuliwa na kamati kuu ya chama
 
Mimi nikitaka kupata za uhakika kuhusu sakata hili nitakuwa nasikiliza BBC pekee badala ya kusoma magazeti kama Tanzania Daima. Hawa CHADEMA wa ajabu sana, kwa maana hiyo yoyote atakayegombea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA taifa anafukuzwa?
 
Kwa wewe inaelekea BBC wakitangaza kwa mfano Dr. Mvungi hajafariki, utakubaliana nao na utaomba vyombo vyote vya habari vya Tanzania viige hilo shirika kubwa la habari duniani kwani huo ndio utakuwa ukweli !

Usiwe mpumba-vu wewe.......watu kama nyie ndio mkiwa kwenye uongozi ndio mnauza nchi.....sababu chochote watakachowaambia wazungu mnaona ni sahihi.
 
Hiyo BBC unasikiliza wewe mwenyewe?mbona hakuna tangazo kama hilo jana jioni wala leo asubuhi. Ambae akusiliza arejee matangazo hayo katika bbc swahili/ habari kwa ufupi. Isitoshe leo BBC ilikuwa na makala ya bayo gesi. Ama kweli CCM wameumia !!!
 
Hilo nalo unawabishia BBC? kweli kupenda kubaya, wewe utakuwa wale wale wanaotumiwa na MBOWE.
 
lakini chakujiuliza ni kwamba, kugombea uwenyekiti ndani ya chama ni dhambi? kama sidhambi yote haya ya nini? jengeni chama chadema acheni majungu kama yale ya NCCR ambayo mwishoye tuliyaona.

mkuu kitu cha kizembe wanachofanya mbowe na slaa ni kufanya chadema kuwa mali yao binafsi wengine wasiwe na chakusema badala yake wawe wasikilizaji tu.
 
mengi tutayasikia hili sakata nafkiri tungemsubiri mwenyewe atoe tamko lake kuhusu hii atua iliyochukuliwa na kamati kuu ya chama

ZITTO akitoa Tamko sasa hivi nchi inaweza kutikisika, acha asubiri subiri kwanza. jamaa ni zaidi ya akina MBOWE 20 na SLAA 10.
 
Je, bbc hawajasema wanaompa fedha za kumwezesha kugombea uenyekiti anapewa na ccm?

Kwanini ccm wanaichagulia chadema mwenyekiti?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Hiyo ni kazi ya vyombo vya PROPAGANDA vya CHADEMA kama Tanzania Daima na MAWIO huwezi kusikia shirika kama BBC linasema uzushi na ujinga kama huo
 
Kipimo cha akili ni pesa na kipimo cha ubaya ni ndoto Zitto usiogope wakifunga wakifunga mlango huu Mungu atafungua mingine 1000 kazi kwao kuifunga!
 
Hiyo BBC unasikiliza wewe mwenyewe?mbona hakuna tangazo kama hilo jana jioni wala leo asubuhi. Ambae akusiliza arejee matangazo hayo katika bbc swahili/ habari kwa ufupi. Isitoshe leo BBC ilikuwa na makala ya bayo gesi. Ama kweli CCM wameumia !!!

wewe unasikiliza BIG BROTHER YA CHADEMA(BBC) au shirika la habari la uingereza? ingia hata kwenye tovuti yao ya bbcswahili.com kila kitu kipo, wewe wa wapi?
 
Back
Top Bottom