BBC yamuhoji Daktari Muhimbili, asema watanzania wengi wanakufa kwa Corona. Awataka kuwa makini



Watu wanakwama zaidi ya wiki mbili mpakani si quarantine hiyo mbona wako poa, hawa majirani zetu Kenya na Rwanda nao ni muda wa kuacha kutuletea upuuzi maana ata sayansi ya COVID inasema ndani ya muda mtu awezi kuwa na maambukizi na ata angekuwa nayo awezi sambaza.

Hili swala la mpakani sasa serikali inabidi itoe elimu kwa majirani zetu inawezekana wana ufahamu tofauti na dunia kuhusu Corona.
 
Kiukweli na Mimi nimemzika Mama yangu mdogo siku chache zilizopita.. Hadi anafariki dalili zilikuwa kama za Corona tu aliumwa siku 4 tu baadae akadae hawezi kupumua alafu anasikia kama kuna kitu kinamkaba.. Akawekwa kwe machine ya kupumua siku moja baadae akafariki.

Cha ajabu ni kwamba hadi amefafiki hospitali hawakutoa chanzo cha kifo wakachukua kipimo cha Corona lakini mpaka sasa mwezi umepita hatujapewa majibu..

Naweza kusema Mimi pia ni Muhanga wa Corona.. Mama yetu tulimpenda sana na hamna aliyewaza kama angefariki ghafla hivi maana hakuwahi kuumwa chochote kwa muda mrefu!

Pole sana kwa kuondokewa na Mama, mlipewa maiti mzike wenyewe?? Kama mlizika wenyewe basi huenda haikua Corona
 


BBC imeonyesha report kwenye tv kutoka tanzania ikionyesha serikali ikizika waliokufa kwa corona usiku wa manane.

Pia wamemuhoji Daktari wa Muhimbili aliyefunguka kuwa watu wengi wanakufa wakiwemo marafiki zake kwa Corona, amesema ni aibu na inatisha kwamba serikali inasema ugonjwa umeisha.

Pia BBC wameonyesha clip ya mchekeshaji Idriss Sultani akicheka picha ya Rais na kueleza kwamba mchekeshaji huyo aliwekwa jela kwa kosa la ajabu la kumcheka Rais.

Pia BBC wamemuhoji Zitto Kabwe aliyesema kwamba Serikali inaficha ugonjwa wa corona kwa kutaka watanzania wote wapate corona watakaokufa wafe na watakaopona wabaki na kinga.
a

Wameamua kuwaacha watu wafe.

Eeh mola wetu hebu na usiwalipe wao kama wanavyowatendea wenzao.

Si nia yetu kuwaombea wao mabaya kwani ulitufundisha kuwa: "adui yako mpende!"
 
Hofu yangu uyo dactari asije kutekwa na kutoweka

Tuna Rais mkaidi haijapata kutokea yaani sijuwi wanaomshangilia kichwani zimwo kweli? au madishi yameshayumba.

Najitahidi kumsaport ila nafsi inanisuta sana sana nashindwa.

Alichoamua huyu Rais jeuri, mkaidi na Dikteta ni ACHA WATU WAPATE CORONA WAJENGE KINGA....WATAKAOKUFA NA WAFE NA WATAKAO PONA WAPONE!
Hiyo ndiyo akili ya Rais anayesifiwa na Mafisi wote wa Lumumba na Wana mpango wa kumfanya Sultan au Mfalme wa maisha.....🇹🇿😭😭!!!
 
Back
Top Bottom