Wasiwasi Watanda Ulaya, Marekani Kutokana na Kushuka Kwa Ubora wa Mbegu za Kiume

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,857
49,553
5D42217C-64ED-4D44-B946-85AA62835764.jpeg


Wataalamu wametahadharisha kwamba ubora wa mbegu za kiume miongoni mwa wanadamu umekuwa ushuka pakubwa, na kuathiri uzazi.
Hili linasababishwa sana na kula vyakula vya kisasa vyenye mafuta mengi na wanga pamoja na kutofanya mazoezi ya kutosha.

Athari zimejitokeza kwenye kiasi cha mbegu za uzazi anazotoa mwanamume na pia ubora wa mbegu zinazotolewa na uwezo wake kuogelea katika majimaji ya ukeni.

Wahudumu katika kliniki za masuala ya uzazi wanasema kiwango cha mbegu za uzazi zilizo bora kimekuwa kikishuka kwa takriban asilimia 2 kila mwaka.

Kushuka huku kwa kiwango cha mbegu za kiume kumeshuhudiwa miongoni mwa wanaofika kutaka kutoa mbegu za kutumiwa kuwatungisha mimba wanawake na wale wanaofika wakitaka wasaidiwe kuongeza kiwango cha ubora wa mbegu za uzazi ndipo waweze kutungisha mimba.

Matokeo ya utafiti huo yamewasilishwa katika kongamano la kila mwaka la Chama cha Matibabu ya Uzazi Marekani ambalo linaendelea mjini Denver, Colorado.

Kudhoofika pakubwa

Utafiti umeonyesha kwamba mbegu za kiume zimekuwa zikidhoofika pakubwa kiasi kwamba zinashindwa kuogelea kwenye majimaji ya mwanamke zikielekea kufikia yai kutungisha mimba.

Idadi ya wanaume wanaoomba usaidizi kutungisha mimba imeongezeka mara saba katika mataifa ya magharibi katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Wataalamu wameeleza hali hiyo kuwa ya kuogofya.

Wataalamu wanaamini unene pamoja na mtindo wa maisha siku hizi wa kuketi vipindi virefu bila kufanya mazoezi kunachangia, pamoja na mabadiliko kwenye lishe na kemikali nyingi ambazo zipo kwenye mazingira.

Utafiti huo ulishirikisha wanaume 124,000 waliotembelea kliniki za uzazi Ulaya na Marekani, ambapo ilibainika kwamba ubora wa mbegu za uzazi unashuka kwa 2% kila mwaka.

Waliangazia kipindi cha kati ya 2002 na 2017.
Wanaume waliotafuta usaidizi kutungisha mimba waliongezeka kutoka 8,000 hadi 60,000 katika kipindi hicho.

Kiwango cha wanawake walioomba huduma ya kutumia teknolojia kutungisha yai mbegu (IVF) kutokana na kasoro kwenye waume zao pia kiliongezeka na kinatarajiwa kuongezeka hata zaidi.

Utafiti mwingine ulioangazia watu 2,600 waliotaka kutumiwa kutoa mbegu za kiumbe za kutumiwa na wengine, ambao kwa kawaida huwa na kiwango cha juu kidogo kuliko kawaida cha uzazi, pia wanaathirika hivyo.

Hii inaashiria kwamba kushuka huku kwa ubora wa mbegu za kiume hakubagui.

Wanasayansi hao mjini Valencia, Uhispania na New Jersey, Marekani walifanya utafiti wa kwanza mkubwa kabisa wa kubaini uogeleaji wa mbegu za kiume kwenye majimaji ya mwanamke.

Ingawa wengi wa wanaume bado wanaweza kutungisha mimba kwa viwango vya sasa, wanasayansi wanaonya kwamba huenda binadamu wakakabiliwa na hatari ya kuangamia mtindo wa sasa ukiendelea.

Mwandishi mwenza wa ripoti ya matokeo hayo ya utafiti James Hotaling amesema: "Kuna uwezekano wa wanaume wengi zaidi na zaidi kuwa gumba na hilo linazua wasiwasi.

"Unahitaji watu wawili ndipo mtoto azaliwe."

Utafiti huo wa sasa umetolewa huku bado kukiwa na mjadala kuhusu utafiti mwingine ambao matokeo yake yalitolewa mwaka jana na kuonyesha kiwango cha mbegu za kiume kimepungua kwa asilimia 59 katika nchi za magharibi kati ya 1973 na 2011.

Dawa za kuua wadudu, kemikali zinazoingilia mfumo wa homoni mwilini, mfadhaiko na unene vinatazamwa kama mambo yanayochangia hili.

Kuna pia unywaji pombe kupindukia, kafeini na ulaji wa nyama iliyopitishiwa viwandani.

Kemikali zinazoathiri kiwango cha uzazi ni pamoja na zile zinazotumiwa kuzifanya plastiki kuweza kunyumbuka na kemikali zinazotumiwa kwenye mbao kuzizuia kushika moto haraka.

Kemikali hizi zinaweza kuingia kwenye mfumo wa chakula kupitia mimea na wanyama.

Wataalamu pia wanalaumu kuongezeka kwa visa vya saratani ya korodani, visa vingi vya wavulana kuzaliwa bila korodani zote mbili au bila korodani moja, pamoja na kubadilika kwa viwango vya homoni aina ya testosterone.

Kiwango cha mbegu za kiume

Kuna mambo mawili ambayo huwa muhimu katika kupima uwezo wa uzazi wa mwanamume.

Kuna kiasi cha mbegu za kiume zinazotolewa na mwanamume (sperm count) na kiasi cha mbegu zilizo na uwezo wa kuogelea na kufikia yai, kwa Kiingereza 'motile sperm count'.

Kwa kadiri mwanamume hutoa mbegu 33 milioni hadi 46 milioni katika kila mililita ya shahawa. Iwapo kiwango chako ni chini ya 15 milioni, basi huwa una tatizo.

Miongoni mwa mbegu hizo, unaangalia pia zile zilizo na uwezo wa kuogelea na muundo wake. Kwa kawaida, asilimia 40 ya mbegu hizo zinafaa kuwa na uwezo wa kuogelea, ambapo kwa mwanamume wa kawaida itakuwa ni mbegu 20 milioni. Ukiwa na chini ya mbegu 5 milioni zinazoweza kuogelea, basi una tatizo.

Chanzo: Wasiwasi kuhusu mbegu za kiume Ulaya na Marekani - BBC News Swahili
 
Yaani sisi waafrika tungekuwa na subira mbona siku moja tungerudisha vyote walivyoiba kwetu hao wakoloni,
Maana kuna nchi sasa hivi uzazi wa mpango umeshawaathiri , wazee ni wengi kuliko vijana hadi wanatoa vibali vya kufanya kazi huko kirahisi rahisi tu , tungeenda huko waafrika tukawatunga mimba , uzao wetu ukajaa huko , wakapatikana wakina obama wa ukweli wengi baadae , sio obama kibaraka wa marekani,
It sounds fuuny lakini mbinu hii ndio marekani waliitumia kumpata Gorbachev, it works,
 
Account ya twitter ya bbc swahili ni kama inaendeshwa na wahuni.

Inapost kitu ukiangalia kwenye mainstream news zao kwa kingereza hamna kitu.

Mfano hii ningetegemea kama ni big news iwe front kule bbcnews lakini wapi. Wao bbcswahili wapo kama waandishi wa udaku tu hamna kitu hapo
 
Wengi mnachangia kwa hisia hapo limezungumziwa suala la ubora wa mbegu za kiume,kama umefika ulaya au usa asilimia kubwa vyakula vyao ktk migahawa/hotel ni Junk' food! kila siku unakula junk food unategemea utakuwa na afya timamu? Tatizo sio ushoga tatizo ni vyakula.
Asilimia kubwa ya gay hawawezi kudindisha atatoa mbegu gani?
 
Wao si wanaona ndoa za jinsia moja na ushoga ndiyo maendeleo ngoja kizazi chao.kipotee kabisa kwenye uso wa dunia kama Mungu alivyokifuta kizazi cha mabazazi wa Sodoma na Gomorrah. Laana hii haiwezi kuwaacha salama hata kidogo
 
Back
Top Bottom