BestOfMyKind
JF-Expert Member
- Apr 26, 2012
- 1,335
- 1,386
Kwa siku kadha sasa, taarifa zimekuwa zikienea kwenye mitandao ya kijamii kwamba Rais wa Tanzania John Magufuli amewataka wanaume nchini Tanzania kuoa zaidi ya mke mmoja.
Taarifa hizo zinadai kwamba kiongozi huyo amependekeza hilo kama suluhu ya kupunguza ukahaba miongoni mwa wanawake wa Tanzania.
Je, kuna ukweli wowote kuhusu madai hayo? Taarifa hizi zilianza wapi na zinadai nini?
Taarifa ya sasa ambayo imekuwa ikisambazwa sana imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili na kuchapishwa katika mtandao wa nipasheonline.com, mtandao ambao bila kuwa makini huenda ukadhani una uhusiano na gazeti la Nipashe la nchini Tanzania ambalo huchapishwa na ippmedia. Kampuni hiyo huchapisha pia gazeti la Jumapili kwa jina Nipashe Jumapili. Hata hivyo ippmedia haina uhusiano wowote na mtandao huo. Taarifa zake za Kiswahili hupakiwa katika tovuti yeye jina ippmedia.com/sw, mtandao ambao umekuwepo tangu mwaka 1998.
Hii Nipashe basi ni ya wapi?
Uchunguzi wetu umebaini kwamba tovuti hii imesajiliwa na mhudumu wa mtandao aliyepo jijini Nairobi. Mtandao huo ulisajiliwa mara ya kwanza Agosti mwaka 2017. Hivyo basi ni mtandao ambao umekuwepo kwa mwaka mmoja hivi.
CHANZO: BBC
Namimi nasema; Umbea, husuda na uongo ndio sifa za wakenya. Oooh Olduvai Gorge ipo Kenya, oooh Kilimanjaro ipo Kenya. Acheni upuuzi