BBC waendeleza ubeberu: Eti Tanzania nchi ya 23 kijeshi Afrika, Uganda ya 14 na Kenya ya 12

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
BBC wa ajabu Sana hawa.

Eti Tanzania ni nchi ya 23 kwa nguvu za kijeshi. Eti Congo DRC ni ya 10. Uganda 14 na Kenya 12.

1. Egypt, 2. Algeria 3. Nigeria 4 south Africa 5. Ethiopia 6. Angola 7. Sudan 8. Morocco 9.Libya na 10 ni Congo DRC.

Maajabu hayaishi duniani. Mbona Libya, Ethiopia, Congo DRC na Nigeria vita kibao na uimara huo wa Majeshi yao?

Source: BBC Swahili news.
 
Nakubaliana nao kwa 100% hapa kazi yao kupiga raia kwa sababu za kipumbavu utakuta mwanajeshi amedundwa na raia kwenye bar au klabu ya pombe za kienyeji kwa kugombea mwanamke anakimbilia kambini halafu wanatoka zaidi ya 10 kwenda kumchangia raia sasa si upuuzi huo.
 
Believe me, tunajifariji tunapojisifiaga kuwa jeshi letu ni miongoni mwa majeshi yenye nguvu Afrika. Jeshi letu lacks professionalism, liko kisiasa sana. Basi tu watu wengi hawajui kuhusu madudu ya hili jeshi.

Nyerere alishawahi sema kuwa jeshi letu ni the most politicized institution in Tanzania, tena walilifanya liwe hivyo kwa makusudi kabisa. Mpaka leo liko hivyo, halijabadilika.

We have a weak army. Anaebisha basi haijui vizuri JWTZ.
 
Sema hoja uliyotumia kuwapinga ndio imenishangaza na mimi

Kwamba nchi ikiwa haipigani vita inaonekana ina jeshi imara sio? sidhani kama ni kweli

Uimara wa jeshi wanazingitia ubora wa mafunzo ya wanajeshi, vifaa(dhana) za kivita za nchi husika, budget kwenye jeshi la nchi husika n.k
 
Hawa DRC ambao SADC yote imebidi ikawasaidie kudhibiti vikundi vya uasi ndo wanasemwa wana jeshi imara haya ni maajabu.

Ila jeshi letu kuwa nafasi hiyo sipingi.
 
Hawa DRC ambao SADC yote imebidi ikawasaidie kudhibiti vikundi vya uasi ndo wanasemwa wana jeshi imara haya ni maajabu.

Ila jeshi letu kuwa nafasi hiyo sipingi.
Wanasema kambi za jeshi za Congo DRC zina wanajeshi 134000. Wanaangalia pia idadi, vifaa, bajeti nk
 
Niliachana na elimu, tafiti za kizungu tangu nijue kusoma na kuandika.
Inabidi DRC waje kutrain jeshi letu.
Wingi wa waaasi wanaojiunga na jeshi kisa maridhiano, ndiyo kumeipaisha Congo DRC. Hata hivyo wanasema hawana vifaa na wanaonewa na mataifa jirani. Double standard tupu!!! Sasa na 10 ya wapi?
 
Back
Top Bottom