BBC Vs BAC....Mambo ya kuangialia jinsia kwenye mavazi yanawezekana kweli??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BBC Vs BAC....Mambo ya kuangialia jinsia kwenye mavazi yanawezekana kweli???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dark City, Mar 20, 2012.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Leo nimekutana na mzee mwenzangu ambaye naye ni BBC (Born before computers), na katika mambo ambayo tumejadili, ni juu ya malezi kwenye familia. Yeye anasema kuwa hawa vijana wa enzi hizi (BAC, born after computers) wana matatizo ya kutojitambua linapokuja suala la mavazi. Aliongea kwa jaziba na kudai kuwa watoto wa kike wamevamia mavazi yetu (ya kiume) na wakome kabisa!!

  Nimejaribu kueleza mtazamo wangu kwamba suala la muhimu ni mtu kujitambua na kufanya tathmini ya mahali anapoenda kabla ya kuamua jinsi ya kuvaa.

  Huyo BBC mwenzangu kaja juu kabisa....anadai kwamba katika misingi yote (dini n.k) vijana wavae kadri ya maelekezo ya Mungu...Ameahidi kuniletea vifungu kutoka kwenye vitabu vitakatifu vinavyopiga marufuku watu kuvaa nguo za jinsia nyingine.

  Tatizo langu ni kwamba....kweli inawezekana kurudi kwenzi hizo za BBC katika mambo ya mavazi?

  Naomba michango yenu kabla ya kikao chetu kijacho!!

  Babu DC!!
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Naamini BAC ni retro ya BBC, with few exceptions. Hamna mapya mengi, design bado kubadilika labda orientation, presentation na nyingine zinazofanana na hizo.

  Pia usisahau kuhusu feminism, na ukweli kuwa the men race is reaching extinction status!
   
 3. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hizo exceptions ni zipi?

  Na je tunaweza kweli kusema kwamba kuna mavazi ya wanaume (suruali, shati au t-shirts) na ya kike (gauni, sketi, blauzi, khanga na vitenge), katika mazingira ya sasa??

  Babu DC!!
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Bado tuna safari ndefu, pamoja na visababishi na viashiria vyote vilivyopo, hadi kufikia wakati ambapo hapatakuwa na maana au umuhimu wa kutambua na kuheshimu tafauti hizi. Suruali, mashati, sketi, blauzi na zinazofanana na hizi bado zitabaki kuwa na "label" ya KE au ME hata kama sisi kama watumiaji tutaamua kwa curiosity tu au uhuni kutokutaka ziwe na kutambulika hivyo.

  Exceptions ndio kama hizo hapo za orientation, presentation n.k. Kuna sarawili ambazo kwa definition ambayo tumejiwekea zinatambulika kuwa ni za Kike na zipo za Kiume (sasa baada ya kuongezeka kwa jinsi, nadhani pia zipo za transgender!). Iweje watu wanavaa nguo fulani zenye "label" tofauti na jinsi yao? Ukiniuliza nitakwambia sheer curiosity, the "nitoke vipi" mentality (the funnier and stranger, the better) na uhuni tu wa kwani nini bwana I am me and my world and I don't really care what ya'll think.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  ashukuru hata hayo mavazi yanayovaliwa, maana tunaelekea hata nguo atakua hazioni labda asifike.........
   
Loading...