BBC: Udororo wa uchumi waathiri sekta ya kilimo Tanzania

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Uchumi waathiri sekta za kilimo na viwanda Tanzania
  • 28 Februari 2017
Mshirikishe mwenzako
Ripoti mpya ya Benki Kuu ya Tanzania inaeleza jinsi ukuwaji wa taratibu wa uchumi wa taifa ulivyo athiri sekta muhimu nchini ikiwemo ya Kilimo na uzalishaji viwandani.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa shughuli kuu za uchumi zimeshuhudia kushuka kwa ukuwaji katika mwaka mmoja uliomalizika ikilinganishwa na mwaka 2015.

Je ina maana gani kwa nafasi ya ukuaji wa uchumi katika siku zijazo? Regina Mziwanda amezungumza na mwanauchumi DKT HOSEANA LUNOGELO, na kwanza amemuuliza takwimu hizi zina maana gani kwa uchumi wa taifa kwa siku zijazo?
 
Hii habari nilisikia BBC,nikaitafuta kwenye sources nyingine sikuipata nikadhani ni kama ile ya Trump kumfagilia magufuli.
 
BBC ni redio ya mkoloni inakazi moja tu, nayo ni ya propaganda.

Habari zao nazipa 50/50.

Kitendo walichokifanya kwa Gaddafi wa Libya ni tosha sana
 
Wa
BBC ni redio ya mkoloni inakazi moja tu, nayo ni ya propaganda.

Habari zao nazipa 50/50.

Kitendo walichokifanya kwa Gaddafi wa Libya ni tosha sana
BBC hawana maslahi yoyote taarifa iwe nzuri au mbaya Sizonje hana cha kuwafanya
 
Kati ya BBC na benki ya dunia, nani anaijuwa Tanzania vizuri kwenye maswala ya uchumi?
 
Yasemwayo ni kweli. Tumepiga hatua 30 nyuma kimaendeleo. Viongozi wengine ni mzigo tu.
 
Back
Top Bottom