BBC: Tanzania imezuia uzinduzi wa ripoti ya Human Rights Watch

Watanzania nyie watu wa ajabu sana...hii report inatetea watoto wenu na dada zenu wanaoonewa huko uarabuni still hamtaki kusikia....
Kwa nn serikali isitumie report hii kama base ya kutafuta ukweli kama amuwaamini hao walioiandaa?
Nimejaribu kumsoma mara mbili mbili nimetoka kapa. Kanishangaza sana.
 
Hizo ndio kazi Serikali inaweza kwa kiwango kikubwa, kukataza haki za kikatiba kwa wananchi. Haitaki kusikia makosa yake, serikali isiyokosea, serikali timilifu.
 
Balozi anaingiaje hapa? Mtu mzima kaenda kivyake Oman ubalozi ubahusikaje? CUF wengi wanazamia Arabuni au EU, ubalozi unahusika vipi?
Mkuu,,,mfanyakaz wa ndani ni kama mfanyakazi mwingine,,anaeajiriwa kwa mkataba na kulipwa kulingana na makubaliano yaliyokuepo,,,,ubaloz wa Tanzania Oman ndo Tanzania yenyewe,,na moja ya majukum yake ni kusimamia wananchi wake,,,siez ongelea report hii kukataliwa kusomwa maana sijui sababu haswa za kukataliwa ni zipi,,,lakin kama hakuna sababu,,ni sawa kabisa report hii ikisomwa hapa kumaanisha kuwa balozi hawatekelezi majukum yao na watz tunapewa taarifa kwanza kuijua hali halisi maana Serikali ni sisi kwanza.
 
Hawa human right watch nao wehu tatizo limetokea Oman halafu ripoti mnazindulia Tanzania kwa kiswahili hao waoman wataelewa kweli

Wewe unaonekana ndiyo mwenye tatizo. Watoto wako wanachukulilwa kwa hila na kwenda kuteswa. Unakataa kupewa taarifa itakayokusaidia kusimamia maisha ya watoto wako kwa namna nyingine, badala yake unataka eti yule mtesi wa watoto wako anayewachukua kwa hila ndiye apate hiyo report!.

Hii ni nini? Tanzania imekwisha!
 
anakataza kila kitu!!!! hivi Yale mageshi yashaanza ushionaji viatu mana wakuchoka watazingira MTU Mugabe jamani vijana tuokoleeni nchi kizalendo tu bila hata kumchanja mtu
 
Wewe unaonekana ndiyo mwenye tatizo. Watoto wako wanachukulilwa kwa hila na kwenda kuteswa. Unakataa kupewa taarifa itakayokusaidia kusimamia maisha ya watoto wako kwa namna nyingine, badala yake unataka eti yule mtesi wa watoto wako anayewachukua kwa hila ndiye apate hiyo report!.

Hii ni nini? Tanzania imekwisha!
hivi housegirl wako anaanza kazi na kumaliza saa ngapi? tuanze na hilo kwanza?
 
Hakuna haja ya kuzuia uzinduzi wake . Bora ukweli usemwe ili waarabu wajue kuwa tunajua matendo yao
 
Katika kila nchi kuna utaratibu wa kufanya utafiti, na katika nchi yetu mtafiti mgeni anabidi awakilishe proposal, kujanza fomu na CV yake ili kujua uwezo wa mtafiti na kujua kama njia anayotumia inaweza toa majibu sahihi ya tatizo analochunguza. Pia mtafiti anabidi kushirikiana na taasisi ya ndani au mtafiki wa ndani. Hivyo vyote hajafuata. Kama nchi tufanyaje?
 
Haya mambo yalianza awamu ya NNE , tatizo Letu pia wananchi tunaambiwa nchi za ghuba / warabu kama Oman na UEA siyo nzuri kufanya kazi za ndani ila wao hawaelewi.

Hata baada ya "Dada Husna" aliyesukumwa toka orofani hadi kupoteza maisha mwezi March, 2017 bado kuna watu walipinga kuwa atakuwa kafa tu au kadondoka mwenyewe bahati mbaya.

Any way, serikali inaelewa hatua za kuchukua tuachie balozi na wizara inayohusika itachukua hatua stahiki.

Pia, balozi zetu zinahitaji "reshuffle" maana malalamiko yamekuwa mengi sana kwa watanzania wengi walio nje ya nchi kukosa misaada pale inapotokea "emergency " na kuhitaji msaada wowote ule.

Hili jambo liangaliwe upya na kwa jicho la utaifa , uzalendo na utu.
 
Ila kuhusu report, kama pana taratibu hazikufatwa basi hakuna sababu ya HRW kulialia bali warudi watimize hivyo vigezo kisha watoe report yao.

Pia, hadi sasa hivi kwa lugha ya kukiuka amri/ katazo la kuzuiwa , HRW wameisha toa findings na conclusion kwenye vyombo vya habari pasipo ruhusa kwa kuzingatia katazo.

Naona HRW, iondolewe tu kwenye Asasi za kijamii iliyosajiliwa hapo Tanzania maana, hawajatii agizo la COSTEC.
 
Hakuna haja ya kuzuia uzinduzi wake . Bora ukweli usemwe ili waarabu wajue kuwa tunajua matendo yao

Ukweli hausaidii, kama tuna watu ambao hawasikii tangia awamu ya NNE , waziri wa kazi , watoto na jinsia alikuwa anaitwa G kabaka alikuwa anasema tunawatafutia watu kazi nje akataja Oman na UEA ila hakusema matatizo ya hao waendao huko yanatatuliwa na nani hali ya sintofahamu inapojitokeza!?

Sisi watafutaji huko nje tuangalie nchi za kwenda na pia tufanye tafiti na kuulizia tuendako kabla ya kwenda huko.

Ila balozi zetu , huko nje zinahitaji " reshuffle ya uhakika" maana , hakuna sababu ya kuwa na ubalozi ambao hauna msaada kwa ndugu na watanzania wenzentu wanapopatwa na masahibu.
 
Hawa human right watch nao wehu tatizo limetokea Oman halafu ripoti mnazindulia Tanzania kwa kiswahili hao waoman wataelewa kweli
Oman kiswahili kipo na hata kiongozi wao alipotembelea tanzania aliongea kiwahili.
 
Back
Top Bottom