BBC: Tanzania imezuia uzinduzi wa ripoti ya Human Rights Watch

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,771
102,124
Mamlaka nchini Tanzania imezuia uzinduzi wa ripoti kuhusu unyanyasaji wa wafanyikazi wanawake kutoka taifa hilo wanaofanya kazi katika mataifa ya Uarabuni.

Shirika la Human Wrights Watch limedai katika matokeo yake kwamba wafanyikazi wa nyumbani kutoka nchini Tanzania walikuwa wakibakwa , kuteswa na kulipwa mishahara duni na waajiri wao katika mataifa ya Uarabuni.

Ripoti yenye kurasa 100 inayodai kuteswa kwa wafanyikazi wa nyumbani wa Tanzania nchini Oman na muungano wa mataifa ya Emirata UAE ilitarajiwa kutolewa leo kwa waandishi wa habari mbele ya waathiriwa lakini hilo halikufanyika.

Katika hatua isiokuwa ya kawaida ,afisa mmoja kutoka shirika linalofadhiliwa na serikali la Sayansi na Teknolojia COSTEC William Kindekete alifutilia mbali mkutano huo katika mji mkuu wa Dar es Salaam akisema kuwa wanaharakati wa shirika hilo la haki za kibinaadamu hawakufuata sheria katika kufanya utafiti wao.

Hatahivyo matokeo ya utafiti huo wa HRW unaonyesha kuwa takriban wanawake 50 walihojiwa wakati wa utafiti huo ambao wanadai kwamba walilazimishwa kufanya kazi kwa kati ya saa 15 na 21 kwa siku huku wakipokonywa pasipoti zao na waajiri wao punde tu walipowasili katika mataifa hayo.

Ripoti hiyo ilibaini zaidi kwamba zaidi ya nusu yao hawakulipwa huku wengine wakisema kuwa hawakulipwa kabisa.

Wawili kati ya watano walidai kupigwa mbali na kunyanyaswa kijinsia.

Ripoti hiyo ya HRW pia inasema kwamba balozi za Tanzania katika eneo la Ghuba hazikutoa usaidizi wowote kwa waathiriwa wakati walipotaka usaidizi

Juhudi za kupata majibu kutoka kwa serikali ya Tanzania hazikufanikiwa kwa kuwa maafisa wengi hawakuwa tayari kuzungumzia swala hilo
 
Attachments

  • Screenshot_2017-11-15-19-50-22~2.png
    Screenshot_2017-11-15-19-50-22~2.png
    15.2 KB · Views: 54
Yaani haya mambo yalianza kama utani tu!

"Ilianza kama safari, twende Fulani ukaone, kumbe yananguvu in hatari..." Kizai zai..!!
 
Mamlaka nchini Tanzania imezuia uzinduzi wa ripoti kuhusu unyanyasaji wa wafanyikazi wanawake kutoka taifa hilo wanaofanya kazi katika mataifa ya Uarabuni.

Shirika la Human Wrights Watch limedai katika matokeo yake kwamba wafanyikazi wa nyumbani kutoka nchini Tanzania walikuwa wakibakwa , kuteswa na kulipwa mishahara duni na waajiri wao katika mataifa ya Uarabuni.

Ripoti yenye kurasa 100 inayodai kuteswa kwa wafanyikazi wa nyumbani wa Tanzania nchini Oman na muungano wa mataifa ya Emirata UAE ilitarajiwa kutolewa leo kwa waandishi wa habari mbele ya waathiriwa lakini hilo halikufanyika.

Katika hatua isiokuwa ya kawaida ,afisa mmoja kutoka shirika linalofadhiliwa na serikali la Sayansi na Teknolojia COSTEC William Kindekete alifutilia mbali mkutano huo katika mji mkuu wa Dar es Salaam akisema kuwa wanaharakati wa shirika hilo la haki za kibinaadamu hawakufuata sheria katika kufanya utafiti wao.

Hatahivyo matokeo ya utafiti huo wa HRW unaonyesha kuwa takriban wanawake 50 walihojiwa wakati wa utafiti huo ambao wanadai kwamba walilazimishwa kufanya kazi kwa kati ya saa 15 na 21 kwa siku huku wakipokonywa pasipoti zao na waajiri wao punde tu walipowasili katika mataifa hayo.

Ripoti hiyo ilibaini zaidi kwamba zaidi ya nusu yao hawakulipwa huku wengine wakisema kuwa hawakulipwa kabisa.

Wawili kati ya watano walidai kupigwa mbali na kunyanyaswa kijinsia.

Ripoti hiyo ya HRW pia inasema kwamba balozi za Tanzania katika eneo la Ghuba hazikutoa usaidizi wowote kwa waathiriwa wakati walipotaka usaidizi

Juhudi za kupata majibu kutoka kwa serikali ya Tanzania hazikufanikiwa kwa kuwa maafisa wengi hawakuwa tayari kuzungumzia swala hilo
Hawa human right watch nao tatizo limetokea Oman halafu ripoti mnazindulia Tanzania kwa kiswahili hao waoman wataelewa kweli
 
Hawa human right watch nao wehu tatizo limetokea Oman halafu ripoti mnazindulia Tanzania kwa kiswahili hao waoman wataelewa kweli
Omani wanakifahamu kiswahili ila namshangaa school mate wangu William Kindeketa naye kujiingiza ktk hili
 
Kwa mwenendo wa awamu hii ya tano sitarajii wao kukubali watu huru kutolea maelezo yoyote juu ya mwenendo wa haki za binadamu hapa nchini na wananchi wake kwa ujumla.
 
Ningeshangaa maana maafisa wetu wa ubalozi huko Oman wameshutumiwa live na wahanga wa unyanyasaji ule mkubwa. Serikali ya "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" wakubali report izinduliwe tu
Serikali ya hapa kazi tu haijali wanawake wakibakwa huko Oman bali wao wanajali misaada toka kwa serikali ya Oman ni Aibu kubwa sana kuendeleza misaada kuliko haki za watanzania wanaoteseka huko.
 
Kwa mwenendo wa awamu hii ya tano sitarajii wao kukubali watu huru kutolea maelezo yoyote juu ya mwenendo wa haki za binadamu hapa nchini na wananchi wake kwa ujumla.
Mtukufu yy anataka pesa toka Oman hajali kama Raia wake huko Oman wanabakwa na kuporwa pesa zao
 
Awamu hii ya Maliyamungu na Mtukufu hawana uchungu na watanzania wote walipo nje ya Nchi wao wanataka pesa toka kokote watanzania wanapoteswa hata wakiuawa wote wao hawajali kitu.
 
Hawa human right watch nao wehu tatizo limetokea Oman halafu ripoti mnazindulia Tanzania kwa kiswahili hao waoman wataelewa kweli
Report ikizunduliwa huwekwa kwenye Lugha zote isitoshe kampuni zinazowapeleka wafanyakazi Oman zipo Tanzania na baada ya Uzinduzi ingesaidia Ubalozi wa Tanzania Nchini Oman kuzinduka na kuanza kuwasaidia watanzania wanaotaabika huko majumbani mwa waarabu.
 
Labda mimi niulize wadau. Wanaonyanyaswa ni wafanyakazi wa kitanzania pekee au wote wenye asili ya Africa? Kama na nchi zingine wananyanyaswa kwa nini repoti ijielekeze kwa Tanzania pekee? Naona kuna ukakasi katika kuzuia ripoti sawa na ukakasi ulioko kwenye ripoti.
 
Labda kama hufwatilii mambo. Nchi nyingine Nyingi tu zimeishatoa ripoti hizi kwa jinsi nchi za kiarabu zinavyo nyanyasa wafanyakazi wa kiafrika.
Mfano; wa hizi ripoti ni ile iliyotolewa Nigeria
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom