Uchaguzi 2020 BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa

Ni kweli kabisa, kama ilivyo kampeni za ccm za kuwaleta marais wa nje nyingine kuja kuwaombea kura, kinyume kabisa cha sheria za kimataifa, zinazokatisha nchi moja kutojiingiza kwenye siasa za nchi nyingine.
You are talking about sheria za kimataifa?! Unataka nilete humu ile video ya wazungu wa Lissu akiwemo Amsterdam na wenzake walichopanga dhidi ya Tanzania...wamepanga kuchochea maandamano na mauaji ili vurugu zitokee na kinachoitwa jumuiya ya kimataifa iitishe mkutano wa usuluhishi na Lissu...wazungu hao wanasema na kuropoka bila aibu kwamba ni lazima damu imwagike Tanzania...kuchomwa kwa ofisi za chadema ni miongoni mwa mikakati hiyo...
 
Kwa hyo mkuu kabudi ametuingiza chaka kuwa tutapata 50/50 ya mgawanyo?alafu mbona vyombo vya habari vya ndani havihoji ili jambo kuwa mkataba umesainiwa ikulu,hii imekaaje kiongozi wangu?
Vyombo vya Habari vipi tena Mkuu?? Vyote vilishawekwa mfukoni na mtu mmoja. Mfumo wetu wa Uongozi umeshanajisiwa na Mtu mmoja hivyo unahitajika kufumuliwa na kusukwa upya. Na hili litaweza kufanyika tu nje ya ccm na si vinginevyo.

Ukishakuta Kiongozi anaetumia mamlaka yake kuingilia uhuru wa Mihimili mingine kama Bunge na Mahakama basi usitegemee uhuru ktk kupata na kutoa Habari. Angalia magazeti Nchini yamepoteza mvuto. Hakuna wafuatiliaji wengi kama ilibyokuwa hapo awali. Vivyo hivyo ktk Vyombo vyetu vingine vya Habari.
 
Ukweli ni upi? Mbona mnataka kuwafanya watu Kama watoto wadogo?! Unadhani watu hawafahamu kwanini mahojiano hayo yamefanyika wakati huu wa uchaguzi ?!Na kwanini huyo Zuhura Yunus asiweze kubalance stori kwa kumleta mtu wa madini kutoka serikalini? Unadhani watu hawajui lengo la mabeberu kwa kutumia media BBC Swahili kipindi hiki? Huyo Zuhura hamnazo Kama ilivyo kwa kijana yule aliyekuwa akihojiwa na aliyejiita mchambuzi...hiyo BBC Swahili ilileta hoja hiyo ya madini kipindi hiki Cha uchaguzi makusudi..stupid BBC...That is not professionalism...
Hata mimi mkuu nimeshangaa siku zote BBC walikuwa wapi?wanavizia kampeni ndio wanaanza kuhoji,Ila pia mimi kama mwananchi wa kawaida naishauri Serikali yangu mikataba kama hii iwe inajadiliwa bungeni na kuwekwa wazi,ili sisi wakaazi wa huku Busonzo tusisubiri mpaka BBC watuambie,
 
Wakuu Jana niliangalia BBC Swahili, wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa, hivi hiki chombo cha habari cha mabeberu kinatutafutia nini?

Ok
Hata lissu alisemea bbc kuwa tutapelekwa miga sijui mica
 
Watapeli sio Barrick ni magufuli na ccm....

Ndio wanaohadaa watz kwa kuomgo wao huku wakiwaita barrick wanaune....

Viongozi wa ccm wanamakubaliano binafsi na barrick sio kwa manufaa ya nchi bali ya viongozi hao wakuu kabisa wa mihimili..... Ndio maana wamekazana kutunga sheria ili waruhusiwe kuvunja katiba ya nchi na wasishitakiwe...... Mnadhani hii inamaanisha nn? Hii ndio maana yake halisi......

Tumsaidie Tundu Lissu tuikomboe nchi hii inayoendeshwa kihuni na kilaghai na magufuli na ccm

Tundulisi si ana character zote za kibeberu , si bora jiwe ambaye hata kwao hataki kwenda
 
Nimemsikiliza Zuhura Yanus, BBC ni waongo, hakuna mkataba wala makubaliano ya 2017, mkataba ni mmoja tuu, ule uliosainiwa Ikulu 2019!.
Yale ya 2017 yalikuwa ni mapendekezo tuu.
BBC Swahili Iache Uongo!.

NB, uongo kama huu wa BBC pia uliwahi kuletwa na ZZK, baada ya kuona makubaliano yamekuwa initialed, akaandika mkataba umesainiwa.
Tulisaidia kufafanua
Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
P
Kama ni waongo basi fungia Star TV ili watu tusisikie "uongo".
 
Ok
Hata lissu alisemea bbc kuwa tutapelekwa miga sijui mica
Hata mm nashangaa maana tuliambiwa na lisu kuwa tutashitakiwa MIGA matokeo yake hatujashitakiwa wala nn,pia tuliambiwa na Serikali kuwa makinikia hayataondoka na tutajenga smelter hapa hapa,lakini matokeo yake makinikia bado yanaondoka pia smelter haijengwa mpaka leo,Sasa sisi wakazi wa huku Katoro tuamini kuwa lissu alitudanganya na Serikali pia imetudanganya?au nyinyi wa huko mjini mnaonaje huko?
 
Nilisikiliza taarifa yote ya habari...na mchambuzi huyu wa Chadema...very stupid indeed...BBC wamefanya hivyo makusudi kwa kumleta anayejiita mchambuzi kutoka Chadema..ni mkakati wa kampeni za Chadema
Lissu alisema ile report ya makinikia ni professorial rubbish sasa yametimia.
 
Nimemsikiliza Zuhura Yanus, BBC ni waongo, hakuna mkataba wala makubaliano ya 2017, mkataba ni mmoja tuu, ule uliosainiwa Ikulu 2019!.
Yale ya 2017 yalikuwa ni mapendekezo tuu.
BBC Swahili Iache Uongo!.

NB, uongo kama huu wa BBC pia uliwahi kuletwa na ZZK, baada ya kuona makubaliano yamekuwa initialed, akaandika mkataba umesainiwa.
Tulisaidia kufafanua
Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
P
Issue ni kipi wanainchi wanakielewa zaidi kuhusu madini kwa awamu hii ya tano, hayo unayodai mapendekezo ndio yapo kwenye vichwa vya wananchi wengi kwa kuwa ndiyo yaliyosemwa sana au kuelezewa na hayo yaliyomo kwenyw mkataba wananchi wanahisi ndio yale yaliyokuwa yanapendekezwa.
Hivyo ni vema vipengele vilivyopo kwenye mkataba viwekwe wazi ili kutoa tafirsili iliyoshihi
 
Nimemsikiliza Zuhura Yanus, BBC ni waongo, hakuna mkataba wala makubaliano ya 2017, mkataba ni mmoja tuu, ule uliosainiwa Ikulu 2019!.
Yale ya 2017 yalikuwa ni mapendekezo tuu.
BBC Swahili Iache Uongo!.

NB, uongo kama huu wa BBC pia uliwahi kuletwa na ZZK, baada ya kuona makubaliano yamekuwa initialed, akaandika mkataba umesainiwa.
Tulisaidia kufafanua
Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
P
Hoja ni je aliuosema yule mtaalam aliyekuwa anahojiwa ni uongo au ukweli? Jibu ni ukweli yaani Hadi kupigwa watu risasi ilikuwa ni kutafuta hisa 16% tuu? Huku si kupigwa ikizingatiwa watangulizi wa jiwe walifikisha umiliki Hadi adilimia 40 kwenye mgodi wa williamson,sasa jiwe ndio kafanyaje hapo? Labda alikuwa anatafuta pesa za kampeni almaarufu kushika uchumba maana mambo mengine yote yamesalia Kama zamani na mengine yamekiukwa kabisa kwa mujibu wa bbc na yule mtaalam waliomhoji
 
Kila goti litapigwa kwa mabeberu, Hata Morales wa Bolivia alijitahidi kusimama dhidi ya hawa mwishowe alishindwa na kufurushwa.

Mikataba ya kimataifa ni migumu na inabidi kuheshimiwa na ni suala mtambuka hasa kutokana na ukosefu katika ujuzi wa kufanya kazi na uhaba wa teknolojia , bila kusahau mabenki ya Tanzania kuwa na mitaji pungufu kuweza kuhimili miamala mikubwa ktk fedha za kigeni.

Miamala mikubwa wa fedha za kigeni inaweza kuyumbisha mabenki hivyo ni moto usioweza kuhimiliwa na mabenki ya Tanzania na kuchelewesha shughuli hizi za chapchap za minada ya madini na ununuzi au ukodishaji wa zana nzito za vifaa vizito vinavyotumika ktk uchimbaji na utafutaji.
Ndio maana Lisu na cdm wamekuwa clear kwamba wao wanataka ubia na wawekezaji wenye uwezo na teknolojia sio vita,hapa ni Bora kuwesesha wazalendo kwa kuwapa mikopo ya mitaji kuliko kuwasubili wazungu kwa kila kitu
 
Hata mimi mkuu nimeshangaa siku zote BBC walikuwa wapi?wanavizia kampeni ndio wanaanza kuhoji,Ila pia mimi kama mwananchi wa kawaida naishauri Serikali yangu mikataba kama hii iwe inajadiliwa bungeni na kuwekwa wazi,ili sisi wakaazi wa huku Busonzo tusisubiri mpaka BBC watuambie,
Kipi Bora kwako kuhoji sasa ili kuweka wazi ambacho hakiwezi kuhojiwa ndani au kukaa kimya tuendelee kupigwa bila kujua? Huoni Lisu alikuwa sahihi toka zamani Hadi sasa kuhusu madini?
 
You are talking about sheria za kimataifa?! Unataka nilete humu ile video ya wazungu wa Lissu akiwemo Amsterdam na wenzake walichopanga dhidi ya Tanzania...wamepanga kuchochea maandamano na mauaji ili vurugu zitokee na kinachoitwa jumuiya ya kimataifa iitishe mkutano wa usuluhishi na Lissu...wazungu hao wanasema na kuropoka bila aibu kwamba ni lazima damu imwagike Tanzania...kuchomwa kwa ofisi za chadema ni miongoni mwa mikakati hiyo...

Acha tu kuleta video, ilete na ikiwezekana omba airtime kwenye vyombo vyote vya habari ili kila mtu aone alichopanga Lisu na hao wazungu. Halafu nyie mkichezea matokeo ya box la kura, mtatuonyesha hao waafrika wanaowatuma tumwage maji.
 
Nilisikiliza taarifa yote ya habari...na mchambuzi huyu wa Chadema...very stupid indeed...BBC wamefanya hivyo makusudi kwa kumleta anayejiita mchambuzi kutoka Chadema..ni mkakati wa kampeni za Chadema
Acha ujinga basi kidogo! Alichozungumza Thabiti kinasikika kwa kila anayehitaji kusikia, hebu sasa wewe jibu hoja moja baada ya nyingine katika kile ambacho kimezunguzwa..
 
Acha ujinga basi kidogo! Alichozungumza Thabiti kinasikika kwa kila anayehitaji kusikia, hebu sasa wewe jibu hoja moja baada ya nyingine katika kile ambacho kimezunguzwa..
Kweli wewe ni Chadema ambao hawezi kuacha kutumia neno mjinga kwenye mijadala...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom