BBC Swahili wajue Tanzania ni nchi huru

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Nchi yetu ni moja ya nchi duniani inayoongozwa kidemokrasia na kwa kufuata mfumo wa utawala wa sheria.

Mfumo ambao chombo kikuu cha utoaji haki mtu au taasisi inayodhani imedhulumiwa haki yake kwa mujibu wa Ibara ya 107A (1) ni Mahakama pekee, na kwa mujibu wa sheria, kanuni pamoja na taratibu za uendeshaji mashauri Mahakamani, wananchi tunazuiwa kujadili au kuzungumzia shauri lililoko mbele ya Mahakamama ili kupitia kujadili na kuzungumzia shauri hilo tusije tukajikuta tunaingilia uhuru wa Mahakama au kuathiri shauri wakati wa kutoa maamuzi.

Kwa kipindi kirefu Shirika la Utangazaji Uingereza BBC kupitia Idhaa yake ya Kiswahili, aidha kwa makusudi limekuwa likiingilia mambo ya ndani ya nchi yetu.

Na kibaya zaidi linafanya hivyo kwa kuingilia maswala ya kisheria zikiwemo kesi ambazo ziko Mahakamani zikingojea kusikikizwa au kutolewa uamuzi, ambapo miongoni mwa mashauri yanayoshupaliwa na shirika hili, ni pamoja na kesi ya mwandishi Erick Kabendera iliyoko Mahakamani.

Watangazaji wa Shirika hili wamefikia hatua ya kumhoji mama mzazi wa Erick Kabendera na kumwelekeza cha kusema, akimwomba msaada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amsamehe mtoto wake, utadhani kama Rais ndiye ameamuru Erick Kabendera kushikiliwa, wakati anashikiliwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, kuna raia wangapi walioko kwenye Magereza ya Tanzania kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo uhujumu uchumi, mbona hao Bbc haiwazungumzii? Huyu Erick Kabendera anao unuhimu gani wa kipekee kujadiliwa na BBC?

Tukumbuke Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano kupitia Ibara ya 13 (1) imetamka wazi kwamba:

"Watu wote ni sawa mbele mbele ya sheria, na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria"

Kwa msingi huo kusiwe na vyombo vya habari au waandishi wa habari wenye jukumu la kutetea baadhi ya raia kwa maslahi binafsi, huku kundi kubwa likiachwa bila kutetewa.

Ifahamike, vyombo vya habari ni taasisi zinazopaswa kufanya shughuli zake kwa weledi mkubwa, na tumeshuhudia mara kwa mara uvunjifu wa amani, machafuko na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia mahali ambapo vyombo vya habari visivyozingatia maadili kupitia kwa baadhi ya waandishi wa habari wasiokuwa na maadili jinsi walivyotumia kalamu zao vibaya kusambaratisha mataifa mbali mbali.

Kwa maoni yangu, kitendo hiki kilichofanywa na BBC kumhoji mama mzazi wa mwandishi Erick Kabendera na kumwelekeza kuomba msaada kwa Rais wa nchi kuhusu kuachiwa kwa mtoto wake si tu kwamba kinaingilia mifumo yetu ya utoaji haki nchini ukiwemo Uhuru wa Mahakama, bali pia kinachonganisha wananchi na Rais wao ili ionekane mbele ya jamii kwamba, bila Rais Magufuli kuingilia kati, Mahakama haiwezi kumtendea haki mwandishi Erick Kabendera kuhusiana na shauri lililoko mbele ya Mahakama.

Naiomba serikali ichukue hatua ikiwemo kulitaka Shirika la Utangazaji Uingera BBC kuacha kuingilia mambo ya ndani ya nchi, hususani uhuru wa Mahakama.

Aidha serikali pia ichukue hatua dhidi ya waandishi wa habari mfano wa Sammy Awami anayewakilisha BBC hapa Tanzania ikiwemo kuwaonya na kama onyo halitasaidia, basi isimamishe kwa muda leseni zao za uandishi wa habari.

Hatuwezi kuendelea kufumbia macho uchochezi wa kiwango hiki. Sisi ni nchi huru inayojiendesha na kujiamulia mambo yake kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu za nchi.

Tuulinde uhuru wetu kwa gharama yoyote, tusikubali kutawaliwa kwa mlango wa nyuma na kuelekezwa cha kufanya hata kisichostahili tufanye.

Tumejenga amani na utulivu kwa akili na maarifa yetu wala hatukufundishwa na BBC jinsi ya kuondoa ukabila, kuondoa ubaguzi wa rangi nk.

#TUIACHE_MAHAKAMA_IFANYE_KAZI_YAKE

Imeandaliwa Na
Mkweru Zakaria Maswale.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmadhani kuwa mnatuhumiwa na kushutumiwa ftom no where kams ninyi mnavyolalamika kimizuka from no where?
Mlipewa hedhima ya kuwa nchi huru kwa kupewa maazimio, sheria na mikataba ya kimataifa hivyo mnalaumiwa sababu ya kwenda kinyume na mliyoyakubali awali.
 
Mimi sumlaumu Kijana Sammy kama mtangazaji, najua yupo kazini na anatumwa kufanya ivyo kwa mujibu wa maelekezo ya waajiri wake.
Kingine ni kwamba mjue tu kwamba BBC ni chombo cha mabeberu, na kamwe hawawezi kurusha habari ambazo ni chanya kwetu wao ni kurusha habari ambazo ukiziangalia na kusikiliza vizuri, ni habari zilizojaa uvunjifu wa Amani, vurugu na uchochezi.
Kamwe hutosikia habari njema kutoka Afrika zikitangazwa na BBC,
Kimsingi ni vyombo vyote vya magharibi ndiyo vyenye mlengo uwo wa hupotoshaji, km si uchochezi kwa misingi ya Uhuru wa habari.
 
Uwezi kuwa huru Afrika kaka, Zimbabwe si unawaona? Watu wenye uhuru wao wameminya kidogo tu si wale pale unaona wanalia kila siku, uwez kuwa huru wakati ww ni maskini hata Condom unaomba
 
inawezekana alikua anawasaidia katika kazi zao za kuichafua Tanzania kimataifa
ndomana wanaivalia njuga hii ishu
 
Mimi sumlaumu Kijana Sammy kama mtangazaji, najua yupo kazini na anatumwa kufanya ivyo kwa mujibu wa maelekezo ya waajiri wake.
Kingine ni kwamba mjue tu kwamba BBC ni chombo cha mabeberu, na kamwe hawawezi kurusha habari ambazo ni chanya kwetu wao ni kurusha habari ambazo ukiziangalia na kusikiliza vizuri, ni habari zilizojaa uvunjifu wa Amani, vurugu na uchochezi.
Kamwe hutosikia habari njema kutoka Afrika zikitangazwa na BBC,
Kimsingi ni vyombo vyote vya magharibi ndiyo vyenye mlengo uwo wa hupotoshaji, km si uchochezi kwa misingi ya Uhuru wa habari.

Basi angalia TBC
 
Back
Top Bottom