BBC swahili upande wa mtandao badilikeni

8ATP

Senior Member
Jul 27, 2017
167
217
BBC swahili ni chombo kikubwa ambacho mtu akitaka kupata habari za uhakika lazima akilini mwako bbc swahili ichukue nafasi.

Lakini cha kushangaza hivi karibuni kumekuwepo makosa mengi ya kiuandishi (typing errors) pia makosa ya matumizi ya kiswahil sanifu, jambo ambalo linakata mzuka hata wa kufuatilia habari zake.

Kwa mfano mpaka sasa kwa upande wangu BBC swahili upande wa mtandao nishaona wababaishaji, yaani baada ya kuwa mfano kwa bloggers wadogo lakini wao wamekua kama mtandao wa kijana ambaye anajifunza kutengeneza website. Kwa mfano leo tu makosa niliyoyaona kwenye taarifa zao:

Viaripoti baadala ya vyaripoti.
Isiy baadala ya Isiyo.
suitafahamu baadala ya sintofahamu.​

Ni bora ingekua inatokea mara moja ila imekua ni mara kwa mara.,
BBC SWAHILI ONLINE MUBADILIKE (BBC SWAHILI ONLINE, YOU NEED TO CHANGE)
ngoja nitupie na ung'eng'e kidogo labda London watasikia.
 
Siku hizi BBC wanazingua sana, nilikua mfuatiliaji wa habari zao sana ila kwa sasa napitia kwa nadra sana kwenye tovuti yao. Niliwahi kuandika mada inayofanana na hii mwaka 2018

 
Back
Top Bottom