BBC swahili radio inazidi kushuka kiwango

Kigger

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
805
710
Sasa hivi BBC radio imeshuka kiwango sio bbc ile ya miaka ya kipindi cha nyuma, yaani ni kucheka cheka tu muda wote hawana story za msingi
 
sasa hivi bbc radio imeshuka kiwango sio bbc ile ya miaka ya kipindi cha nyuma, yani ni kucheka cheka tu mda wote hawana story za msingi
Wamebaki na udaku tu! Hawana wachunguzi wala wachambuzi wa habari, hakika imekuwa radio hovyo kabisa!
 
Hakuna makala za uchambuzi zilizofanyiwa tafiti. Hata kwenye mahojiano wanapwaya sana. DW wako vizuri hasa kipindi chao cha saa saba mchana cha MAONI.

Wana interview watu kwa staha nakuwapa nafasi ya kujieleza kwa utulivu na muda wa kutosha
 
Bibisii ya Marehemu Zeyana Seif, Tido muhando, Ally Salehe, Chama Omary Matata, Suluma Kassim haipo tena
 
  • Thanks
Reactions: Ctr
Mambo yanabadilika kadri muda unavyozidi kwenda mbele, cha muhimu inatakiwa na wewe ubadilike, sasa hapo ndio sijui ubadilike vipi na sijui mambo yepi yamebadilika ila nachojua redio zimekua nyingi mfano CRI,
 
Nenda kwenye tovuti yao ya Kiswahili unaweza kulia, habari hazieleweki kabisa. Redio ya BBC Swahili haina tofauti na redio za FM za nchini Tanzania kwa sasa.

BBC Swahili bora, ilikuwa ya miaka hiyo, siyo ya sasa.
 
Zimebaki redio chache sana za Kimataifa ambazo zinatoa huduma iliyo bora kwa lugha ya Kiswahili. Binafsi, nawapa namba moja DW Swahili. Watangazaji wake wapo siriasi na kazi. BBC Swahili hakuna kitu kwa sasa!
 
Huyu mtangazaji mpya tokea EARADIO Anazingua kazidisha kucheka.

Pia kuna mdau huko juu kagusia suala la interview hawatoi muda wa kutosha mtu anaelezea jambo hajamaliza within short time anakatishwa halafu wanaendelea na mambo yao.

Imekuwa wasafi fm na redio zingine za kibongo.

Samahani dada Kisanga kama huko humu.
Ujirekebishe.

DW wako vizuri nawapa
 
sasa hivi bbc radio imeshuka kiwango sio bbc ile ya miaka ya kipindi cha nyuma, yani ni kucheka cheka tu mda wote hawana story za msingi

Kirusi Kimoja ' HATARI ' kilichoingia hapo kiitwacho Scola kikitokea East Africa Radio na East Afrca Television ndicho kimeharibu Kila Kitu japo hata Dada Regina nae amezidisha sana Mizaha na Kuiondoa kabisa ile ' radha ' ya Kipekee ya iliyokuwa BBC ya akina Tido Mhando au hata ile ya kabla ya akina Tido ya Wakongwe. Nakubaliana nawe kwa 100% kuwa BBC ya sasa ' inaboa ' na ina Utoto na Upuuzi mwingi sana tu na nashangaa Kuona hata wenyewe hawajajishtukia katika hili. Siku si nyingi na Wenyewe tutaanza Kuwaita ' Waswahili Waswahili ' kutokana na Utangazaji wao. Wewe Mtu muda wake wote alikuwa anatangaza Kipindi cha ' DADAZ ' cha Wanawake kilichojaa Umbea, Majungu, Uswahili, Utoto na hata tabia za Kihuni ( Kimalaya ) tupu leo hii unamuajiri aje atangaze Kipindi cha Watu Makini na Kinachohitaji Akili Kubwa Kukiendesha kwani Kisiharibike tu Mkuu? Nimependa mno hii ' Observation ' yako na natamani Uongozi wao BBC wasome haya Maoni yetu ili wawahi Kujitathmini na ikiwezekana hata Kujirekebisha kwani bado hawajachelewa kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom