BBC Swahili: Karibu Wakenya milioni 2.6 tayari wana virusi vya corona

Masi Lambo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
532
360
Karibu Wakenya milioni 2.6 tayari wana virusi vya corona, wanasayansi wameeleza baada ya kupima damu iliyotolewa kwa ajili ya protini inayotumika kwenye mfumo kinga.

Protini hiyo (antibody) hutengenezwa na mwili kwa ajili ya kushambulia virusi na bakteria, na uwepo wake kwenye damu unaashiria kuwa mtu huyo hakuwahi kuwa na maambukizi- hata kama mtu huyo hakuwahi kuonesha dalili.

Watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa tiba nchini Kenya wameunga mkono mfuko wa kuchangia damu uliofanyika nchi nzima kati ya mwezi Aprili tarehe 30 na tarehe 16 Juni.

''Kupimwa kwa antibodies kumeonesha kuwa Wakenya wengi tayari wamepata maambukizi kuliko ilivyokuwa ikibainika katika shughuli za upimaji nchini humo.,'' Ilieleza taasisi ya Kemri mapema wiki hii ikinukuliwa nan a gazeti la the Star nchini Kenya.

Virusi vya corona: Utafiti wabaini Wakenya karibu milioni 2.6 wameugua Covid-19 - BBC News Swahili
 
Kenya inafeli wapi? Hata baada ya kufuata taratibu, kupokea misaada na kukesha kuisakama Tz mbona namba kubwa hivi?

Narudia tena. Wanakuza idadi ili kupokea fedha zaidi. IMF, WHO & WB wanatapeliwa. Years later there will be a movie about this shit.
 
Mmmm itakuwa uchumi wao utapanda sana mabeberu wakijua wao wanaichukulia kwa makini sana Corona.
 
Back
Top Bottom