BBC: maoni ya wasikilizaji kama kura za maoni za Synovate

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Nimefuatilia ujumbe mfupi ambao wasikilizaji walituma BBC leo saa 12:30 jioni. Sikuhesabu idadi lakini takribani ujumbe 15 zilizohusu Chadema, ni ujumbe 2 tu ziliunga mkono maandano ya Chadema jana. Wafuasi wa Chadema huwa hawasikilizi BBC? Mbona ujumbe uliotumwa VoA zote zimelaani serikali na polisi? Au BBC wanashirikiana na ccm kuchakachua ukweli wa mambo?

Mkuu wa matangazo alikuwa Charles Hillary.
 
Unajua tena tumetuma jumbe lakini msomaji ndiye anayechagua za kusoma. Well, acha lisemwe watakalo kusema lakini wengine tutasimamia kwenye ukweli na siyo unafiki.

Mimi si mpenzi wala mwanachama wa Chadema ila vitendo vya Polisi vimeniudhi. Waliojeruhiwa au kuuawa wana familia kama mimi. Binafsi nina mikono yote na miguu yote na elimu zuri lakini bado maisha yananigonga. Fikiria walioko hospitalini na waliopata vilema na waliobaki yatima.... inakuwaje?
 
Hata walipokuwa wanamhoji Mbowe walikuwa wanambana mno
 
Si hawa ndiyo walitabiri kwamba Kikwete angeshinda ushindi wa kishindo? Hawana maana hawa wameshapoteza credibility yao.
 
gurudumu> kwani charles hilari si ni walewale kama tido na kibonde wa clous hawana jipya
 
Mie tangu wakati wa uchaguzi niligundua BBC wameamua ku take sides. Tena wakati huo nilikuwa bado CCM mpaka nilipotoka kwa ajili ya kuibiwa pesa zetu kwa michango ya msg. Hata hivyo nimewashangaa sana hawa waliopaswa kuwa professionals wa kuigwa. Nimeachana na BBC
 
Aahhhaaa mimi nilidhani nimeacha kuisikiliza BBC kumbe tuko wengi? Dahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hata ITV saa nne na nusu usiku wamekusanya maoni ya waliolaani Chadema tu!!!
 
Back
Top Bottom