hayaland
JF-Expert Member
- May 4, 2012
- 712
- 399
Nilikuwa nafuatilia habari za BBC London katika television. Cha kushangaza habari ya mlima Kilimanjaro na harakati za nchi kuzima moto katika mlima huo mkubwa barani Afrika ameripoti mwandishi Emmanuel Igunza kutoka nchini Kenya. Nimejiuliza sana kwa nini habari za Tanzania aripoti mwandishi kutoka nchi jirani?
Haya matukio ya mwandishi kuripoti habari za nchi nyingine tumezoea kuziona katika nchi ambazo zina vita. BBC wakiripoti habari za Somalia mwandishi wa habari lazima atoke nchini Kenya.
Nimejiuliza kwa nini mwandishi wa BBC aliye Tanzania hakuripoti habari hii na kuripotiwa na mwandishi kutoka Kenya?
Inaumiza sana