Bazazi na kondomu

mtukichwa

Member
Oct 11, 2010
34
8
Kuna jamaa mmoja alikuwa na tabia ya kutembea na ndugu wa wapenzi zake. Taarifa zikawafikia ndugu za mpenzi wake mpya ambae yeye kwa maelezo yake ndio alitaka kumuoa.

Sasa katika kulijadili swala hilo kama ni la kweli ama ni la uongo, ndugu wa mchumba wakapanga wamtegeshee jamaa na kumpima kama tuhuma ni za kweli ama ni uzushi mtupu. Hivyo wakamleta binamu wa yule mchumba wa yule jamaa ambae alikuwa ni chotara wa kiarabu na kisomali kwa ajili ya kuipima imani ya jamaa.

Ikafika siku jamaa akatambulishwa kwa binamu. basi jamaa kama kawaida akaanza kumzoea kwa sana yule mdada na outing za ushemeji zikaongezeka. Ndipo familia ikaamua itege siku watu wote wajifanye wamesafiri kisha jamaa aje apewe mzigo. Basi jamaa kama kawa akatia timu, na binamu bila kujivunga akaanza kumtega jamaa na kivazi chepesi na mikao ya ajabu ajabu. Sasa jamaa akaona isiwe taabu wacha nifuate KONDOMU katika gari nije kumaliza mzigo.

Kumbe muda woote huo watu wapo nje wanasubiria kuja kufumania. Sasa baada ya kuona jamaa anaelekea kwenye gari (Wakidhani jamaa amekereka na yale mambo na ameamua kuondoka) si ndio wakajitokeza na kumpa jamaa stori nzima pamoja na mtego huo. kwahiyo jamaa akashinda uaminifu wa familia na tuhuma zote kuonekana ni majungu tu kisha akapewa mke.

MORAL OF THE STORY IS NEVER CARRY CONDOMS TO YOUR INLAWS HOUSE.
 
Duh!jamaa wangechelewa kidogo tu,wangekutana naye akiwa anarudi baada ya kumaliza mchezo!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom