BAWATA:Chuki binafsi na Msukumo wa Dr Kigwangala ndio chanzo ya kumfungia Dr Mwaka

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,816
HATUA ya kituo cha tiba asili cha tabibu Dk. Juma Mwaka ‘Foreplan’ pamoja na vituo vingine viwili, kumesukumwa na maslahi binafsi, anaandika Regina Mkonde.

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini limelalamikiwa kuchukuwa hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa msukumo wa binafsi ya baadhi ya watumishi wa baraza hilo na kwamba, sababu zilizotolewa ni za ‘kipuuzi’.

Pia imeleezwa kwamba, hatua hiyo ni juhudi za kurudisha nyuma ama kukwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa Tiba Asili.

Hayo yamesemwa leo na Mohamed Matokeo, Mwenyekiti wa Baraza la Waganga wa Tiba, Ushauri na Utafiti wa Dawa Asili Tanzania (Bawata) wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Bawata tukiwa chombo huru cha waganga wa tiba asili, tunasikitika sana utendaji kazi unaofanywa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ambacho ni chombo cha kiserikali kilichopewa mamlaka ya kusimamia taaluma hii na kuiendeleza,” amesema na kuongeza;

“Lakini baraza hilo limekuwa ni chombo kinachorudisha nyuma fani ya tiba asili hapa nchini, kwani limekuwa likikwamisha kwa makusudi juhudi za waganga wa tiba asili walioonesha ufanisi katika kutoa huduma ya tiba asili.

Imekuwa kawaida kwa baraza hilo kuitisha au kuwafungia waganga wa tiba asili na vituo vyao kwa sababu zinazoonekana ni za kibinafsi.”

Matokeo ametoa mfano wa tukio lililotokea jana la kufungwa kwa baadhi ya vituo vya tiba asili ambapo amesema kuwa, wahusika walifungiwa pasipo kupewa nafasi ya kujitetea na au kuhojiwa.

“Sisi bawata tunapinga hatua hii ya kiuonevu kwani wametoa maamuzi ya kuwafungia bila ya kuwahoji wahusika, tena hawa ni waganga halali kisheria wamesajiliwa na wanalipa kodi vizuri,” amesema.

Sharifu Karama, Katibu Mkuu Taifa wa Bawata amedai kuwa, kuna baadhi ya watumishi wa afya wanaojishughulisha na uuzaji wa dawa za tiba asili kwamba ndiyo wanaochochea kukandamizwa kwa masilahi ya waganga wa tiba asili nchini.

“Kuna baadhi ya watumishi wa afya wanauza dawa za tiba asili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo kwenye jengo la serikali.

“Kutokana na hali hiyo, Bawata tunaamini kwamba, baraza la tiba asili na tiba mbadala linaongozwa na waganga wa kisasa na kwamba tuna taarifa kuwa, kuna baadhi ya viongozi wa baraza hilo nao wanauza dawa asili kwa hiyo wanalitumia baraza kutimiza hadhma yao,” amesema.

Hata hivyo, Foreplan ilianza kuwindwa na Hamis Kigwangala, Naibu Waziri wa Afya baada ya kufanya ziara ya kushtukiza tarehe 15 Desemba mwaka jana na kuibua maswali mengi.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutolewa siku saba za uchunguzi na kwamba, kinachofanyika sasa kinatajwa kuwa ni matokeo ya ‘dhamira’ iliyooneshwa baada ya ziara hiyo.
image.jpeg
 
sina hakika na tiba za huyu jamaa,
Ila nasiki akina mama wakienda masuala ya uzazi anawavua nguo na na kufanya trace pass kitu ambacho sio sahihi
 
View attachment 365987
Duh!
Hawa jamaa elimu naona hamna
 
Haijalishi kuwa watu wana wivu au chuki
ukweli ni kwamba kitendo cha Mwaka kujiita 'daktari' huku akifanya matangazo makubwa ya TV
na akivaa kabisa kama 'daktari' aliesomea ni 'utapeli'....

mimi binafsi nilikua naamini ni daktari aliesomea muhimbili na baadae kufanya tafiti zake binafsi
na kuanzisha clinic yake
kumbe sio hivyo
 
Huyu DOCTOR Mwaka mbona alikuwa kama medical doctor badala ya kuwa wa tiba mbadala, si mumeona alikuwa anavaa stetoscope shingoni? je! huyo ni wa tiba mbadala kweli?
 
Kwa hili kama kigwa umefanya nakuunga mkono MTU alikuwa anajifanya Dr kwa kuvaa koti jeupe stetoscope shingoni na kuwadanganya mama zetu na dada zetu kwani angevaa kaniki watu wasingeenda na kufanya kipindi kuelezea viungo vya mwanamke kama Dr kweli safi sana hiki kituo kifungiwe maisha tu
 
NAMNUKUU, “Kuna baadhi ya watumishi wa afya wanauza dawa za tiba asili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo kwenye jengo la serikali."

Elimu inasaidia sana. Hawa jamaa hawana elimu ndo maana wanaropoka tu.

ITM pale Muhas ni kituo cha muhimu sana katika utafiti wa dawa asilia. Pale dawa asili zinatafitiwa kitaalamu na kwa usafi zaidi. Pale kuna watu na Phd zao.

Wanafanya EXTRACTION ya Active ingredients baada ya kufanya utafiti wa kina mainly kwa kutumia animal models. Kuna research yangu moja nilifanya pale...!

Enzi hizo nikiwa chuo nilikuwa sinywi soda au juisi za dukani, nilikuwa naenda kununua ROSELA wanazotengeneza pale; Pia dawa za malaria .. nk

Hawa waganga wa jadi wafuate utaratibu & sio kutafuta JUSTIFICATION zisizo na maana.
Kwahiyo ulimfahamu Dr. Kayungi?
 
Nakumbuka mweshimiwa alisema "Mabadiliko ninayofanya mwanzoni yataleta maumivu kwa wananchi, lakini lazima tufanye ili nchi irudi kwenye msitari naamini badae watazoea"

Ha ha ha huko makazini watu wanakimbizana na vyeti sembuse huyu jamaa
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom