Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Hospitali ameenda sana mkuu. Madaktari walimshauri atumie tiba mbadala tofauti na upasuaji kwa hoja ya kwamba hata akifanya upasuaji uvimbe utarudi.
Walimshauri abadili life style, asiwe na msongo wa mawazo na pia ale mlo kamili pamoja na mboga mboga kwa wingi.
Jaribu hii, inaweza kukusaidia:
1. Iweke sehemu yenye uvimbe kwenye maji ya moto kwa muda wa kama nusa saa hivi asubuhi na jion,usiku.
2. Paka sehemu yenye tatizo(MNDUKUNI) mafuta ya mnyonyo kila baada ya kutoka kuiweka sehemu hiyo kwenye maji ya moto kila siku asubuhi na jion/usiku. Paka na lala nayo.
3. Jenga tabia ya kutawdha kwa kutumia maji ya moto.
4. Tumia kijiko kimoja kila siku kutwa mara tatu, mchanganyiko uliotengenezwa na asali, habal soda na mdalasini.
5. badili mfumo wako wa kula, kula vyakula vyenye kambakamba, epuka vyakula vya aina ya Chipsi.
6. na acha kutumia pilipili.

Inshallah
 
Wakuu kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na hizi vimbe za sehemu ya haja kubwa ambazo zimekuwa zikiniletea maumivu makali kwa kipindi cha miaka mitatu.

Nilijaribu dawa mbali mbali zikiwemo anusol ya cream na suppositories lakini hazikuwahi kunisaidia hadi ikafikia kipindi nikashauriwa kufanyiwa upasuaji lakini nilikataa kutokana na wengi wanaofanyiwa upasuaji huu ugonjwa umekuwa ukiwarudia baada ya miaka kadhaa

Nilijaribu na baadhi ya dawa za mitishamba lakini bado hazikufua dafu bali vimbe ziliendelea kunitesa hadi ikafika kipindi nikakata tamaa

Lakini mwezi uliopita nililetewa na shangazi yangu dawa iliyo kwenye kichupa kidogo iliyo katika mfano wa maji maji

Nilipouliza nikaambiwa ni maji ya mgomba yalioandaliwa kwa kuchanganywa na mafuta ya mnyonyo kiasi.

Wakuu nimetumia ndani ya wiki vimbe zote zimepotea kabisaa.
Kama kwenu kuna migomba usikate aisee huwezi jua kesho yako

Nawasilisha

Ahsante sana kwa kutufahamisha dawa hii.
Maradhi haya yanatesa watu wengi sana hivyo utakuwa umewasaidia na hakika utalipwa heri nyingi.
Amiin
 
Wakuu kwa muda mrefu nimekuwa nikisumbuliwa na hizi vimbe za sehemu ya haja kubwa ambazo zimekuwa zikiniletea maumivu makali kwa kipindi cha miaka mitatu.

Nilijaribu dawa mbali mbali zikiwemo anusol ya cream na suppositories lakini hazikuwahi kunisaidia hadi ikafikia kipindi nikashauriwa kufanyiwa upasuaji lakini nilikataa kutokana na wengi wanaofanyiwa upasuaji huu ugonjwa umekuwa ukiwarudia baada ya miaka kadhaa

Nilijaribu na baadhi ya dawa za mitishamba lakini bado hazikufua dafu bali vimbe ziliendelea kunitesa hadi ikafika kipindi nikakata tamaa

Lakini mwezi uliopita nililetewa na shangazi yangu dawa iliyo kwenye kichupa kidogo iliyo katika mfano wa maji maji

Nilipouliza nikaambiwa ni maji ya mgomba yalioandaliwa kwa kuchanganywa na mafuta ya mnyonyo kiasi.

Wakuu nimetumia ndani ya wiki vimbe zote zimepotea kabisaa.
Kama kwenu kuna migomba usikate aisee huwezi jua kesho yako

Nawasilisha
Hayo mafuta unakunywa au unapaka mkuu. Mimi nina mgonjwa.
 
Kuna mti unaitwa mlonge jaman, kama mtu anashida hiyo ajaribu kunywa mlonge, achemshe majani yake anywe tena anywe kwa wingi, siku moja tu maumivu yatapungua na matumaini atayaona
 
Hii issue ni serious case.
Kuna ndugu yangu hawezi kukaa kwa zaidi ya dakika tatu,miezi kadhaa sasa. Analalamika kuna uvimbe mkubwa sana so akikaa unapasuka na kutoa damu. Hizo enusol zote kamaliza, aloevera nayo katumia sana.

Naomba mtoa mada atoe ufafanuzi vizuri jinsi ya kutengeneza hii dawa.
Mimi mwenyewe naona dalili kama kauvimbe kanaanza anza hivi.
Pamoja na hio dawa ya mgomba jitahidi unywe maji ta kutosha kwani wengi wetu ni wavivu na matokeo yake ni choo kigumu(constipation)utachubuka tu na kuota hizo haemorrhoids ama bawasili..
 
Back
Top Bottom