Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Wana JF naomba kuuliza hivi, Uvimbe (vinyama) ambao huwa unaota sehemu ya haja kubwa kuna namna ingine ya kuundoa bila kwenda hospitali kufanyiwa operesheni?? Naomba mnijuze.
 
Pole Laura,

Matibabu ya Haemorrhoids (vivimbe vya damu njia ya haja kubwa) yanategemea na grade ya hilo tatizo. Daktari anakuexamine na kukuuliza maswali kisha anadetermine ni grade ngapi.

- Grade 1: Zinatoka damu wakati wa haja kubwa lakini hakuna kivimbe kilichotokeza nje ya mk*nd* (kumradhi kwa lugha)
Hapa matibabu ni kutumia vidonge maalum vinawekwa kwenye njia ya haja kubwa (rectal suppositories (scheriproct)), na pia kula chakula chenye roughage ya kutosha mfano moboga za majani, matunda kama mapapai, parachichi, embe etc, na maji kwa wingi.

- Grade 2: Zinatoka damu na kuna kivimbe/vivimbe kilichotokeza hasa baada ya haja kubwa lakini kinarudi chenyewe ndani baada ya haja.
Hapa matibabu ni rectal suppositories, chakula chenye roughage na sclerotherapy (sina uhakika kama tiba hii ipo Tanzania tayari).

- Grade 3: Zinatoka damu na kuna kivimbe/vivimbe hasa baada ya haja kubwa, na havirudi vyenyewe..mpaka urudishe kwa kusukuma na kidole/vidole.
Hapa matibabu ni upasuaji tu hamna jinsi.

- Grade 4: Zinatoka damu, kuna vivimbe hata bila haja, vivimbe havirudi hata vikisukumwa na vidole, wakati mwingine maumivu na hata damu kuvilia kwenye vivimbe.
Hapa matibabu ni upasuaji tu hamna jinsi. Na inawezekana hata upausuaji zaidi ya mara mbili au tatu.

Ushauri: Kamuone daktari bingwa wa upasuaji haraka, akuexamine kupata grade, kisha akushauri matibabu gani ni stahiki.
 
NB: Jifunze kuwa na muda maalum wa kwenda haja kubwa (bowel training). Unaamua kama ni asubuhi au jioni saa 12 basi kila siku unaenda chooni muda huo hata kama hujabanwa, usijikamue....tulia tu utumbo mkubwa wenyewe utasukuma ukizoea. Hiyo itakusaidia kupunguza kusukuma na kusabbisha kivimbe kutoka nje na kumwaga damu. Utakapozoea basi kila muda huo ukifika utajisikia kwenda haja, na ukienda chooni bila kusukuma choo kinatoka, na uvimbe unakuwa hautokezi nje.
 
hivo vinyama vinasababishwa na nini?

- Matatizo ya kutopata choo kama constipation, kupata choo kigumu sana
- Kula sana vyakula visivyo na roughage (low fiber diet)
- Kuongezeka kwa mkandamizo tumboni..mfano wakati wa kusukuma choo, au ukiwa na uvimbe mkubwa wa tumbo
- Wakati au baada ya ujauzito
- Kukosekana kwa valve za veins zinazodrain kwenye njia ya haja (hii ni inakuwa kwenye familia fulani fulani, ndio maana unaweza kuta haemorrhoids zinarithiwa)
- Uzee
-
 
Riwa nakushukuru sana kwa maelezo uliyotoa hapa nahisi nahitaji kumuona daktari. Maana uvimbe wangu ni mkubwa sana na kwa grade ulizoainisha hapa nipo grade 3.
 
Riwa nakushukuru sana kwa maelezo uliyotoa hapa nahisi nahitaji kumuona daktari. Maana uvimbe wangu ni mkubwa sana na kwa grade ulizoainisha hapa nipo grade 3.

Pole Laura...usihofu, ukimuona daktari atakushauri, kama ni uvimbe mmoja inakuwa raishi pia kwa operation, maana huwa inatokea kuwa na uvimbe zaidi ya mmoja, na operation huwezi toa vivimbe viwili kwa wakati mmoja.
 
Laura Mkaju;


Pole sana Laura,Go and see a doctor na Utapona tu,Fuata Ushauri wa Riwa,ni dhahiri ni wa Kitaalamu!!
Binafsi niliumwa Ugonjwa huo Mwaka 2008 na nilifanyiwa Operesheni uvimbe ukaondolewa katika hospitali ya Regency!! Ni operasheni ndogo sana hivyo hakuna chochote cha kuhofia; Ikiwa Diagnosis ya Mganga itahitaji ufanyiwe Upasuaji basi chagua wakuchome sindano ya ganzi ili uchape Usingizi ukiamka unakuta watu wameshamaliza kufanya mambo yao kuliko kuchomwa kwenye uti wa mgongo(sina hakika ya kumbukumbu zangu kuhusu hii option ya pili lakini nadhani daktari wangu aliniambia ipo)

Kwa sehemu kubwa Ugonjwa huu unasababishwa na Ulaji Usio zingatia kanuni ambao husababisha Kupata choo kigumu mara kwa mara,kujikamuakamua wakati wa downloading husababisha vijinyama kutoka nje,Maji Mengi,Vyakula vyenye kambakamba(Fibre),eg Mapapai,Mboga za majani,Matunda etc ndiyo dawa ya kuhakikisha tatizo hilo halijirudii tena!!
Kupatapata choo kigumu ni Hatari sana;Mimi tangu siku ile vyakula hivyo ni vipaumbele kwangu!!

Ugua pole,nadhani Riwa anaweza kuwa wa msaada zaidi,Ugua Pole!!!
 
Last edited by a moderator:
Na mimi ugonjwa huu unanisumbua sana tu,kwa sasa umri wangu ni miaka hamsini na mara nyingi napoenda haja kubwa najikamua sana mpaka huwa nasikia kizunguzungu.Miaka 4 iliyopita nilipimwa Buganso na wakagundua vivimbe hivo na nikafanyiwa procedure inaitwa lords,lakini hivi sasa naona kama tatizo limerudi tena so kuna wakati na bleed sana wakati wa haja kubwa na kuna wakati si bleed nimepimwa kila vipimo kukgundua kuna tatizo gani laknini majibu yako ok sasa nifanyeje,naomba ushauri
 
Na mimi ugonjwa huu unanisumbua sana tu,kwa sasa umri wangu ni miaka hamsini na mara nyingi napoenda haja kubwa najikamua sana mpaka huwa nasikia kizunguzungu.Miaka 4 iliyopita nilipimwa Buganso na wakagundua vivimbe hivo na nikafanyiwa procedure inaitwa lords,lakini hivi sasa naona kama tatizo limerudi tena so kuna wakati na bleed sana wakati wa haja kubwa na kuna wakati si bleed nimepimwa kila vipimo kukgundua kuna tatizo gani laknini majibu yako ok sasa nifanyeje,naomba ushauri

Haemorrhoids ni ugonjwa mgumu kutibu ukapona kabisa, especially kama kwenye familia mna historia ya kuwa na tatizo hilo. Inamaana kuna mapungufu katika veins zinazodrain mfuko na njia wa haja kubwa (anorectal). Kwa hiyo utakuta tatizo linajirudia rudia.

Kwa ujumla vivimbe vya haemorrhoids vinakuwa vimejaa damu, wakati wa haja kubwa au kustrain kivimbe kikubwa kinaweza pasuka na kutoa damu (fresh blood) nyingi tu, hali hiyo inaweza endelea kwa siku kadhaa mpaka vivimbe viishe kupasuka, halafu inakata huku vivimbe vipya vikijitengeneza, vikushakuwa vikubwa vinaanza tena kupasuka na kumwaga damu. Mzunguko ndio unakuwa hivyo.

Ukifanyiwa operation wanakuwa wanashona ile sehemu yenye kivimbe na kupunguza uwezekano wa kivimbe kurudi tena hapo, hivyo inachelewesha vivimbe kutokea tena hata for years. Lakini inawezekana kutokea tena. Kwa hiyo siyo jambo la kushangaza sana kama ulitibiwa na sasa vimerudi tena, unahitaji matibabu tena. Ila pia fuatilia jinsi ya kukinga kwa kutumia diet na kujitrain kwenda choo kwa muda.
 
Jaribu kunywa maji mengi sana ... maji ni muhimu mno

Mkuu RIWA HAPO JUU AMEKUPA PERFECT MEDICAL ADVICES wacha mi niongezee kidogo nikupe some algorthimic tips how to reduce Pain If have any

1. Apply directly a cold pack on the hemorrhoid region to lessen the inflammation and the pain. The easiest method to do this is to ask a loved one to apply the cold compress as you are lying face down.

2.If your using toilet paper before you use it dampen it with water or baby oil. Baby wipes are also recommended as they are extra gentle for your sensitive skin

3. Always clean the region well with lukewarm water may times every day. A bidet is very effective for this purpose

4. As much as possible, do not sit or stand for long periods.

5. Take a hot bath several times a week. Do not take salt baths as they can cause irritation in the hemorrhoid. Also, avoid strong detergents in cleaning your anal area.

6. To help achieve smooth bowel movement, add fiber into your diet. Take fresh vegetables and fruits that are high in fiber. Legumes, beans and whole grains are also highly recommended for fiber intake

7.As i told you before add water consumption. Try to drink at least eight to ten glasses a day. This will smoothen your stool, allowing smooth passage.

8. Exercise every day. Do brisk walking or jogging at least 30 – 45 minutes, three to four times a week. This will help in the food absorption and make moving your bowels less painful.

9. Do not push hard during bowel movement. It can cause extra strain to the hemorrhoid and can cause further damage.

10. Avoid lifting heavy objects. If it is unavoidable, use proper body posture and mechanics to prevent putting extra pressure and tension on the lower extremities especially the pelvic area.

11. Take over-the-counter drugs recommended to ease hemorrhoid pain. Those drugs that contain corticosteroids are effective in combating pain. However, you should check at least with the store pharmacist to be sure that the drug can help your condition. You should remember to take these drugs on the prescribed period as prolonged intake can cause inflammation or pockmarks in the anal lining.

12. In few cases, hemorrhoids need proper surgical treatment, either through sclerotheraphy, to reduce the size of the piles, or the rubber band ligation or clinically known as hemorrhoidectomy. Ask your physician to know more about other treatments.

13. Do not believe that rectal or anal bleeding is rooted mainly from hemorrhoids. It can be a sign of a serious health problem kama damu inatoka for a long time Kimbia haraka hospitali
 
pole sana Laura,
Kuna siku nilkuta kipindi cha afya jamii ITV kama miezi miwili iliyopita walkua wakielezea hili tatizo na kutoa ushauri ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa (tiba mbadala).
Kwa kweli sikufanikiwa kupata kila kitu lakini ilkua tiba nzuri sana!
Labda mwenye uelewa zaidi au aliyebahatika kukipata vizur kipindi atusaidie
 
Kwa kuongezea tu, naomba tusiamini uchawi/kurogwa maana tiba zote zite na scientifically proven kwamba zinatibu. Pole mwana jf mwenzangu na muone dr kwa tiba zaidi.
 
kwa maelezoo yako inaashiria kama ana kitu inaitwa GENITAL WARTS (sunzua laini), jikabidhi kwa daktari aliyefuzu, utapata jibu kama zinahitaji dawa, kuzichoma (cauterization) au kuzikata (excision).
 
Beware!
It might be cancerous. You cut you promote growth.
Pamoja na lugha yako mbaya, chukua "kazi" yako ipeleke kwa daktari wa kina mama. Uchunguzi ufanyike ijulikane ni nini ndo tiba ifuate.
Huwezi kurupuka kutoa tiba hujui nini unatibu lol!
 
Mkuu hiyo dawa uliyoitaja unaijua vizuri lkn? Naona unataka huyo msichana atoke mbio akiwa uchi maana atasikia kitu inawaka moto.Hiyo haishauriwi kuwekwa kwenye open wound na maumbile ya mwanamke hayana tofauti sana na open wound ndo maana ukimpaka pilipili kwenye nyeti zake basi utakuwa umezua balaa kubwa.
By the way kama tatizo ni warts basi zinatakiwa zichomwe kwa kutumia Caustic pencil(silver nitrate pencil) ambayo inatakiwa ifanywe na daktari mwenyewe.Otherwise please consult a medical doctor immediately.

Ni vigumu kutamka tiba ya aina gani aitumie kabla ya Daktari kuviona na kuvichunguza sawasawa. Sababu ni kwamba yapo maoteo ya namna nyingi sehemu za siri na kila moja likiwa na sababu zake. Kuna genital warts zinazosababishwa na aina fulani za virusi, kuna papilloma, condyllomata acuminata kama complications za magonjwa ya ngono yasiyotibiwa kikamilifu na bila kusahau maoteo ya jamii za saratani. Namshauri mhusika amwone Daktari yeyote hata kama si Gynaecologist kwa vile kimsingi madaktari wote wana uelewa angalau wa msingi kwa matatizo ya jumla na ni wao huamua endapo tatizo lina uzito wa kumwona Bingwa wa maradhi au wamalize wenyewe.

Nasisitiza tena kwamba aina ya matibabu ni sherti yaamuliwe na Daktari atakayemuona, kupima uzito wa tatizo, kulielewa na kufanya uamuzi wa kutibu na si ushauri wa vijiweni bila ya kumwona mhusika.
 
Back
Top Bottom