BAWACHA: Spika Ndugai kuita barua rasmi kipeperushi ni kiburi cha madaraka. Amekuwa Mtetezi wa wanawake kuanzia lini?

Hotuba ya Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu
Yaani Chadema hopeless kabisa.Hakina msemaji ? yaani eti hotuba ya mjumbe wa kamati kuu

Duni alikuwa sahihi aliposema Chadema kila mtu ana sharubu

Kila mtu anajiibukia tu na kutoa hotuba
 
Absolute power corrupts absolutely. Hapo ndo alipofika Ndugai. Yuko kwenye rebellious corner ya madaraka kama akina Nebkadreza ambao walikuwa wanadharau kila order haha ya Mungu mwenyewe!!!
 
Nionavyo mimi, kukata rufaa kwa waathiriwa ni ushahidi kuwa walishafukuzwa uanachama na wamekosa sifa ya kuendelea kuwa wabunge wa bunge la JMT, kwa mujibu wa Katiba.

Rufaa maana yake ni 1) ama ku'restore' haki iliyokiukwa kwa upande wa waathiriwa 2) au ku'approve' uamuzi uliokwishafanyika kwa upande wa chama.

Mimi nadhani ukimya wa wabobezi wa sheria katika suala hili unatia shaka kubwa ya kuonyesha njia kunapojitokeza ukinzani wa jambo kama hili, hasa ambapo ukinzani wenyewe unatokana na tafsiri ya Katiba ya JMT.

Wabobezi wetu katika mambo ya sheria wameonyesha 'ostrich spirituality of burying the head in sand'.
 
Barua kutoka ktk chama husika unaita kipeperuushi?

Hiki kiburi cha madaraka ni ulafi wa kijinga kabisa.
 
Hivi wakiondolewa akina Halima ndio majina mengine yatatumwa rasmi NEC na Bungeni au?
 
The man is not sick. Ana akili timamu kabisa. Kitu ambacho wengi wetu tunashindwa kuelewa ni kwamba Ndugai hatetei hao COVID-19, bali anatetea LIGASI.

COVID-19 ni mojawapo ya LIGASI kuu za Chuma, Shujaa wa Afrika ambazo watetezi wamejiapiza watazitetea mpaka silaha ya mwisho iliyoko mikononi mwao! Kwa hivyo, ni mpambano mgumu.
Mimi nafikiri tofauti kidogo kama alivyosema Ndugai mwenywe haya mambo ni magumu saana, yaani yeye kapewa maelekezo na mwenda zake awaapishe wabunge hao 19 ,hakuwa na choice by then,angepinga agizo hilo muhimili mmoja usingeweza kufanya kazi na muhimili mwengine ,sasa angefanyeje ? ilibidi akubali kwa uhai wa Taifa kwa wakati huo...kwa sasa ameshauri wasililizwe kwenye kati kuu ya chadema , Barua iambatanishwe na muhutasri wa kikao hicho then awatimue thats all...mwacheni mzee spika kazi ya uongozi ni ngumu ....
 
Hotuba ya Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu

Tarehe 20 April 2021 Naibu Spika alitoa kauli Bungeni kwamba ofisi ya Spika haikuwa na taarifa rasmi ya CHADEMA kuhusiana na kuvuliwa uanachama kwa waliokuwa wanachama wake 19.

Ibara ya 67 (1)(b)ambayo imeweka masharti na sifa za mtu kuteuliwa kuwa Mbunge kuwa ni lazima awe amependekezwa na Chama cha siasa ‘ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.

Mei 3, 2021 Spika ameonyesha Barua aliyopokea kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Bungeni. Hii inaonyesha nia ovu kwenye ofisi ya Spika. BAWACHA tunamtaka Spika aueleze umma ni lini alipokea barua hiyo na pia kutoa ufafanuzi wa kwanini kunakuwa na kauli mbili kinzani ndani ya ofisi

Spika pia amezungumzia Suala la viambatanisho kwenye barua,hii ni hoja isiyokuwa na mashiko kwani si mamlaka ya Spika kudai viambatanisho hivyo. Ni dhahiri kwamba Spika anatengeneza hoja zisizo na msingi juu ya udhaifu wake katika kutekeleza matakwa ya kikatiba aliyoapa kuilinda.

BAWACHA tunajiuliza, je wakati CCM kinamuandikia barua ya kumvua uanachama Sofia Simba au wakati CUF wanamuandikia barua ya kuwavua uanachama wanawake 8 waliokuwa wabunge wa viti maalum alikuwa wapi kudai viambatanisho hivyo? Au huu utaratibu ni kwa CHADEMA tu?.

Hata hivyo badala ya kujibu barua ya Katibu mkuu, Spika ameibuka miezi mitano baadae na kuzungumza bungeni ambako si njia rasmi ya mawasiliano lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa CHADEMA ndani ya Bunge anayeweza kujibu hoja hizo.

Hii inaonyesha namna gani Spika anavyotumia vibaya madaraka yake na kuonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi.

Katika maelezo yake Spika ameiita barua aliyoandikiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA “Kipeperushi”. Hii ni dharau kubwa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini kilichosajiliwa kisheria.

Kuiita Barua rasmi kipeperushi inaendelea kuonyesha kiburi cha madaraka alichonacho Spika ambacho kinaendelea kumshushia hadhi mbele ya jamii.Sisi Baraza la Wanawake Chadema hatutakuwa tayari kuona viongozi wetu wakidhalilishwa na chama chetu kikidharauliwa na tena.

CHADEMA ina katiba yake na ndani ya katiba hiyo kuna miongozo, kanuni na taratibu kuhusu vikao na uendeshaji wa Chama. Kwa muktadha huo mkutano wa Baraza Kuu ambalo litapitia Rufani iliyokatwa na waliokuwa wanachama hao litakaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Hata hivyo kukata rufani hakutengui maamuzi ya awali mpaka hapo rufani hiyo inaposikilizwa na maamuzi kutoka tofauti na maamuzi ya awali.

Kitendo cha Spika kutochukua hatua kwa kuwa kuna rufani imekatwa kupinga maamuzi ya awali linaonyesha namna gani alivyo na nia ovu juu ya jambo hili kwani anaelewa namna taratibu zilivyo na kwa makusudi ameamua kupindisha. si mamlaka ya Spika kuingilia mambo ya ndani ya chama.

Sisi Baraza la Wanawake Chadema tunapenda kuwahakikishia umma wa watanzania kwamba Chama chetu hakina mfumo dume kwa sababu, mosi, ndio chama chenye wajumbe wengi wa kamati kuu wanawake (9) kuliko vyama vingine vyote vya siasa kikiwemo Chama anachotoka Spika.

Katika kikao kilichofanya maamuzi ya kuwavua uanachama kulikuwa na wajumbe Wanawake 4 kwasababu wengine 5 walikuwa kwenye kundi la watuhumiwa.

Pili, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Chama chetu ndio kilipitisha wanawake Zaidi ya 60 kugombea nafasi za ubunge wa majimbo kuliko vyama vingine vyote pengine kwenye ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati.

Leo hii Spika anajivika hadhi ya kuwa mtetezi wa wanawake huku akiwa amesahau kwamba ni yeye ambaye Bunge lililopita alikuwa mstari wa mbele kutweza haki za wanawake kiasi cha kuwafukuza bungeni wanawake ambao baadhi ni sehemu ya hao wanaoitwa wabunge 19 kushiriki vikao.

Spika Mtetezi wa wanawake, amekuwa akitumia askari wa kiume kuwaondoa Bungeni baadhi ya hao wanaoitwa wabunge 19 bila kujali jinsia zao

Wakati Halima na Esther walipopigwa na kuumizwa na askari Magereza Spika alionekana kufurahia tukio hilo. Hivyo ni unafiki mkubwa kujivika kilemba cha kujifanya ni mtetezi wa haki za wanawake.

Katika Bunge lililopita Chama cha Wananchi (CUF) kiliwavua uanachama wanachama wake 8 Wanawake waliokuwa Wabunge wa Viti Maalum na pale Spika alipoandikiwa barua aliwaondoa Bungeni mara moja.

Kwenye barua yake Spika alisema “Suala la kuwavua uanachama wanachama ni suala la utashi wa chama” sasa iweje leo Spika huyo huyo ajisahaulishe kuwa amewahi kuwavua ubunge wabunge 8 Wanawake kwa mara moja na leo hii kujifanya amegeuka ghafla kuwa mtetezi wa wanawake?

CADEMA imewahi kuwavua uanachama wabunge wake 4 wa kiume, je na huo pia ulikuwa mfumo jike kama anavyodai sasa hivi kwamba Chadema ina mfumo dume?.

Kikao kilichokaa na kuwavua uanachama wanaoitwa wabunge 19 ni kikao halali cha Kamati Kuu ya Chama ambacho kinaundwa na wajumbe wa jinsia zote na kina mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.

Wakati wa kusikilizwa kwa shauri la kuwavua uanachama, waliokuwa wanachama hao waliitwa kwa barua kuhudhuria kikao hicho ili waweze kusikilizwa lakini walikataa kuhudhuria hivyo shauri lao likasikilizwa bila wao kuwepo.

Kwa mujibu wa taratibu pale unapoitwa na ukakaidi kuhudhuria basi haki yako ya kusikilizwa inapotea hivyo shauri lako litasikilizwa upande mmoja (ex parte hearing).

Suala la maridhiano ni baina ya CHADEMA na Rais na kwa kutambua umuhimu wake CHADEMA ilimuandikia barua rais naye pia kwa kutambua umuhimu wake akakubakubali hivyo halina mahusiano yoyote na Spika.

Baraza la Wanawake CHADEMA tunaona kama Spika ana lengo la kuvuruga mazungumzo hayo huenda akawa na manufaa binafsi kuona nchi iliyogawanyika.

Pia tunapenda kumwambia Spika kwamba chama chetu hakina mgogoro wowote na hata pale kunapotokea mgogoro Katiba yetu inatuongoza namna ya kushughulika na utatuzi ndani ya chama.

Suala tunaloliongelea ni kuhusiana na waliokuwa wanachama wetu ambao tuliwavua uanachama kwa kosa la usaliti, uasi, ubinafsi na kugushi nyaraka za chama na ni jukumu la Spika kufanya kazi yake na sio kuwa mshauri wa namna ya kuendesha chama chetu.

Kwa maelezo yake,Spika amesema hapangiwi lini achukulie hatua suala la wanaoitwa wabunge 19. Spika anatakiwa atambue kwamba suala la utekelezaji wa Katiba si suala la utashi wa yeye kuamua ni lini achukue hatua. Hivyo tunamtaka Spika atekeleze matakwa ya kikatiba.

Taratibu za upatikanaji wa Wabunge wa Viti Maalum kwenye Chama huanzia ngazi ya chini kabisa kabla ya kufikia Kamati ya Utendaji na kisha Sekretarieti ya BAWACHA Baada ya hapo majina hupelekwa kwenye Kamati kuu ambayo hupitisha majina na kuyawasilisha Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Hivyo basi wanaoitwa wabunge 19 kujichagua na kujipeleka kwenda kuapa sio tu kwamba ni uvunjaji wa Katiba ya Chama Bali ni kiwango cha juu kabisa cha ubinafsi, uasi na usaliti.

Tunamtaka Spika atueleze wakati anawaapisha wanaoitwa wabunge 19, aliwaomba nakala ya Katiba, muhtasari nanyaraka nyingine anazozitaka Sasa hivi?.

Mwisho tunawaomba waandishi wa habari na umma tuendelee kumuuliza maswali ya msingi Spika kama tulivyoainisha hapo juu lakini kubwa likiwa ni kwanini anaendelea kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda? Je, anaweka mfano gani kwa wananchi.

Kwamba leo wanaweza kuvunja Katiba kama anavyofanya yeye kwa kiburi na wasichukuliwe hatua? Na je hizi hoja zake, zinailenga CHADEMA peke yake au ana maslahi binafsi na wanaoitwa wabunge 19?.

Tunazitaka Kamati za Utendaji za BAWACHA kila Jimbo kukutana hara kwa ajili ya kujadiliana hatua stahiki za kuchukua juu ya suala hili kwani sisi kama chama tutasimamia utekelezwaji wa Katiba ya JMT na hatutakuwa tayari kuona mtu yoyote, mwenye madaraka yoyote akiivunja katiba.

Baada ya kupokea mapendekezo kutoka Majimboni tutatoa maazimio ya hatua gani tutachukua kushinikiza utekelezaji wa jambo hili. Haijalishi kama wangekuwa wanaume au Wanawake kama ilivyo Sasa, pale Katiba itakapovunjwa tutasimama, kukemea na kuchukua hatua.

Tunamtaka Spika sio tu ajisifie ni miaka mingapi amekaa ndani ya bunge, bali aangalie kwenye kipindi cha uongozi wake ameacha alama gani chanya kwenye Taifa.

"Alama hizi lazima ziwe zile zinazotuunganisha kama nchi, kuleta Amani, haki na usawa kwa wote huku ikiweka misingi ya kuheshimu Katiba, Sheria na taratibu mbalimbali tulizojiwekea.
Kile ni kipeperushi tu. Jitahidini kuwa na elimu ya utumani wa nyaraka zilizokamilika.
 
Ndugai jibu hoja toka kwa BAWACHA kwamba Je huo urafiki wako na wao wa namna ya Kharidi na Filimoni umeanza lini?
 
Mimi nafikiri tofauti kidogo kama alivyosema Ndugai mwenywe haya mambo ni magumu saana, yaani yeye kapewa maelekezo na mwenda zake awaapishe wabunge hao 19 ,hakuwa na choice by then,angepinga agizo hilo muhimili mmoja usingeweza kufanya kazi na muhimili mwengine ,sasa angefanyeje ? ilibidi akubali kwa uhai wa Taifa kwa wakati huo...kwa sasa ameshauri wasililizwe kwenye kati kuu ya chadema , Barua iambatanishwe na muhutasri wa kikao hicho then awatimue thats all...mwacheni mzee spika kazi ya uongozi ni ngumu ....
Sijui wewe unauona uongozi wa aina gani?
Kupewa amri kutii mambo ambayo siyo haki, siyo sheria na siyo hata kanuni za kazi yako, ukatii, huo hauwezi kuwa uongozi.
Mtu asiyeamini ktk highest good of anything hafai kuongoza.
Mie ningemheshimu kama kiongozi kwa kukataa shinikizo kama lilikuwepo kulingana na unavyosema.
Kumbuka uzuri wa juu wa mtu yeyote ni kuwa tayari kufa kwa ajili ya ukweli unaouamini.
The highest good of any individual is to die for what he/she believes to be true.
You are not ready to die for the principles you believe In, you are definitely unfit for Leadership.
 
Hotuba ya Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu

Tarehe 20 April 2021 Naibu Spika alitoa kauli Bungeni kwamba ofisi ya Spika haikuwa na taarifa rasmi ya CHADEMA kuhusiana na kuvuliwa uanachama kwa waliokuwa wanachama wake 19.

Ibara ya 67 (1)(b)ambayo imeweka masharti na sifa za mtu kuteuliwa kuwa Mbunge kuwa ni lazima awe amependekezwa na Chama cha siasa ‘ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.

Mei 3, 2021 Spika ameonyesha Barua aliyopokea kutoka kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA Bungeni. Hii inaonyesha nia ovu kwenye ofisi ya Spika. BAWACHA tunamtaka Spika aueleze umma ni lini alipokea barua hiyo na pia kutoa ufafanuzi wa kwanini kunakuwa na kauli mbili kinzani ndani ya ofisi

Spika pia amezungumzia Suala la viambatanisho kwenye barua,hii ni hoja isiyokuwa na mashiko kwani si mamlaka ya Spika kudai viambatanisho hivyo. Ni dhahiri kwamba Spika anatengeneza hoja zisizo na msingi juu ya udhaifu wake katika kutekeleza matakwa ya kikatiba aliyoapa kuilinda.

BAWACHA tunajiuliza, je wakati CCM kinamuandikia barua ya kumvua uanachama Sofia Simba au wakati CUF wanamuandikia barua ya kuwavua uanachama wanawake 8 waliokuwa wabunge wa viti maalum alikuwa wapi kudai viambatanisho hivyo? Au huu utaratibu ni kwa CHADEMA tu?.

Hata hivyo badala ya kujibu barua ya Katibu mkuu, Spika ameibuka miezi mitano baadae na kuzungumza bungeni ambako si njia rasmi ya mawasiliano lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa CHADEMA ndani ya Bunge anayeweza kujibu hoja hizo.

Hii inaonyesha namna gani Spika anavyotumia vibaya madaraka yake na kuonyesha udhaifu mkubwa wa kiuongozi.

Katika maelezo yake Spika ameiita barua aliyoandikiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA “Kipeperushi”. Hii ni dharau kubwa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini kilichosajiliwa kisheria.

Kuiita Barua rasmi kipeperushi inaendelea kuonyesha kiburi cha madaraka alichonacho Spika ambacho kinaendelea kumshushia hadhi mbele ya jamii.Sisi Baraza la Wanawake Chadema hatutakuwa tayari kuona viongozi wetu wakidhalilishwa na chama chetu kikidharauliwa na tena.

CHADEMA ina katiba yake na ndani ya katiba hiyo kuna miongozo, kanuni na taratibu kuhusu vikao na uendeshaji wa Chama. Kwa muktadha huo mkutano wa Baraza Kuu ambalo litapitia Rufani iliyokatwa na waliokuwa wanachama hao litakaa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Hata hivyo kukata rufani hakutengui maamuzi ya awali mpaka hapo rufani hiyo inaposikilizwa na maamuzi kutoka tofauti na maamuzi ya awali.

Kitendo cha Spika kutochukua hatua kwa kuwa kuna rufani imekatwa kupinga maamuzi ya awali linaonyesha namna gani alivyo na nia ovu juu ya jambo hili kwani anaelewa namna taratibu zilivyo na kwa makusudi ameamua kupindisha. si mamlaka ya Spika kuingilia mambo ya ndani ya chama.

Sisi Baraza la Wanawake Chadema tunapenda kuwahakikishia umma wa watanzania kwamba Chama chetu hakina mfumo dume kwa sababu, mosi, ndio chama chenye wajumbe wengi wa kamati kuu wanawake (9) kuliko vyama vingine vyote vya siasa kikiwemo Chama anachotoka Spika.

Katika kikao kilichofanya maamuzi ya kuwavua uanachama kulikuwa na wajumbe Wanawake 4 kwasababu wengine 5 walikuwa kwenye kundi la watuhumiwa.

Pili, kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Chama chetu ndio kilipitisha wanawake Zaidi ya 60 kugombea nafasi za ubunge wa majimbo kuliko vyama vingine vyote pengine kwenye ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati.

Leo hii Spika anajivika hadhi ya kuwa mtetezi wa wanawake huku akiwa amesahau kwamba ni yeye ambaye Bunge lililopita alikuwa mstari wa mbele kutweza haki za wanawake kiasi cha kuwafukuza bungeni wanawake ambao baadhi ni sehemu ya hao wanaoitwa wabunge 19 kushiriki vikao.

Spika Mtetezi wa wanawake, amekuwa akitumia askari wa kiume kuwaondoa Bungeni baadhi ya hao wanaoitwa wabunge 19 bila kujali jinsia zao

Wakati Halima na Esther walipopigwa na kuumizwa na askari Magereza Spika alionekana kufurahia tukio hilo. Hivyo ni unafiki mkubwa kujivika kilemba cha kujifanya ni mtetezi wa haki za wanawake.

Katika Bunge lililopita Chama cha Wananchi (CUF) kiliwavua uanachama wanachama wake 8 Wanawake waliokuwa Wabunge wa Viti Maalum na pale Spika alipoandikiwa barua aliwaondoa Bungeni mara moja.

Kwenye barua yake Spika alisema “Suala la kuwavua uanachama wanachama ni suala la utashi wa chama” sasa iweje leo Spika huyo huyo ajisahaulishe kuwa amewahi kuwavua ubunge wabunge 8 Wanawake kwa mara moja na leo hii kujifanya amegeuka ghafla kuwa mtetezi wa wanawake?

CADEMA imewahi kuwavua uanachama wabunge wake 4 wa kiume, je na huo pia ulikuwa mfumo jike kama anavyodai sasa hivi kwamba Chadema ina mfumo dume?.

Kikao kilichokaa na kuwavua uanachama wanaoitwa wabunge 19 ni kikao halali cha Kamati Kuu ya Chama ambacho kinaundwa na wajumbe wa jinsia zote na kina mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.

Wakati wa kusikilizwa kwa shauri la kuwavua uanachama, waliokuwa wanachama hao waliitwa kwa barua kuhudhuria kikao hicho ili waweze kusikilizwa lakini walikataa kuhudhuria hivyo shauri lao likasikilizwa bila wao kuwepo.

Kwa mujibu wa taratibu pale unapoitwa na ukakaidi kuhudhuria basi haki yako ya kusikilizwa inapotea hivyo shauri lako litasikilizwa upande mmoja (ex parte hearing).

Suala la maridhiano ni baina ya CHADEMA na Rais na kwa kutambua umuhimu wake CHADEMA ilimuandikia barua rais naye pia kwa kutambua umuhimu wake akakubakubali hivyo halina mahusiano yoyote na Spika.

Baraza la Wanawake CHADEMA tunaona kama Spika ana lengo la kuvuruga mazungumzo hayo huenda akawa na manufaa binafsi kuona nchi iliyogawanyika.

Pia tunapenda kumwambia Spika kwamba chama chetu hakina mgogoro wowote na hata pale kunapotokea mgogoro Katiba yetu inatuongoza namna ya kushughulika na utatuzi ndani ya chama.

Suala tunaloliongelea ni kuhusiana na waliokuwa wanachama wetu ambao tuliwavua uanachama kwa kosa la usaliti, uasi, ubinafsi na kugushi nyaraka za chama na ni jukumu la Spika kufanya kazi yake na sio kuwa mshauri wa namna ya kuendesha chama chetu.

Kwa maelezo yake,Spika amesema hapangiwi lini achukulie hatua suala la wanaoitwa wabunge 19. Spika anatakiwa atambue kwamba suala la utekelezaji wa Katiba si suala la utashi wa yeye kuamua ni lini achukue hatua. Hivyo tunamtaka Spika atekeleze matakwa ya kikatiba.

Taratibu za upatikanaji wa Wabunge wa Viti Maalum kwenye Chama huanzia ngazi ya chini kabisa kabla ya kufikia Kamati ya Utendaji na kisha Sekretarieti ya BAWACHA Baada ya hapo majina hupelekwa kwenye Kamati kuu ambayo hupitisha majina na kuyawasilisha Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Hivyo basi wanaoitwa wabunge 19 kujichagua na kujipeleka kwenda kuapa sio tu kwamba ni uvunjaji wa Katiba ya Chama Bali ni kiwango cha juu kabisa cha ubinafsi, uasi na usaliti.

Tunamtaka Spika atueleze wakati anawaapisha wanaoitwa wabunge 19, aliwaomba nakala ya Katiba, muhtasari nanyaraka nyingine anazozitaka Sasa hivi?.

Mwisho tunawaomba waandishi wa habari na umma tuendelee kumuuliza maswali ya msingi Spika kama tulivyoainisha hapo juu lakini kubwa likiwa ni kwanini anaendelea kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda? Je, anaweka mfano gani kwa wananchi.

Kwamba leo wanaweza kuvunja Katiba kama anavyofanya yeye kwa kiburi na wasichukuliwe hatua? Na je hizi hoja zake, zinailenga CHADEMA peke yake au ana maslahi binafsi na wanaoitwa wabunge 19?.

Tunazitaka Kamati za Utendaji za BAWACHA kila Jimbo kukutana hara kwa ajili ya kujadiliana hatua stahiki za kuchukua juu ya suala hili kwani sisi kama chama tutasimamia utekelezwaji wa Katiba ya JMT na hatutakuwa tayari kuona mtu yoyote, mwenye madaraka yoyote akiivunja katiba.

Baada ya kupokea mapendekezo kutoka Majimboni tutatoa maazimio ya hatua gani tutachukua kushinikiza utekelezaji wa jambo hili. Haijalishi kama wangekuwa wanaume au Wanawake kama ilivyo Sasa, pale Katiba itakapovunjwa tutasimama, kukemea na kuchukua hatua.

Tunamtaka Spika sio tu ajisifie ni miaka mingapi amekaa ndani ya bunge, bali aangalie kwenye kipindi cha uongozi wake ameacha alama gani chanya kwenye Taifa.

"Alama hizi lazima ziwe zile zinazotuunganisha kama nchi, kuleta Amani, haki na usawa kwa wote huku ikiweka misingi ya kuheshimu Katiba, Sheria na taratibu mbalimbali tulizojiwekea.
Kweli Jamaa anaringa utadhani yuko mbinguni
Anamtupia Nape madongo halafu anamwambia haina haja ya kujieleza
Hapo hapo anamwombea Msamaha....
labda ule unabii unaweza ukatimia
 
Back
Top Bottom