BAWACHA: Rais Samia asiwatambue Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama CHADEMA

na kama wanadai wamewavua uanachama huku hawataki kusikiliza rufaa zao sasa kinachowasumbua nini ? mmemvua uanachama siyo mwanachama wenu kinachowafanya waanze kutaka kumsumbua mama avunje katiba kuingilia mhimili wa bunge ni nini?
Una andika na kujikomenti mwenyewe?! Hii ni sawasawa na kufanya mastabesheni!
 
Kwanza waseme wanaitambua serikali iliyopo madarakani ilishinda kihalali uchaguzi wa 2020.
 
Unateseka sana ndugu. Wewe pambana na hali ya unyonge wako. Iache chadema ipambane na hali yake
 
"Msimamizi Mkuu wa Katiba na Sheria za nchi, ni Serikali. Mamlaka ya yote ya Serikali yapo mikononi mwa Rais. Hivyo, Msimamizi mkuu wa Utii wa Katiba na sheria ni Rais." ibara za 33 na 34 zipo wazi.

Kwa hiyo, Rais anayeona wazi sheria na katiba zikivunjwa na mhimili wa Bunge, huku pesa za umma zikichotwa na kuwalipa wavunjaji hao kwa Ubunge usio na baraka za Katiba halafu akafumbia macho; huyo Rais anakuwa amefeli na hajui Mamlaka yake ya Kikatiba katika Taifa hili.

Na kwa namna hiyo anakuwa ameshiriki uovu huo kwa njia ya kufumbia macho (omission) kinyume na Ibara ya 26 ya Katiba yetu.

Pia, baada ya CHADEMA kuwafukuza uanachama akina Mdee na kumuandikia Spika barua ya taarifa hiyo; ni msimamo wa kisheria kwamba Spika alitakiwa kuwaondoa Bungeni maramoja.

Suala la rufaa ni mkondo mwingine.

Na iwapo hatua ya Rufaa itawapa ushindi akina Mdee; ndipo Spika atawarejeshea ubunge wao.

Huwezi kuwakumbatia Covid 19 kwa dhana ya kusubiri uamuzi wa rufaa yao. Huu ni ujinga tu.

By the way, kila mtu anayeshiriki kuvunja sheria na kujinufaisha mishahara kinyume cha sheria (proceeds of crime), atawajibishwa tu.

Mtu pekee mwenye kinga kwa Katiba yetu ni Rais tu.

Hawa wengine wote wanajidanganya tu. Watawajibishwa kwa makosa ya jinai.

Adv. Livino Haule
 
Kuna wakati kuwaelewa Chadema ni lazima unywe pombe kwanza

Wote tunakumbuka mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 Chadema ilitangaza kuyakataa matokeo yaliyompa ushindi Dr Magufuli na mama Samia na wakadai hawamtambui Rais aliyetangazwa.

Leo Chadema hao hao wanamtaka Rais Samia aliyeshinda pamoja na hayati Magufuli 2020, asiwatambue wabunge wake wa viti maalumu walioko bungeni.

Pamoja na kwamba siyo kazi ya Rais Samia kutambua nani ni mbunge na nani siyo, Chadema waelewe wanatuchanganya wafuasi wao kwa namna wanavyoendesha mambo kienyeji.

Ramadhan Kardem!
Inakua ngumu sana kujibu au kukubali hoja ya aina hii kwa sabab ni ukweli ambao ukiusema unakua ni mtovu wa nidhamu na unapaswa uwajibishwe.
 
Mkuu nisaidie kunikumbushaCHADEMA walimpinga Rais Samia Suluhu Hassan lini? au baada ya uchaguzi upi?
 
Katika mkutano huo, Catherine Ruge amesema:

Tumeona kwenye vyombo vingi vya habari kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani anaenda kulihutubia Bunge tarehe 22 -04-2021 kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kwa rais wa JMT kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Dkt John Magufuli.

Kuelekea tukio hilo, sisi BAWACHA tuna jambo mahususi amabalo tungependa kuliwasilisha kwa Mh. Rais.

Jambo hilo ni uwepo wa wanaoitwa Wabunge 19 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa anakwenda kulihutubia Bunge hapo kesho, sisi wanawake wa CHADEMA tungependa atambue, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna watu wanaoitwa Wabunge 19 ambao wapo katika hilo bunge analotaraji kuhutubia, kinyume na katiba...

Hata hivyo, hao Wabunge 19 hawajakidhi vigezo kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwakuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameapa kuilinda katiba ya JMT na amekuwa akieleza hivyo mara kadhaa kwenye hotuba zake ambazo amekuwa akizitoa baada ya kuwa ameapishwa.

...atakuwa amevunja katiba kwa kuwaruhusu hao wanaoitwa Wabunge 19 kuhudhuria vikao vya bunge na kushiriki shughuli mbalimbali za bunge.


----- MAONI YANGU ----

BAWACHA hawaelewi maana ya kutofautisha mihimili​

Nimesikiliza maongezi ya Bawacha walivyokuwa wanaongea na waandishi wa habari Dodoma yaani inaonekana wazi kuwa hawajui ni nini wanataka au ninini wafanye.

Unapomwambia Rais anapoenda bungeni asiwatambue au aende kuongelea suala la hao wabunge ni kumkosea adabu mheshimiwa Rais.

Yaani mnamtaka avunje katiba hadharani ili baadae mje tena muanze kusema kavunja katiba; hivyo atakuwa anaingilia mhimili mwingine, hiyo haiwezekani.

tafuteni agenda nyingine siyo kumuingiza mama kwenye mifarakano ya taasisi yenu.

Asante

lowasa sio fisadi bana
 
Legacy ya mwendazake hiyo kapandikiza covid 19 bungeni kupitia Ndugai.Naona mataga wanajitoa ufahamu kuhalalisha uozo mwingine wa kazi ya mikono ya mwendazake.
 
Chadema kam walishawafukuza hawa bawacha wangakaa kimya tu sababu hawatambuliki, au chadema wangefanya kuchagua wabunge wengine wa viti maalum tuone itakuwaje!!
 
Habari zenu wana Jamvi.Nimekaa nawaza sana siasa za hapa nyumbani Tanzania,nawaza namna Siasa inavyotugeuza itakavyo,nawaza namna tunavyoimbishwa nyimbo mpya mpya kila siku na wanasiasa.Nimeenda mbali zaidi nikawaza kwanini watanzania tumekuwa na maswali sana juu ya uwepo wa wabunge feki bungeni?Kwann Chadema wamekaa kimya juu ya rufaa za hawa wabunge wanaodaiwa kuwa HEWA?Tukisema Ndugai,Mahera na Mbowe lao moja tutakuwa tumekosea wapi?

Wataalamu wa Siasa njooni mnisaidie.
 
Habari zenu wana Jamvi.Nimekaa nawaza sana siasa za hapa nyumbani Tanzania,nawaza namna Siasa inavyotugeuza itakavyo,nawaza namna tunavyoimbishwa nyimbo mpya mpya kila siku na wanasiasa.Nimeenda mbali zaidi nikawaza kwanini watanzania tumekuwa na maswali sana juu ya uwepo wa wabunge feki bungeni?Kwann Chadema wamekaa kimya juu ya rufaa za hawa wabunge wanaodaiwa kuwa HEWA?Tukisema Ndugai,Mahera na Mbowe lao moja tutakuwa tumekosea wapi?

Wataalamu wa Siasa njooni mnisaidie.
Walikubali kumtumikia mtu kwa shinikizo aliliwapa na kusaliti viapo vyao kwa chama Chao tena kwa kejeli na matusi unataka wasaidiae je.Zaidi ya wait kupambana na matunda ya usaliti .
 
Jiwe atake asitake tutamuongezea muda
WhatsApp Image 2021-04-20 at 12.07.26 PM.jpeg
 
Back
Top Bottom