BAWACHA: Rais Samia asiwatambue Wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama CHADEMA

Iboya2021

JF-Expert Member
Dec 1, 2020
1,618
1,481
Katika mkutano huo, Catherine Ruge amesema:

Tumeona kwenye vyombo vingi vya habari kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani anaenda kulihutubia Bunge tarehe 22 -04-2021 kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kwa rais wa JMT kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Dkt. John Magufuli.

Kuelekea tukio hilo, sisi BAWACHA tuna jambo mahususi amabalo tungependa kuliwasilisha kwa Mh. Rais.

Jambo hilo ni uwepo wa wanaoitwa Wabunge 19 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa anakwenda kulihutubia Bunge hapo kesho, sisi wanawake wa CHADEMA tungependa atambue, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna watu wanaoitwa Wabunge 19 ambao wapo katika hilo bunge analotaraji kuhutubia, kinyume na katiba...

Hata hivyo, hao Wabunge 19 hawajakidhi vigezo kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwakuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameapa kuilinda katiba ya JMT na amekuwa akieleza hivyo mara kadhaa kwenye hotuba zake ambazo amekuwa akizitoa baada ya kuwa ameapishwa.

...atakuwa amevunja katiba kwa kuwaruhusu hao wanaoitwa Wabunge 19 kuhudhuria vikao vya bunge na kushiriki shughuli mbalimbali za bunge.

----- MAONI YANGU ----

BAWACHA hawaelewi maana ya kutofautisha mihimili​

Nimesikiliza maongezi ya Bawacha walivyokuwa wanaongea na waandishi wa habari Dodoma yaani inaonekana wazi kuwa hawajui ni nini wanataka au ninini wafanye.

Unapomwambia Rais anapoenda bungeni asiwatambue au aende kuongelea suala la hao wabunge ni kumkosea adabu mheshimiwa Rais.

Yaani mnamtaka avunje katiba hadharani ili baadae mje tena muanze kusema kavunja katiba; hivyo atakuwa anaingilia mhimili mwingine, hiyo haiwezekani.

tafuteni agenda nyingine siyo kumuingiza mama kwenye mifarakano ya taasisi yenu.

Asante
 
Na kama wanadai wamewavua uanachama huku hawataki kusikiliza rufaa zao sasa kinachowasumbua nini? Mmemvua uanachama siyo mwanachama wenu kinachowafanya waanze kutaka kumsumbua mama avunje katiba kuingilia mhimili wa bunge ni nini?
 
RAIS NI SEHEMU YA BUNGE......
Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) ya Katiba na lina sehemu mbili, ambazo ni Rais na Wabunge.
siyo kweli bunge lina jitegemea na taasisi ya rais inajitegemea huwezi rais ukaanza kumpangia bunge mambo ya kufanya utakuwa umenajisi bunge muacheni mama msimvunjishe sheria
 
na kama wanadai wamewavua uanachama huku hawataki kusikiliza rufaa zao sasa kinachowasumbua nini ? mmemvua uanachama siyo mwanachama wenu kinachowafanya waanze kutaka kumsumbua mama avunje katiba kuingilia mhimili wa bunge ni nini?
Unapo hukumiwa kifungo uka kata rufaa. Unaisikilizia rufaa ukiwa magereza au una isikilizia ukiwa huru?
 
siyo kweli bunge lina jitegemea na taasisi ya rais inajitegemea huwezi rais ukaanza kumpangia bunge mambo ya kufanya utakuwa umenajisi bunge muacheni mama msimvunjishe sheria
KATIBA INASEMA HIVYO ,Wewe unasema "siyo kweli".
Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) ya Katiba na lina sehemu mbili, ambazo ni Rais na Wabunge.
 
KATIBA INASEMA HIVYO ,Wewe unasema "siyo kweli"..............
Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) ya Katiba na lina sehemu mbili, ambazo ni Rais na Wabunge.
je ni sheria kwa rais kuingilia majukumu ya maamuzi ya bunge? yeye ni signatory wa yanayopitishwa bungeni ndiyo ushiriki wake siyo kuingilia maamuzi ya bunge
 
Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) limetaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kuulizwa sababu za wanawake 19 waliofukuzwa uanachama wa chama hicho kuendelea kuwa wabunge wa viti maalum.

Pia limeviomba vyombo vya habari vikiripoti habari kuhusu wanawake hao wakiongozwa na Halima Mdee, kutoandika kuwa ni wanachama wa Chadema kwa kuwa wameshafukuzwa.

Novemba 27, 2020 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza Mdee na wenzake 18 kuvuliwa uanachama wa chama hicho kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Waliovuliwa uanachama ni Mdee, Esther Matiko, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Asia Mohammed, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.
Kabla ya kutangaza uamuzi huo, Mbowe alitaja hatua nyingine tatu ambazo kamati kuu imezichukua ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa miongoni mwao waliokuwa viongozi wa Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha) na lile la wanawake (Bawacha) na kuagiza mchakato wa kujaza nafasi zao uanze mara moja.

Akizungumza leo Jumatano Aprili 21, 2021 kwa niaba ya makamu mwenyekiti wa baraza hilo, mweka hazina wa Bawacha, Catherine Ruge aliwaomba wanahabari kumuuliza Ndugai wabunge hao wanatoka chama gani cha siasa.

“Hivi hamuwezi kujiuliza kwamba hata hapo walipo wanawakilisha halmashauri zipi, maana mbunge wa viti maalumu lazima uwe na halmashauri lakini wao wapo tu na hakuna mahali popote wanapowajibika zaidi ya maslahi yao,” amesema Ruge.

Kuhusu rufaa waliyokata amesema ni haki yao na kuongeza kuwa walipaswa kuwa wamejiondoa lakini kutofanya hivyo ni kukaidi maagizo ya chama ambalo ni kosa jingine.

MWANANCHI
 
Sasa kama wameshawafukuza uanachama kinachowasumbua kuwa fuatafuata ni nini? waacheni waendelee na mambo yao nyie hamuwatambui mnataka wao wawatambue nyie kama kina nani? mnawapa umaarufu hebu kaeni bila kuwaongelea muone kama kuna tatizo shida mnayo nyie mnaowaongelea kila siku mmeshawafukuza basi.
 
Nimesikiliza maongezi ya Bawacha walivyokuwa wanaongea na waandishi wa habari Dodoma yaani inaonekana wazi kuwa hawajui ni nini wanataka au ninini wafanye.

Unapomwambia Rais anapoenda bungeni asiwatambue au aende kuongelea suala la hao wabunge ni kumkosea adabu mheshimiwa Rais.

Yaani mnamtaka avunje katiba hadharani ili baadae mje tena muanze kusema kavunja katiba; hivyo atakuwa anaingilia mhimili mwingine, hiyo haiwezekani.

tafuteni agenda nyingine siyo kumuingiza mama kwenye mifarakano ya taasisi yenu.

Asante

========

Katika mkutano huo, Catherine Ruge amesema:

Tumeona kwenye vyombo vingi vya habari kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani anawendakulihutubia Bunge tarehe 22 -04-2021 kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa kwa rais wa JMT kufuatia kifo cha mtangulizi wake, Dkt John Magufuli.

Kuelekea tukio hilo, sisi BAWACHA tuna jambo mahususi amabalo tungependa kuliwasilisha kwa Mh. Rais.

Jambo hilo ni uwepo wa wanaoitwa Wabunge 19 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa anakwenda kulihutubia Bunge hapo kesho, sisi wanawake wa CHADEMA tungependa atambue, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna watu wanaoitwa Wabunge 19 ambao wapo katika hilo bunge analotaraji kuhutubia, kinyume na katiba...

Hata hivyo, hao Wabunge 19 hawajakidhi vigezo kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwakuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameapa kuilinda katiba ya JMT na amekuwa akieleza hivyo mara kadhaa kwenye hotuba zake ambazo amekuwa akizitoa baada ya kuwa ameapishwa.

...atakuwa amevunja katiba kwa kuwaruhusu hao wanaoitwa Wabunge 19 kuhudhuria vikao vya bunge na kushiriki shughuli mbalimbali za bunge.
Tuliambiwa kuwa kuna Mhimili mmoja umejichimbia zaidi kuliko mwingine. Pesa za matumizi ya mihimili mingine zinatoka kwenye huo "mhimili mkuu" hivyo kuna haja ya mhimili huo kuona kuwa pesa zinatumika kwa mujibu wa sheria, na katiba ndiyo sheria mama ambayo inasema mtu hawezi kuwa mbunge mpaka awe mwanachama wa chama cha siasa.

Anaweza asiseme moja kwa moja lakini anaweza kushauri/kusisitiza utii wa katiba katika nchi.
 
KATIBA INASEMA HIVYO ,Wewe unasema "siyo kweli"..............
Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania lilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 62(1) ya Katiba na lina sehemu mbili, ambazo ni Rais na Wabunge.
Rais ni sehemu ya Bunge, siyo kiongozi wa Bunge.
 
siyo kweli bunge lina jitegemea na taasisi ya rais inajitegemea huwezi rais ukaanza kumpangia bunge mambo ya kufanya utakuwa umenajisi bunge muacheni mama msimvunjishe sheria
Wewe usiwe iboya kama jina lako. Katiba inatamka wazi kuwa bunge lina sehemu mbili yaani Rais na Wabunge. Ukikiri ujinga wako utapungukiwa nini?
 
Back
Top Bottom