BAWACHA kutinga Bungeni tarehe 10/05/2021 kuwatimua Wabunge 19 waliopora nafasi za CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,667
Bawacha wamepanga kwenda Bungeni Dodoma tarehe 10/05/2021 kudai nafasi zao 19 za Ubunge zinazokaliwa kwa mabavu na akina Halima Mdee na wenzake .

Mwenyekiti wa Bawacha wilaya ya Chato bi Husna amesema maandamano yao jijini Dodoma kuelekea Bungeni hayatakuwa na kikomo hadi suluhisho lipatikane.

BAWACHA wamesema safari yao ni ya amani.

Chanzo: ITV habari
 
Kama wanajielewa wafanye maandamano kwenda ofisi yao kuu pale ufipa kushinikiza uongozi wa juu wa chama kuchukua hatua la tuwahesabu kuwa wana chuki na wivu kwa wanawake wenzao.

Isitoshe kumekuwa na matumizi yasiyo halali ya ruzuku, lakini hawakuchukua hatua kama hiyo ya kuandamana kudai maelezo.

Hakika jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.
 
Waachane na siasa za maandamano. Kwa namna Rais wa awamu ya 6 anavyo operate (so far) ni jambo linaweza kumalizwa kwa mazungumzo tu.
 
Haya maandamano nadhani yamechelewa na labda yangefaa zaidi mwezi Nov mwaka 2020.

Hii approach kwa sasa sio sahihi na ni bora turudi kwenye basics: Kwanini CHADEMA wasiteue wabunge 19 na kupeleka taarifa ofisi za NEC kwa kuwa wale “walifoji” nyaraka na kimsingi hawatambuliki?

Kwanini rufaa ya akina Mdee haisikilizwi na Baraza Kuu kubariki kutimuliwa kwao? Hivi kipi ni rahisi zaidi on paper kati ya kuratibu maandamano mpaka Bungeni au kuitisha hilo Baraza?
 
Back
Top Bottom