Bavicha yatoa Tamko kuhusu Wanafunzi waliyofukuzwa vyuo vikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bavicha yatoa Tamko kuhusu Wanafunzi waliyofukuzwa vyuo vikuu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Henry Kilewo, Dec 17, 2011.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  [FONT=&quot]TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUFUKUZWA .[/FONT]
  [FONT=&quot]UTANGULIZI:[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa miaka ya hivi karibuni Vyuo mbalimbali vimekua na tabia ya kuwafukuza ama kuwasimamisha masomo wanafunzi wanaoendelea na masomo kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini mwetu kutokana na mashinikizo mbalimbali kutoka kwa viongozi wa kiserikali kwa kisingizio kuwa wanafunzi hawa wanafanya siasa vyuoni.[/FONT]
  [FONT=&quot]Itakumbukuwa kuwa migomo na maandamano ya wanafunzi kwa vyuo vikuu hapa nchini haijaanza pale mfumo wa vyama vingi uliporuhusiwa kuanza mwaka 1992 ,bali migomo na maandamano haya yamekuwepo tangu kuanzishwa kwa vyuo hivyo. [/FONT]
  [FONT=&quot]Mathalani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa na historia ya migomo na maandamano ya mara kwa mara tangu kuanzishwa kwake , na hivyo dhana ya kuwa wanafunzi wanagoma kutokana na misukumo ya kisiasa sio sahihi hata kidogo bali ni mbinu ya watawala kujaribu kuficha madhaifu yao .[/FONT]
  [FONT=&quot]Wanafunzi hawa wamekuwa wakigoma kutokana na serikali ya CCM kuendesha mambo yake kibabe na kwa dharahu ya hali ya juu ambapo imefanya elimu kuwa Privilage na si haki kwa watanzania.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa mantiki hiyo basi, kutokutendewa haki kwa wanafunzi hawa na serikali yao, kukosekana kwa miundombinu bora ya kusoma na kujifunzia, wanafunzi hawa kunyanyaswa na watawala wa vyuo hivyo, kukosekana kwa mikopo kwa wakati muafaka, serikali kuingilia uendeshaji wa vyuo ,serikali kuvunja serikali za wanafunzi bila kutoa sababu za kimsingi na sababu nyingine mbalimbali ndio chanzo cha vurugu na migomo vyuoni.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hivyo basi , kutokana na sababu tajwa hapo juu Baraza la Vijana na CHADEMA (BAVICHA) tunatamka wazi kuwa kitendo cha Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam, Dodoma na Muhimbili kuwafukuza wanafunzi kwa ujumla wake zaidi ya 100 ni kitendo cha uonevu kwa wanafunzi hawa na kamwe hakivumiliki hata kidogo na haswa ikizingatiwa kuwa ni watoto wa watu masikini na ambao kimsingi wanajilipia ada wenyewe kwani wanakopa na baada ya muda watapaswa kulipa fedha hizo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa nini tunapinga uamuzi huu wa kuwafukuza wanafunzi vyuoni;[/FONT]
  [FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot]Ni kinyume na Tamko la Ulimwengu la mwaka 1990 la uhuru wa kitaaluma (Academic Freedom) ambalo tulisaini mnamo mwezi April tarehe 29 hapa Dar Es Salaam , linasema wazi kuwa ni lazima Vyuo vijiendeshe kwa uhuru kamili bila kuingiliwa na serikali .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot]Kufukuzwa kwa wanafunzi hawa ni utekelezaji wa Maazimio ya vikao vya CCM vilivyofanyika na haswa vile vya Halimashauri Kuu ambavyo vimetoa maelekezo mbalimbali kwa Serikali juu ya kuwachukulia hatua wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamekuwa wakiikosoa serikali waziwazi , na hata wahadhiri ambao wamekuwa wakitumia taaluma zao kwa uwazi na kusema juu ya mapungufu ya serikali wachukuliwe hatua ya ama kufukuzwa kazi na au ajira zao kusitishwa. Hivyo hii ni muendelezo wa utekelezaji wa maamuzi hayo.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot]Kuvunjwa kwa taasisi za wanafunzi na haswa serikali za wanafunzi , hii ni kutokana na tangazo la serikali kuhusiana na kanuni za serikali za wanafunzi lililochapishwa tarehe 12/06/2009 ambalo ni tangazo namba 178 lilivunja rasmi nguvu za serikali za wanafunzi kuanzia na muundo wake, majukumu yake na hata jina la vyeo husika kwa kufuta rasmi cheo cha urais kwenye serikali za wanafunzi. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mara baada ya taasisi hizi kuvunjwa wanafunzi wamekosa chombo cha kuwasilisha matatizo yao kwa menejimenti za vyuo husika.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot]Wanafunzi waliofukuzwa vyuoni hawajatendewa haki kwani hawajapata fursa hata ya kusikilizwa na kujitetea mbele ya vyombo husika vya vyuo hivyo, na wakati huo huo walikuwa wanamadai ya kimsingi kabisa .Hivyo hii ni kinyume kabisa haki za kimsingi (Natural Justice).[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot]Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi, Dr Shukuru Kawambwa amekuwa na tabia ya kuingilia taasisi za elimu ya juu , kwa mfano mnamo tarehe 22/06/2011 aliandika dokezo sabili kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitoa maelekezo kwa Bodi ya mikopo kusimamisha mikopo kwa Wanafunzi kwa ajili ya Mafunzo kwa vitendo hadi hapo uongozi wa UDOM utakapoamua nani alipwe na nani asilipwe. Pamoja na ukweli kuwa wanafunzi wana mikataba na bodi ya mikopo bado waziri anaweza kuagiza mikataba hiyo kuvunjwa na bodi husika. Na hata kitendo cha kuwafukuza wanafunzi hawa ni muendelezo wa serikali kuingilia vyuo hivi na utendaji wake.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]6. [/FONT][FONT=&quot]BAVICHA , tunapinga na kulaani tamko lililotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuwa vijana hawa wasipate fursa yeyote ya kudahiliwa na vyuo vingine hapa nchini , hii ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa kila mtu ana haki ya kujiendeleza kwa kadiri ya uwezo wake. Hivyo kitendo hiki kamwe hakivumiliki kwa mtu mmoja kuwa na mamlaka ya kuwanyima wengine fursa ya kupata elimu kwa sababu ambazo hazielezeki na ni vitisho visivyovumilika hata kidogo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hivyo basi BAVICHA tunaitaka serikali na management zake za vyuo ziache tabia ya kutibu matokeo au matawi ya matatizo vyuoni humo kwa kukimbilia kufukuza wanafunzi bali kutatua kiini cha matatizo. [/FONT]
  [FONT=&quot]Pia tunawahimiza vijana wote wanaosoma katika vyuo , Sekondari ,taasisi mbalimbali za kitaaluma, wanaharakati na wadau wa elimu na maendeleo ya kweli hapa nchini kuungana pamoja ili kuupinga utamaduni huu mpya wa kuwanyanyasa wanafunzi wa Vyuo Vikuu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Jambo hili likiachwa ili liendelee bila kuchukua hatua litaathiri sana taifa kwani watawala wanataka kutengeneza taifa la watu waoga na wasiokuwa na uwezo wa kuhoji masuala mbalimbali.[/FONT]
  [FONT=&quot]Sambamba na haya, kuna wanafunzi wengi waliopaswa kuanza mwaka wa kwanza wa masomo mwaka huu lakini wameshindwa kufany hivyo kwa kile kinachoelezwa na bodi ya mikopo kutokua na bajeti ya kuwakopesha. Wanafunzi hawa wamesharudi makwao.[/FONT]
  [FONT=&quot]Majibu haya ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi hawa ni kielelezo cha serikali ya CCM kutokujali wala kuthamini elimu na kwamba anasa na kutapanya mali za umma ndio kipaumbele chake. Serikali haina fedha za kusomesha wanafunzi lakini ina fedha za kulipa posho kwa viongozi wake wachache. Katika hili, BAVICHA tunaitaka serikali itafakari upya swala la elimu na hata sera ya elimu ya juu hapa nchini[/FONT]
  [FONT=&quot]Tamko hili limetolewa na;[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]…………….[/FONT]
  [FONT=&quot]John Heche[/FONT]
  [FONT=&quot]Mwenyekiti wa BAVICHA TAIFA.[/FONT]
   
 2. P

  Pure nomaa JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 1,051
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  Hii ndo serikali ya posho kwanza,elimu baadaye Poleni sana wanafunzi mliofukuzwa tuko pamoja ALUTA CONTINUE.
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  UVCCM wako wapi? Zainabu Kawawa, Malisa, Ole Millya na Shigela lile tamko lenu la kuiagiza serikali liliishia wapi? Au mlikuwa mnachanhamsha jukwaa
   
 4. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ahsante BAVICHA. The government is too funny, I'm not complaining anymore I'm just laughing :lol:
   
 5. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mimi naunga mkono kufukuzwa kwa wanaohatarisha amani na Usalama nchini ,lakini nina neno moja kwa nini serikali inatumia nguvu zote kuwafukuza Wanafunzi kwa kitendo cha kuvunja Sheria za nchi wakati wapo watu wanafahamika kabisa wameiba mali za umma kupitia kagoda, EPA, RICHMONDI lakini wanawambia wapime wajiuzulu wenyewe??

  Hapa kuna haki???

  JK ulisema huwajui wamiliki wa DOWANS Lakini Lowassa katuambia kuwa wewe ulimupa maelekezo yote juu ya wizi wa Richmond na baadaye Lowassa kasema ndiye aliyekuletea jina la Rostam Aziz katika sakata la wizi wa DOWONS . Hapa tunafahamu kuwa hata mchakato wa DOWANS kuishitaki gvt
  na kudai 111bils unajua sasa kati ya Wanafunzi na wewe nani anahatarisha Usalama wa Nchi??

  Ni bora ukawalejesha Wanafunzi haraka na kuwaongezea Posha badala ya kuwahonga Wabunge!!!
   
 6. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tnx BAVICHA!
   
 7. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hongereni sana BAVICHA kwa Tamko lenye Mashiko kwa Mustakabali wa nchi yetu japo mimi siyo mwanachama wenu.
   
 8. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #8
  Dec 17, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thnx sana BAVICHA, hii ya wanafunzi kufukuzwa imeniuma sana, alafu tunahadhisha eti miaka hamsini ya uhuru!!! uhuru gani huu? uhuru wa nani? uhuru wa watanzania? Wezi wa EPA, Richmond, Dowans, Meremeta, Kagoda wapo wapi?
  Mimi nafikiri ni uhuru kwa Mafisadi wote, C.C.M na watoto wao kina Rtz1, Nape, Shigela, Malisa.
  Sio uhuru wa watanzania huu, uhuru wetu tunausubili kwa hamu siku ikifika, na ipo karibu yaja.
   
 9. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh, na nyie BAVICHA mmezidi na matamko. Tunataka vitendo bana. Injinieni maandamano ya vyuo kudai haki za hawa washikaji sio kuongea maneno tuuu.
   
 10. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,209
  Likes Received: 268
  Trophy Points: 180
  Ilitawa lyaho lihwanile ni mutukha..... Jina lako limefanana na la gari.... Ha ha ha natania tu Mkuu, ila naunga mkono ipo haja ya kwenda mbele zaidi ya matamko
   
 11. n

  nyangwe Senior Member

  #11
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  well said BAVICHA, please could u take more action eg going to court ( kuweka zuio la mahakama) if possible
   
 12. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,472
  Trophy Points: 280
  inasikitisha sana kuona masikini wameandikiwa no loan! Wanye nazo 90 asilimia.
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  BAVICHA hamuwezi kutoa msaada wa kisheria kwa hawa wanafunzi??
   
 14. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Hili ndio niliokuwa nalisubiri kutoka Bavicha...ni Tamko la 20 kutoka kwa Heche lisiokuwa na tija kwa Taifa
   
 15. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kwako tamko la tija ni lipi? Au Lile lililotolewa PWANI na kina Riz1 kwamba rais ajaye hatotoka Kaskazini? The end is comin, moto hauzimwi kwa kufunika na majani makavu....
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Sasa mtawasaidiaje hao wanafunzi wapelekeni India wakasome ...nyie ndio mmeatuma wafanye maandamano wasaidieni:bange:
   
 17. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  u
  Nadhani mijitu mingine inafikiri kwa makalio. Embu kawaambie masaburi wenzako waje na tamkoi kenye tija basi! hata kama lingekua tamko la laki moja, BAVICHA imeshasema na imejiexpressitself na tumewaona wanauchungu na vijana wenzao.

  Kawaambie masaburi wenzako waje na tamko la kulaani vikao vya baba na mama zao kuelekeza wanafunzi hawa wafukuzwe we panya.
   
 18. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #18
  Dec 17, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Angalia akili yako ilivyo fupi kama pua yako! Masaburi utayajua tu.
   
 19. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #19
  Dec 17, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Rtz,
  Nimeshakwambia mara nyingi sana kwamba sabuni ya Omo si ya kuogea, mwenzetu unang'ang'ania! Ona sasa uso wako unavyobabuka!
   
 20. k

  kipinduka Senior Member

  #20
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  c muanzishe chuo kama mnaona mnaonewa hata cc 2nasoma lazime ufuate taratibu,heche acha ku2mia upupu kwenye ukwel mbona unaudhalilisha ualimu au
   
Loading...