BAVICHA yaisulubu serikali ya Tanzania mbele ya chancelor Angela Merkel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BAVICHA yaisulubu serikali ya Tanzania mbele ya chancelor Angela Merkel

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Scolari, Oct 6, 2012.

 1. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Deogratias Munishi ameiangushia kombora kali serikali ya Tanzania mbele ya Chancela wa Ujerumani Angela Merkel alipokua akihutubia mkutano mkuu wa vijana wa CDU uliofanyika mjini Rostock Jana.

  Katika hotuba yake, Munishi alionyesha jinsi serikali inavyotumia vyombo vyake kukandamiza demokrasia ya vyama vyingi ikiwa ni pamoja vyombo hivyo kuua raia hovyo huku akitoa takwimu za mauji yalifanywa kwenye shughuli halali za CHADEMA ikihusisha tukio la kikatili ya mauaji ya mwandishi wa habari mwezi Septemba.

  Akihitimisha, Munishi aliitaka serikali ya Ujerumani inayotoa misaada mingi kwa serikali ya Tanzania kuitaka serikali hiyo kuheshimu utawala wa sheria, haki za msingi za binadamu na misingi ya Demokrasia.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  "Rostock" pamewahi kutokea nini kwenye mji huu, manake hili jina lilitumika kutambulisha mtu mwenye roho mbaya.

  Nikirudi kwenye topic, naona serikali ya ccm itapasuka msamba si muda mrefu, kwani inahitaji sana kuungwa mkono na ujerumani kwenye mgogoro wa mpaka na malawi, ukizingatia kuwa uingereza tayari inaegemea malawi. Sasa haya mashtaka mbele ya donor yataipagawisha ccm iliyobakiza mbinu moja tu kujiweka madarakani.
   
 3. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #3
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Nafasi yoyote inayo patikana siyo ya kueleza wema wa kuchonga bali lazima iwe kueleza ukweli na uhalisia wa siasa za Tanzania kwa sasa! Wafadhiri lazima wajue kuwa sehemu ya fedha zao zinatumika kuuwa raia wasio kuwa na hatia.
   
 4. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Pesa za misaada wanazotoa wadhungu huibwa na hao mafisadi wa ccm na kutunzwa kwenye bank za uswis na europe.
  Na mafunzo ,vifaa wanavyotoa kwa jeshi la polisi ni kwa ajili ya kuua raia wasiyo na hatia
   
 5. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mafisadi wamejaa hapana pa kutokea
   
 6. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mbona stori haina collaboration na heading ilikuwa hotuba rasmi ya bavicha au huyu munisi? ni yupi huyu ni yule aliyekuwa golkipa zamani? tuwekeeni na source na habari picha maana tusiwape mwanya hawa wenzetu wapate la kuongea hawachelewi kusema ooh si kweli na ije sasa story full wazee
   
 7. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 8. Mdutch

  Mdutch JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo patamu.!
  Hapa hawajaja vilaza wa CCM wanaodaigi CHADEMA inapewa pesa na Ujerumani kuleta fujo Tanzania. Sasa mmechongewa kwa anayewapaga pesa. Mtalijua jiji mwaka huu. Baba anatwanga ile mbaya, watoto nao wanakandamiza kwa kwenda mbele!

  Viva Bavicha , Viva Munishi.
   
Loading...