BAVICHA wilaya ya Geita tunasema poleni bodaboda wote wa Geita

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Kwa niaba ya Baraza la vijana chadema (Bavicha) wilaya ya Geita ninatuma salamu za rambi rambi kwa Mwenyekiti wa Boda Boda Mkoa wa Geita Bw Ndagiwe Carlos, kwa kuondokewa na Mwanachama wako Bw Samweli John wa kituo cha US BONY mtaa wa Balenge ambae amekufa akiwa Kwenye harakati za kutafuta riziki ya kila siku.

Mimi Kama msemaji wa Baraza kwa ngazi ya wilaya Bavicha tumeipokea kwa masikitiko taarifa hiyo kwani tumepoteza Nguvu kazi ya wilaya yetu ya Geita na taifa letu kwa ujumla vile vile tumeipoteza nguvu ya mabadiliko Kama isemavyo kauli mbiu yetu ya Vijana.

Baraza tumeamua kuungana nanyi na kuwapa pole kwa msiba huu mzito wa kijana wetu, Ninaomba ufikishe salamu za Baraza kwa Boda boda wote pamoja na familia ya Marehemu uwaambie vijana wa chadema tuko nao kwenye wakati huu mgumu.

Wito wangu kwa vijana wanaotumia vyombo vya moto katika wilaya yetu ninawaomba mvitumie kwa tahadhali na umakini ili kuokoa Majeraha na vifo ambavyo vinaweza kuepukika maana chadema tumaumia sana kupoteza vijana wetu kila mara, Nahitimisha kwa kusema poleni sana Boda Boda poleni sana Geita kwa kuondokewa na kijana wetu mpendwa, chadema tunawapenda Sana.

Asanteni Sana.

Ni Mimi Mhere Mwita,
M/Kiti wa Bav (W) Geita,
Tarehe 16/05/2018.
FB_IMG_1526482320594.jpg
 
Poleni sana. Angalizo, Huo ni msiba sio siasa msije na nyie mkaleta siasa msibani kama wale wenzenu was kijani kibichi
 
Back
Top Bottom